Katika hali isiyokuwa ya kawaida nyama ya fisi imegeuka kitowewo kwa
wananchi na wakazi wa vijiji vya Bukana na Mori Wilayani Rorya Mkoani
Mara baada ya kunyanganyana nyama hiyo hivi karibuni jambo ambalo
limewaacha watu wengi vinywa wazi na kujiuliza kuwa nyama hiyo ni kwa
ajili ya chakula au matumizi mengine.
Kitendo hicho
kimewashangaza baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo kwani
lilikuwa la kustaajabisha kwa binadamu kuchukua nyama za mnyama huyo
ambaye anahusishwa
na masuala ya
kishirikina katika maeneo mengi ya nchi ya Tanzania ambapo wengine
waalipoulizwa kwa nini wanafanya hivyo wamedai wanaenda kula huku
wengine wakidai ni dawa.
Baadhi ya sehemu za viungo zilizokuwa zikigombaniwa ni mkia, sehemu za
siri pamoja na mifupa yake hali ambayo imewafanya wengine kukosa na
kuacha vipande vya ngozi, utumbo na kichwa.
Jacob Nyamu ni shuhuda wa tukio hilo akiongea kwa njia ya simu na CLEO NEWS anaeleza juu ya Tukio hilo ambalo mpaka sasa limewacha watu vinywa wazi
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena