Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au kutengenezwa supu. Mbegu zake zinaweza kusagwa na kupata unga unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji, chapati na maandazi. MAZINGIRA Mchicha unaweza kulimwa karibu katika aina yeyote ya hali ya hewa na kwenye udongo wa aina yeyote ili mradi usituamishe maji. Udongo wenye rutuba nyingi unafaa zaidi kwa ustawishaji wa zao hili. AINA Kuna aina nyingi za mchicha; zifuatazo ni aina zinazostawi hapa nchini:- Mchicha Mweupe Aina hii ina majani marefu yenye rangi ya kijani ya kupauka. Huvunwa kwa kung'oa na huuzwa sana sokoni. Mchicha Mpana Ni ule ambao ni mnene na una majani mapana na yenye rangi ya kijani kibichi. Huweza kuvunwa kwa kurudiwarudiwa Mchicha Mwembamba Huu ni mdogomdogo na unaota shambani kama gugu. Majani yake ni madogo na huchanua mapema. Mchicha wa Unga Mchicha huu huwa mwekundu unapokuwa mdogo na hukua haraka. Hutoa mbegu nyingi ambazo zinaweza kusagwa unga, ambao unaweza kutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile, uji na maandazi. Majani yake hupikwa kama mboga au hutengenezwa supu. KUTAYARISHA SHAMBA Tayarisha shamba mwezi mmoja kabla ya kupanda. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuongeza rutuba ya udongo. Mbolea hizi pia hufanya udongo ushikamane vizuri na kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu. Weka kiasi cha ndoo moja yenye ujazo wa lita ishirini katika eneo la mita mraba mmoja. Changanya vizuri mbolea hii na udongo. Wiki mbili kabla ya kupanda laininsha udongo na sawazisha udongo. KUPANDA Kuna niia kuu mbili za kuoanda mchicha, Kupanda mchicha moja kwa moja shambani na kuotesha miche kwanza kwenye kitalu. Kupanda Moja kwa Moja Shambani Mbegu hupandwa moja kwa moja kwenye shamba la kudumu na baadaye mimea hupunguzwa na inayobaki huachwa katika nafasi ya sentimita 15 hadi 23. Mbegu huweza kupandwa katika sesa au matuta. Kiasi cha kilo moja hadi mbili za mbegu kinatosha kuotesha katika eneo la hekta moja. Ili kuepuka mlundikano wa mbegu sehemu mmoja, changanya mbegu na mchanga kwa kiasi kinacholingana kabla ya kumwaga shambani. Kisha mwaga na funika kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Tandaza nyasi kavu na mwagilia maji. Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tatu mpaka tano na baada ya kuota ondoanyasi. Kuotesha Miche Kwenye Kitalu Kutayarisha Kitalu: Sehemu itakayooteshwa mbegu inatakiwa iwe laini na yenye rutuba ya kutosha. Hivyo baada ya kulima lainisha udongo kwa kupigapiga mabonge makubwa. Kisha tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha debe moja au mbili katika kila eneo la mita mraba moja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri, kisha sia mbegu zilizochanganywa na mchanga kwenye mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15. Baada ya kusia, funika mbegu kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Weka matandazo na mwagilia maji. Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota. Baada ya siku 4 mpaka 6 ondoa matandazo na endelea kumwagilia maji. Sikiliza hapa zaidi >>>>>>
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena