Swali hili limekuwa kwenye vichwa vya wanasayansi hasa upande wa materialistic, kwenye mfulululizo wa mabandiko haya nitajibu swali hilo.
Kama binaadam wenye uhuru na maamuzi kamili kuna viumbe wengine wanao ishi pamoja nasi wenye uhuru na maamuzi kamili kama sisi na kwa milenia nyingi viumbe hao wamekuwa washiriki wetu wakubwa, kwani wana sifa moja kuu kama tuliyo nayo sisi, inayo tutofautisha na viumbe wengine wote, sifa ya Uhuru, sisi na wao hatuishi kwa kufuata silka zetu kama waishivyo viumbe wengine, tu huru.
Kila mtu anauliza, Tuko peke yetu?
Ikiwa basi kuna uwezekeno wowote wa binaadam kutawaliwa na kiumbe kingine asiye kuwa yeye basi kiumbe huyo atakauwa ni huyu mshirika wake mwenye sifa kama zake. Jini.
Mchoro huu kwenye asasi za siri unafahamika kama 'head of mendes' au kichwa cha shetani, kila unacho kiona hapo kinayo maana na tafsiri yake.
Kwa maelfu ya miaka maisha ya binaadam yamekuwa yaakiathiria kwa njia moja ama nyingine na Majini au Mashetani. Katika jamii yoyote duniani wanafahamika kwa majina mbali mbali, katika dini zote duniani wametajwa kuwepo kwao, na katika maendeleo makubwa ya sayansi ya sasa hasa sayansi ya nyota na safari za binaadam kwenda angani mchango wao ni mkubwa na unakubalika, sababu kwa muda wote wa historia ya binaadam huyu ndiye amekuwa mshirika wake.
Mendes na alama nyingine zenye tafsiri maalum ndani ya asasi za siri wakiwemo freemason.
Binaadam ametawalishwa dunia na Muumba wake, lakini kati ya vitakavyo kuwa chini yake moja wapo ni huyu mshirika wake mwenye uwezo unao karibiana kabisa na wa kwake na ambaye anaifahamu dunia vyema kuliko anavyoifahamu binaadam mwenyewe kwani wao, majini walikuwepo hapa duniani kabla ya Binaadam. Kuja kwa wanaadam kuliwanyang’anya majini kilichokuwa chao, Dunia. Wao ndiyo waliokuwa watawala lakini tena kutokana na uovu wao ameletwa mtawala mwingine aliyebora kuwashinda wao, atakaye fanya ile kazi iliyowashinda.
Hadithi maarufu ya jini likitoka kwenye chupa ambayo liliishi humo miaka 1000 na zaidi.
Ukirejea kwenye vitabu vitakatifu hasa Quran utaona jinsi gani Shetani (Ibilisi) alivyokataa kumpa heshima yake baba yetu Adam (Rehma na Amani Ziwe juu yake) na ikawa sababu ya yeye kufukuzwa katika Rehma za Mungu naye akaapa kuwa atalipiza hilo na kitu cha kwanza alicho fanya ni kusababisha yeye baba yetu Adam na mkewe Hawa (Eve) wafukuzwe katika bustani ya Adeni (Peponi). Shetani akawa ni adui mkubwa na namba moja wa Binaadam na kila wakati akitafuta nafasi ya kumpoteza binaadam kutoka kwenye malengo ya kumbwa na kuletwa kwake duniani.
Malengo ya Kuumbwa binaadam ni ili amuabudu Mola wake bila kumshirikisha na yoyote wala chochote na malengo ya kuletwa kwake Duniani ni kuusimamisha Ufalme wa Mungu Mmoja hapa duniani baada ya waliotangulia, majini kushindwa. Lakini kwa muda wote Shetani amekuwa akitafuta nafasi ili kuyafanya malengo hayo yawe kinyume chake, kwamba Binaadam amuabudu Shetani na asimamishe ufalme wa Shetani duniani.
Hata hivyo pamoja na kwamba majini si viumbe wawezao kuonekana kwa jicho la kawaida la binaadam ingawa wao, majini wanatuona lakini bado majini hawana uwezo kumshinda Binaadam, hivyo hatakama shetani atataka kusimamisha ufalme wake kwa kupigana vita na binaadam, basi shetani hatoweza, atashindwa vibaya mno. Sasa afanye nini kumshinda adui yake mwenye nguvu kumshinda yeye, aliyesababisha yeye kufukuzwa mbinguni na kulaaniwa, aliyekuja kutawala dunia ambayo ndugu zake (mashetani wenzake) waliokuwa wanaitawala kabla?
Uwepo wa majini au mashetani, devils, unaonekana kwenye mchoro huu ambapo shetani anaonekana kwenye sikio la binadam akijaribu kuweka ushawishi wake kwenye mawazo ya mtu huyo.
Hata hivyo pamoja na kwamba majini si viumbe wawezao kuonekana kwa jicho la kawaida la binaadam ingawa wao, majini wanatuona lakini bado majini hawana uwezo kumshinda Binaadam, hivyo hatakama shetani atataka kusimamisha ufalme wake kwa kupigana vita na binaadam, basi shetani hatoweza, atashindwa vibaya mno. Sasa afanye nini kumshinda adui yake mwenye nguvu kumshinda yeye, aliyesababisha yeye kufukuzwa mbinguni na kulaaniwa, aliyekuja kutawala dunia ambayo ndugu zake (mashetani wenzake) waliokuwa wanaitawala kabla?
Mchoro huu umechorwa na watu ambao wanasadiki kumuona binadam akibadilisha maumbile kutoka kwenye umbo la binadam kwenda kwenye umbo la viumbe wanao onekana kwenye michoro hiyo. Hali hiyo imepewa jina la 'shape shifting'
Mtu kuwa na ugomvi na nafsi yake (self conflict) ni jambo la hatari zaidi kuliko mtu kuwa na ugomvi na mtu mwingine. Vita vya nchi ndani kwa ndani (civil war) vinaogopewa zaidi kuliko vita vya taifa moja kulivamia taifa jingine. Adui anaye toka ndani yako (nafsi yako) ni mbaya zaidi kuliko adui anaye toka nje. Watu wamejinyonga, wamekunywa sumu, Falme, nchi na dola kubwa duniani zimeporomoka sababu ya adui anaye tokea ndani yao.
Shetani anamtawala binaadam kupitia Binaadam. Reptilia wale wakaingiliana na Binaadam na kutengeneza kizazi kipya chenye mchanganyiko wa Mashetani, (Reptilia) na Binaadam, Katika mfululizo wa maelezo haya kizazi hicho nitakuwa nikikiita kizazi cha Nyoka, kokote nitakapo taja kizazi cha Nyoka basi nitakuwa namaanisha kizazi hichi kilichotokana na Reptilia ambao ni mashetani pamoja na binaadam kama ambavyo Yesu mwenyewe alivyo waita kwenye kitabu cha Mathayo.
Shetani anamtawala binaadam kupitia Binaadam. Reptilia wale wakaingiliana na Binaadam na kutengeneza kizazi kipya chenye mchanganyiko wa Mashetani, (Reptilia) na Binaadam, Katika mfululizo wa maelezo haya kizazi hicho nitakuwa nikikiita kizazi cha Nyoka, kokote nitakapo taja kizazi cha Nyoka basi nitakuwa namaanisha kizazi hichi kilichotokana na Reptilia ambao ni mashetani pamoja na binaadam kama ambavyo Yesu mwenyewe alivyo waita kwenye kitabu cha Mathayo.
“Enyi nyoka, wana wa Majoka...”
Kumekuwa na ngano nyingi kuhusiana na watu ambao wanayo damu maalum, ya kizazi maalum, ngano hizi zinanguvu sana magharibi mwa na dunia, na wakati mwingine hata mashariki yake. Watu hawa pia wanafahamika kama 'the shining Ones', inasemekana kuwa watu hawa wanayo damu mahususi ya wafalme, au damu ya waungu, damu ya Annunaki waliokuja kutoka sayari ya mbali. Watu hao ndiyo wenye haki ya kuitawala dunia kwa mujibu ya mafundisho yao kama tutakavyo ona huko mbele.
Kutokana na ushawishi waliokuwa nao wavamizi hao kwenye jamii waka waweka watoto wao hao ambao si binaadam bali ni majini katika nafasi za juu kiserikali na kiuchumi na kwa maelfu ya miaka kizazi hicho cha nyoka ndicho kimekuwa kikiitawala dunia.
Mchoro huu wa kale mno ukionesha michoro ya waungu kutoka sayari ya mbali, mtizame wa kwanza kushoto kichwani anayo miale, ambayo ni ishara ya nuru kali kutoka usoni pake kudhihirisha kuwa anayo damu tukufu. Ishara hiyo imendelea kutumika mpaka leo ikitumiwa kuwaonesha watakatifu mbalimbali duniani, akiwemo Yesu.
Kutokana na uchunguzi na sifa zilizotajwa za ‘wageni’ hawa reptilia zinafanana na zile za Mashetani. Mashetani wana sifa kubwa moja, kusema uwongo, daima ni waongo. Mathalani ukimfuata mganga wa kienyeji anayefuga majini kama hujamuambia shida yako basi huenda akakutajia yeye, na atakapo taja atakutajia kumi au zaidi na moja tu ndiyo inayoweza kuwa ya kwako na au hata asifanikiwe kutaja ile ya kwako.
Kwenye mapiramidi ya Mexico, anaonekana Reptilia kwenye umbo la binadam, mbele ya binadam, tizama kwenye kichwa cha mjusi huyo unaiyona nuru ya kichwani mwake inayo ashiria uwepo wa damu tukufu ya wafalme kwenye mwili wake? The shining Ones.
Habari yenyewe iko hivi, unapoaga kuwa unakwenda kwa mganga flani ambaye katika tiba zake anahusisha na mambo ya kishetani; huwa kwa kawaida angani panakuwepo na majini, endapo basi shetani flani akasikia shida unayo endea kwa mchawi yule basi humpa taarifa yule shetani anayefugwa na yule mchawi kwa hiyo unapofika pale basi tayari taarifa zimeshafika, ispokuwa yule shetani aliyepata taarifa mwanzo au yule aliyeletewa au wote wawili huongezea ya kwao kama kumi ya uwongo ndiyo sababu yule mchawi hatokuambia shida yako kwa usahihi sababu hafahamu na anategemea taarifa za uwongo toka kwa mashetani.
Mtaalam akiwa kazini. Chezea kazi wewee!!!
Maelfu ya miaka walipo wavamia wanaadam sehemu mbali mbali duniani na boti zao zieleazo angani kama nyungo mashetani hawakuacha tabia yao hii ya kusema uwongo, waka wadanganya binaadam kuwa wao ni waungu.
Mashetani hawana viwiliwili, ingawa wanaweza kuyaroga macho ya binaadam na kuonekana katika maumbile tofauti tofauti ya viumbe wengine kama walivyo zishukia jamii hizo na umbile la Reptilia na hata wanaweza kujivalisha katika mwili wa kiumbe kingine chochote kama tuonavyo na tusikiavyo mtu aliye pandisha shetani na kisha shetani huyo kuanza kuzungumza kwa kupitia kinywa cha mtu huyo. Hivyo ni moja ya tabia yao kujibadilisha maumbile kama walivyo fanya Mesepotamia. Katika maumbile yote basi hili la nyoka linapendeza kwao zaidi.
The devil incarnation.
Mashetani huwa yanaishi angani, kwenye mapango na mashimoni na hata watafiti walipojaribu kuchunguza ni wapi kabila hili la Reptilia wametokea hawakupata ila sehemu hizi tatu, mashimoni, mapangoni na kutoka angani. Rejea mafundisho ya mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alipowaambia wafuasi wake wafungieni ndani watoto wenu wakati wa magharibi (wakati jua linazama) maana ndiyo wakati mashetani wanatoka katika mashimo yao.
Shape shifting
Sifa nyingine ya mashetani hupenda kusafiri usiku wakiwa katika chombo chenye umbo la duara kama kisosi ama ungo ingawa kinaweza kuwa katika umbo jingine lolote na wakiwa na kijinga cha moto mkononi mwao kama ilivyoelezewa kwa ‘Reptilia wale wakati wanawasili nchi za Sumeria, Egypt na Mesopotamia na sehemu nyingine duniani, waliitwa ni waungu waliokuja na ndege zing’aazo, ikiwa na maana ndege ziwakazo. Rejea Safari ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alipokuwa anakwenda Miiraji walikutana na Shetani aliyekuwa anasafiri angani na mkononi ameshika kijinga cha moto.....
Sasa utajua ni kwa nini Babilon, Mesopotami, Egypt, Sumeri na kwengineko ulimwenguni ambako ‘wageni’ hawa walifika kuna athari kubwa ya elimu kuhusu Uchawi, Elimu ya Nyota, Elimu ya Maumbo, Elimu ya Mahesabu, Jua, Mfumo wa Sayari, majina ya Sayari mbalimbali, rangi zake, ukubwa wake na nafasi yake kutoka kwenye Jua na kutoka kwenye Sayari nyingine, Utajua ni kwa nini Ustaarabu wao ulikuwa ni wahali ya juu ukilinganisha na jamii zingine, majengo yao ya ajabu kupita kiasi, umelitizama Piramidi kubwa la gaza wewe? Tafuta vidio yake utizame utajua ni kwanini waliweza kujenga kitu kama kile.
Ni nani mjenzi wa Pyiramidi hizi, lini zilijengwa na kwasababu gani? Punde nitaivunja vunja msingi wa historia ya dunia hii ambao umejengwa kwako wakati ukiwa kwenye 'Indoctrination Camp' (shule/chuo), endelea kufuatilia posti hizi.
Kitabu kikongwe zaidi cha kimila na kidini cha watu wanao jiita ni ‘wayahudi’, au ‘kizazi teule’ Talmudi, au Talmudi ya Wababilon hapa ndipo ilipokuwa chimbuko lake, kitabu hicho kimebeba lile lengo kuu la Shetani la kumpoteza Binaadam. Yaani Binaadam amuabudu Shetani na asimamishe utawala wa shetani Duniani. Yale yote yaliyo ruhusiwa katika vitabu vitakatifu yamekatazwa na kuzuiwa vikali katika kitabu hicho na yale yote yaliyo katazwa katika vitabu vitakatifu yameamrishwa na kutiliwa nguvu yafanywe katika kitabu hichi.
almudi inayo hazina kubwa ua uchawi na ushirikina.
Yaliyo andikwa katika kitabu hichi ndiyo yanayofundishwa na kufanyika kwenye dini ya Mashetani. Moja ya kurasa zake imeandikwa; Asiye kuwa myahudi hapaswi kukisoma na akikamatwa sheria yake ni auwawe, na myahudi atakaye kamatwa anamfundisha asiye kuwa myahudi wote lazima wauwawe. Kitabu kingine kitumiwacho na watu hao kama kitabu kitakatifu chenye maudhui sawa na yale ya Talmudi lakini kikiwa zaidi na elimu kubwa ya uchawi ni Kabbala, na vitabu vyote viwili vimebeba ile nadharia ya kuichukua dunia yote iwe ni ya kizazi fulani na wengine wote wawe watumwa, na kizazi kinachoandaliwa kuichukua dunia kinakwenda kwa jina la kizazi teule.
Kwa maelfu ya miaka umbile la Reptilia, yaani Mjusi na Nyoka limekuwa ndilo umbile litumiwalo na Shetani zaidi katika huu ushirika wake na Binaadam na pia katika kumpotosha Binaadam katika malengo yake. Kama utaikumbuka hadithi ya nabii Musa kama ilivyoelezwa katika vitabu vitakatifu alipokwenda kukutana na wale wachawi wa Firaun, wachawi wale walitupa fimbo zao chini na kisha zikageuka nyoka wanaokimbia Musa naye akatupa fimbo yake ikawa ni Nyoka ikawameza nyoka wa wale wachawi.
Kwenye biblia kuna hadithi ya binaadam wa kwanza na mke wake ambao walikuwa kwenye bustani ya Adeni, halafu Shetani akajibadilisha umbile lake na kuwa Nyoka na kisha akawadanganya.
Kwenye biblia kuna hadithi ya binaadam wa kwanza na mke wake ambao walikuwa kwenye bustani ya Adeni, halafu Shetani akajibadilisha umbile lake na kuwa Nyoka na kisha akawadanganya.
Sanamu la kale la mungu icer alipokuwa anabudiwa Babyloni.
Kihistoria katika mji wa Iraq kulikuwa na Utamaduni wa Waubaid kwenye mji wa Babiloni, mji wa mababu wa wafuasi wa dini ya mashetani ambao sasa mbali na majina mengi pia wanajiita Illuminanti kama tutakavyoona, walikuwa wanamuabudu mungu ambaye umbile lake ni kama la reptilia, mjusi. Jina lake ni Icer.
Utamaduni wa wamarekani walioishi Mexico maelfu ya miaka nyuma walimuabudu mungu mwenye umbile la Nyoka, nyoka mwenye mabawa aliyeitwa Aztec au Toltec. Wahindi walikuwa na waungu wengi lakini mmoja wao alikuwa ni Nyoka aliitwa Buholnkiya.
Waigypt nao walikuwa na mungu wao ambaye ni Nyoka aliitwa Kneph na mafirauni wa Misri walikuwa wakichorwa na bado wanaendelea kuchorwa pamoja na Nyoka.
Mungu wa British ya zama za kale alitwa Dragon mungu wa dunia naye alikuwa kama mjusi. Waungu wa namna hii wako wengi duniani na jamii nyingi zinamuabudu Shetani, Lucifer katika umbo la Reptilia.
mungu Aztec wa Marekani ya kusini akila kafara yake.
Utamaduni wa wamarekani walioishi Mexico maelfu ya miaka nyuma walimuabudu mungu mwenye umbile la Nyoka, nyoka mwenye mabawa aliyeitwa Aztec au Toltec. Wahindi walikuwa na waungu wengi lakini mmoja wao alikuwa ni Nyoka aliitwa Buholnkiya.
Waigypt nao walikuwa na mungu wao ambaye ni Nyoka aliitwa Kneph na mafirauni wa Misri walikuwa wakichorwa na bado wanaendelea kuchorwa pamoja na Nyoka.
Farao wa misri, umeona alama ya nyoka?
Mungu wa British ya zama za kale alitwa Dragon mungu wa dunia naye alikuwa kama mjusi. Waungu wa namna hii wako wengi duniani na jamii nyingi zinamuabudu Shetani, Lucifer katika umbo la Reptilia.
ShNyoka aliyejizungusha kwenye yai, ilikuwa ni alama yenye kufahamika kwa wahindu, waegypty, na wa druidisi. Alama hiyo inawakilisha tendo la uumbaji wa ulimwengu. Haya ni mafunzo kwa mwanamasonia wa darja la 25.
Katika nchi ya Tanzania sehemu mbalimbali kumekuwa na habari juu ya nyoka wa ajabu na nyoka wanao abudiwa na watu.
Tumesikia visa kuhusu wahubiri wakubwa mikoani kwetu kwamba wameweza kuponesha watu, kuwapa watu utajiri, kuwaondolea matatizo yao na kadha wa kadha lakini baadae miongoni mwao wakawaweka waumini wao kwenye utata sababu wamekamatwa wakitumia nguvu za kiza na moja wapo ni Nyoka kutoka katika vinywa vyao wakati wamewaambia waumini wao wafunge macho, na mara nyingi imetokea ni kwa wale waumini wenye uwezo kama wao na waumini wa kawaida hawaoni chochote, Nyoka, Nyoka kila mahala, Shetani Shetani kila mahala.
Kama tulivyoona kuwa kizazi kile hakikuwa kingine ila Majini walioamua kuchukua umbo la Nyoka (Reptilia) na kuwarubuni binaadam, wakajiita waungu, na wakazaa na binti wa binaadam na watoto wale wakaitwa wana wa waungu na hatimaye mashetani hayo yakaanza kuabudiwa kama Mungu kwa kupitia alama na maumbo mbalimbali ambayo yote yalikuwa na maudhui ya Nyoka na Mijusi (Reptilia) na kama tulivyoona utafiti mbali mbali umeelezea kuwa kizazi hicho kilitokea mapangoni, Mashimoni, na kwenye Nyota ya Dracu makazi ambayo ndiyo hasa mazingira wanayoishi majini.
Kizazi hicho kikapewa nguvu na utukufu na kutawalishwa nchi, chini ya familia kumi na mbili, ingawa wachunguzi wengine wanadi ziko kumi na tatu na hata kumi na tano, kizazi hicho kikatapakaa duniani kote, Kutoka Mesopotamia, Egypt mpaka India, Afrika ya Kaskazini na Kusini, Amerika zote mbili na hata Ulaya, na hata sasa wameishikilia dunia, na kama mto uendao chini ya aridhi taratibu kuelekea baharini ndivyo kinavyokwenda kizazi hiki kukifikia kile wanachokiita KUITAWALA DUNIA (Total Global Domination).
ShIndustry ya filamu inatuambia nini kuhusiana na kazi zake za namna hii?
Kwa hiyo majini ndiyo viumbe pekee vyenye uwezo sawa na binaadam kwa maana ya UHURU, ndiyo viumbe walipewa kazi kama tuliyonayo binaadam, kazi ya Kusimamia Amri za Muumba wetu, ila waliposhindwa ndipo binaadam alipo letwa, Hayawani wengine wasingeweza kufanya kazi hii sababu hawako Huru, ni Binaadam na Majini tu ndiyo walio Huru, ikiwa basi kuna chochote kitakachotokea kuhusiana na utawala wa hapa Duniani, viumbe hawa wawili ndiyo wakuangaliwa, ndiyo maana mtu akifanya maovu utawasikia watu wakisema “Huyu kapotezwa na Shetani” Huwezi kusikia kuwa kapotezwa na Simba, au Kuku, au Mjusi hapana hawa hawako huru ni Shetani mpinzani wake ndiye aliye huru ndiye mwenye uwezo wa kumpoteza.
Mjusi wala Nyoka hawezi kuzaa na binaadam sababu wana mifumo tofauti ya uzazi, sasa iweje kuwepo na kizazi cha Nyoka? Hapana, Nyoka ni umbo walilolichagua majini kulivaa, kama tujuavyo hawana kiwili wili ila wana uwezo wa kujivika umbo la kiumbe chochote na wao kwa ajili ya kumpotosha na hatimaye kumtawala binaadam wamechagua umbile la Nyoka!
Mashetani hao waliojiita waungu na kumfundisha binaadam taaluama mbali mbali ikiwemo ile ya elimu ya nyota, mahesabu, matibabu, na sayansi ya ujenzi, sayansi ya uchawi na mengine mengi.
Mwana masonia wa daraja la 33 aliyekuwa na cheo kikubwa ndani ya Masonic Scottish Rite, Jim Shaw kwenye kitabu chake alichokiita The Deadly Deception ameelezea wazi jinsi Fremasonry wanavyoabudu Shetani kwenye umbile la Nyoka ndani ya hekalu lao lililopo ndani ya Washington D.C.
Strike the deal with the devil
Jamii za kileo zimekuwa zikiathiriwa, kurubuniwa na kuharibiwa na hili kabila la Reptilia ambalo lilikuwepo kwa kipindi kirefu hata kabla ya kuja binaadam na kumrubini binaadam maelfu ya mika nyuma hata kabla ya kuja Kristo, Jamii nyingi za kale zinaamini kuwepo kwa kabila hili lililoingiliana na kushirikiana na binaadam katika nyanja mbalimbali.
Wanaamini kuwa jamii hiyo iliishi chini ya aridhi, na walikuwa na maumbile ya Nyoka na walikuwa na nguvu za ajabu za kiasili. Na pia zinadai kuwa wengi waliopotea waliwaabudu hao viumbe wa chini ya aridhi kwa heshima kuu, utiifu na hofu. Kafara ya binaadam ilitolewa ilkuwaomba waungu Nyoka (Mashetani) wasimletee binaadam madhara, mahekalu na minara ilijengwa mahala ambapo iliaminika ndiko kwenye mlango wa kuelekea chini ya aridhi wanapoishi waungu nyoka.
Mapango na mashimo chini ya aridhi ni moja ya makazi yao makubwa.
Wanaamini kuwa jamii hiyo iliishi chini ya aridhi, na walikuwa na maumbile ya Nyoka na walikuwa na nguvu za ajabu za kiasili. Na pia zinadai kuwa wengi waliopotea waliwaabudu hao viumbe wa chini ya aridhi kwa heshima kuu, utiifu na hofu. Kafara ya binaadam ilitolewa ilkuwaomba waungu Nyoka (Mashetani) wasimletee binaadam madhara, mahekalu na minara ilijengwa mahala ambapo iliaminika ndiko kwenye mlango wa kuelekea chini ya aridhi wanapoishi waungu nyoka.
Mojawapo ya sehemu hizo tukufu kwa waungu hao ni ile iliyopo kusini mashariki mwa Oaxaco, Mexico ambapo kuna masalio ya kale sana, moja wapo ya masalio hayo ni Hekalu la “Milta”. Ushahidi mbali mbali unaonesha kuwa katika zama hizo za kale hekalu hilo lilikuwa lina sehemu ya kuelekea chini ya aridhi, ambako kuna uwanda mpana na kisha linateremka chini zaidi na kukuta uwanda mwingine na kisha unashuka chini zaidi na kukutana na uwanda wa tatu kwenye eneo hilo la tatu kuna jiwe kubwa mno ambalo linafunika ulimwengu wa jamii hiyo (majini). Kutokana na maelezo ya mtafiti Charles A. Marcoux na wachunguzi wengine na wakazi wa asili wa eneo hilo ambao ni wahindi kuwa karne kadhaa zilizopita wakazi wa hapo walikuwa wanatoa kafara ya binaadam kwa waungu wanaoishi chini ya aridhi. Wahanga hao walikuwa wakitupwa katika mashimo hayo yenye kiza wakiwa hai na baada ya hapo hawakuonekana tena.
Lango la kuingia kwenye hekalu la Malta, tizama ukuta huo ulivyo jengwa kwa mawe makubwa, uzito wa mawe hayo limoja tu linakaribia tani 70! Walitumia zana gani kunyanyua na kuyapanga hapo?
Wachungaji kadhaa walifika katika maeneo hayo karne kadhaa nyuma na wakaenda chini ya aridhi katika mashimo hayo mpaka walipofika katika uwanda wa tatu na kuweza kufungua mlango huo na kuteremka chini wakiwa na tochi mikononi wakazidi kuteremka katika kile kinacho onekana ni njia ndefu zisizo na mwisho chini ya aridhi zinazoelekea kwenye milima isiyofahamika, dunia nyingine kabisa.
Baada ya kwenda umbali mkubwa wakaanza kupatwa na hofu baada ya kuanza kuona nyoka wakitokeza kwenye miamba yenye kiza, maumbo ya jabu na vivuli katika minara ya kale iliyochongwa kwenye miamba hiyo, sauti za ajabu na upepo ukaanza kuvuma kupitia kwenye njia hizo na hofu ikawazidi na kuhisi hawako katika dunia na kuanza safari ya kuyakimbia makazi hayo.
Moja ya mchoro ukionesha moja ya mahekalu yanayo patikana Malta, uzio wake ni mawe makubwa yaliyo pangwa vizuri kabisa.
Baada ya kwenda umbali mkubwa wakaanza kupatwa na hofu baada ya kuanza kuona nyoka wakitokeza kwenye miamba yenye kiza, maumbo ya jabu na vivuli katika minara ya kale iliyochongwa kwenye miamba hiyo, sauti za ajabu na upepo ukaanza kuvuma kupitia kwenye njia hizo na hofu ikawazidi na kuhisi hawako katika dunia na kuanza safari ya kuyakimbia makazi hayo.
The road to unknown, underworld.
Habari nyingine kama hiyo ni ile inayo husu hekalu la Wagiriki linaloitwa “Temple of Apollo” lililoko Uturiki. Eneo mwanzo lilikuwa likimilikuwa na Dola ya Wagiriki ambayo ilitawala eneo kubwa kuzunguka bahari ya Mediterranea. Katika hekalu hilo kuna pango ambalo wanyama na watu waliokuwa wakiingia humo hawakuweza kurudi tena. Miaka ya 1980 wanafunzi kadhaa wa Kiaustralia waliongia katika pango hilo nao pia hawakuweza kuonekana tena. Serikali ya Uturiki ikaweka nondo kuzuia watu wengine wasipotee kwa kuingia humo lakini kama ilivyofahamika wanafunzi wa Kiaustralia hawakuonekana tena.
Moja ya kazi za Hollwood zinazo lenga kuwahimiza watoto wetu kujenga mahusiano na mashetani na hata kuwategemea kwenye mambo mbalimbali.
Kutoka na maandishi ya kale ya Mwanafalsafa wa kigiri aliyeishi kati ya mwaka 63 BC na 24 AD yanasema kuwa pango hilo ni mlango wa kuelekea kwenye aridhi ya wafu inayomilikuwa na waungu wa chini ya aridhi.
Ushahidi mbalimbali unaonesha kuwepo kwa jamii nyingine inayoishi pamoja nasi, jamii hii ipo chini ya aridhi, mashimoni na mapangoni ingawa ni vigumu kuelezea kuwepo kwa viumbe hao kwenye sayansi ya Bailojia, lakini kwenye sayansi ya Jiografia na Miamba pamoja na ile Sayansi ya Nyota kuwepo kwa athari ya jamii hiyo kuna onekana wazi, kwenye mila tamaduni na dini mbalimbali jamii hii imeelezewa waziwazi kuwepo kwake na athari yake kwenye maisha yetu.
Hadithi maarufu sana Uingereza hii, hadithi kuhusu watoto wawili waliokuwa wanaishi chini ya aridhi kwa miaka ya kutosha.
Katika gazeti la Amazing Stories Science Fact Magazine la Dec 1946 Ukurasa wa 162 kuna barua iliyoandikwa na George A. Lehew, ameelezea hadithi inayofanana na ile ya ya kwenye hekalu la “Milta”. Miaka kadhaa nyuma mtu aliyejulikana kwa jina la Steve Brodie anasema alipotelea chini ya aridhi maeneo ya Arizona na baadae akakutwa anatembea kwenye maeneo ya New York akiwa hana kumbu kumbu ya wapi alikuwa, Brodie ameielezea taarifa hii kwa mtafiti John Robinson ambaye akielezea kwenye kipindi cha redio New York hata hivyo Brode alipotea tena kimiujiza ujiza.
Kipindi flani katika karne ya 12, mwandishi aliyekuwa anaitwa Gervase ameandika habari ya ajabu kuhusu, watoto wawili ambao ghafla walitokea katika katika mji mdogo wa Bury St. Edmund, England. Habari hiyo pia imeripotiwa na waandishi kadhaa katika kipindi hicho na baadae ambao ni pamoja na William wa Newbury kwenye kitabu cha HISTORIA RERUM ANGLICARUM, kilichoandikwa Yorkshire, England (1136-1198); Abbot Ralph wa Coggeshall kwenye kitabu cha CHRONICON ANGLICARUM; wengine waliyoandika habari hiyo ni Giraldus Cambrensis na Walsingham. Habari hiyo akaja kuandikwa tena kwenye jarida la FLYING SAUCERS UNCENSORED, na Harold T. Wilkins (Citadel Press., New York, N.Y. 1955., uk.97-98) na wote wanakubali kuwa habari hiyo ni ya kweli.
alipotokeza juu ya aridhi walijikuta wapo sehemu ya ajabu sana na mazingira waliyo kuwa wanaishi kabla.
Habari hiyo inaelezea kuwa wakazi pamoja na wakulima wa eneo hilo waliwaona watoto wawili wakishanga shangaa maeneo hayo wanao onekana kama waliotolewa kwenye mapango na mashimo ya kale yaliyokuwa yakijulikana kwa wakazi hao kama “Wolf-Pitts”, mashimo hayo ni ya kale mno lakini hayajulikani ni lini na ni nani aliyachimba mashimo hayo lakini ni ya kale mno. Kilicho cha ajabu na cha kutisha kwa watoto hao ni kuwa walikuwa na ngozi yenye rangi ya kijani kibichi lakini maumbile yao yalikuwa ni ya binaadam wa kawaida. Wakazi hao walijaribu kuzungumza na watoto hao lakini ilikuwa ni vigumu kwa sababu watoto hao walikuwa wakizungumza lugha ambayo ni tofauti na ya wakazi hao.
Watoto hao ni misichana na mvulana, wanakijiji wakamua kuwachukua na kujaribu kuwapatia kila aina ya chakula walichokuwa nacho lakini vyote vilonekana ni vigeni kwa wao hivyo hawakuvichukua na hata baada ya muda mrefu wa kujaribu kujihifadhi katika mazingira mapya mvulana alikufa na alibaki msichana ambaye baada ya kufahamu lugha ya wakazi wa pale akawaelezea hadithi yake ya wapi walipotokea na kaka yake, alielezea kuwa katika dunia aliyotoka watu wake wana ngozi kama yake au kama iliyokuwa yake kwani kadiri muda ulivyopita ngozi ya kijani ilikuwa ikipotea,
Anasema kuwa nchi yao iko chini ya aridhi ni kubwa mno na kuna mto wa chini ya aridhi ambao nao pia ni mkubwa na unapakana na nchi nyingine inayong’ara, anakumbuka siku moja yeye na kaka yake walipokuwa wanachunga wanyama wa chini ya aridhi na wakashika njia moja katika safari yao ndefu ambayo ni kama ya masiku kadhaa ingawa katika dunia yao hakuna kitu kinachoitwa mchana wala usiku njia iliwafikisha kwenye mfereji mrefu unao panda juu ambao hatimae uliwafikisha katika ulimwengu wetu ambao kilikuwa ni kitu cha kushangaza mno na baada ya kuzunguka kwa muda na kuanza kutafuta shimo walilitokea lakini hawakuweza kuliona kutokana na mwanga mkali wa jua ambao haupatikani katika ulimwengu wao ndipo walipoonwa na wanakijiji.
Ikiwa habari hii ni kweli kama walivyosema waandishi wa habari yenyewe basi watoto hao ni zao la Mashetani na Binaadam ambao wanakamatwa kwa ajili ya kutolewa kafara na kufanyishwa kazi chini ya aridhi. Kila mwaka nchini Uingereza kunaripotiwa kesi za watoto waliopotea zaidi ya 400,000, Marekani nako kesi hizo zinafikia 98,000 kila mwaka; watoto hawa wanakwenda wapi?
Uwezekano kwamba jamii ya kale ya kabila la mashetani linaloishi chini ya aridhi si jambo geni wala jipya. Kabila hili lililojitikeza katika umbile la Nyoka na Mijusi tangu awali linauthibitisho kwenye mafundisho ya kiroho na kihistoria ya tangu enzi na enzi. Na kwamba kabila hilo ni huru kama ambavyo tulivyo sisi binaadam na linaishi chini kabisa ya aridhi baada ya Mantel ( huu ni ukanda unaotenganisha tabaka la juu la aridhi na tabaka la chini ambalo lina joto mno) Joto hilo halimuwezeshi kiumbe yoyote mwenye maumbilie kuweza kuishi eneo hilo, na hivyo mijusi hao kama kweli ni mijusi na nyoka tunao wafahamu wasingeweza kuishi eneo hilo, lakini kwa sababu majini hawana maumbile na wameumbwa na moto kwa wao hayo ni makazi yao ya kudumu.
Neno Serpent ambalo kiswahili linamaana ya Nyoka au ina ya Reptilia, neno hilo linatokana na neno “Nachash” ambalo kutokana na wafasiri wa lugha hasa ya kiyahudi ambapo asili ya neno hilo linamaana ya reptilia, nguvu za giza, maarifa, kurusha uchawi, nyoka, n.k . Yote haya yanaelezea tabia ya kabila hili la chini ya aridhi. Maana ya asili ya “Nachash” ambalo India pia walilitumia lakini haikuwa haswa ikimaanisha Nyoka ila bali ikimaanisha kiumbe chenye akili na maarifa ya hali ya juu, mwenye uwezo wa kufikiri na kuzungumza.
Mungu wa wagiriki akiwa na nyoka.
Kutoka na maelezo yanayopatika kwenye vitabu vya kale vya Kiyahudi vinaelezea kuwa kabla dunia haijaharibika kwa maovu jamii hiyo inayoishi chini ya aridhi ilijitokeza juu na kuanza kushirikiana na wachawi kwa lengo la kuwapatia wachawi hao ujuzi na maarifa mbalimbali na wao wachawi wawaisaidie wakazi hao wa chini ya airdhi uwezo na nguvu za kumtawala binaadam, kama wanavyo fanya freemasonry sasa.
Credits...SalimMsangiBlog
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena