Yanga imeendelea kuipa presha na kuipumulia Simba inayoongoza ligi kuu Tanzania bara kwa pointi 41 baada ya kuifumua Ndanda kwa bao 4-0 katika mchezo mkali liofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam
Mlinzi wa Yanga Vicent Bossou alihitimisha kalamu ya ushindi kwa kufunga bao la nne katika dakika ya 89 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na mlinzi mwenzake, Juma Abdul.
Amis Tambwe alipachika bao la tatu dakika ya 26 huku Donald Ngoma akifunga mabao mawili katika dakika ya 21 na dakika ya tatu kwenye mchezo huo akiwa na magoli 37 katika klabu msimu huu kutokana na ushindi huo Yanga imefikisha pointi 40 dhidi ya Simba yenye pointi 41.
Kikosi cha Yanga dhidi ya Ndanda ni:- 1.Deogratius Munishi 2.Juma Abdul 3.Mwinyi Haji 4.Vicent Bossou 5.Kelvin Yondani 6.Saidi Juma 7.Saimoni Msuva 8.Haruna Niyonzima 9. Donald Ngoma 10. Amisi Tambwe 11.Emanuel Martin
Akiba Ali Mustafa Andrew Vicent Justin Zullu Thabani Kamusoko Obrey Chirwa Geofrey Mwashuiya Deusi Kaseke.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena