Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Simba ulimi nje kwa Azam

Wafalme wa pori Simba Sports Club hapo jana walichapwa bao 1-0 na klabu ya Azam katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi. Azam iliilambisha Simba ice cream dakika ya 29 ya mchezo kwa goli lililofungwa na Himid Mao na kupelekea shangwe na nderemo kwa mashabiki wa Azam ambao walipata sapoti kubwa sana ya mashabiki wa Yanga.

Simba ambayo ilifikia hatua ya fainali baada ya kuwaondoa mashindanoni mahasimu wao wa jadi; Yanga walishindwa kutamba mbele ya Azam ambao waliandika rekodi ya kutoruhusu hata bao moja kwenye mashindano hayo mwaka huu.

 Kwa upande mwingine, Smon Msuva wa klabu ya Yanga alitangazwa mfungaji bora wa kombe la mapinduzi, Aishi Manula wa Azam akaibuka golikipa bora wa mashindano, Said Mohamed wa timu ya Taifa Jang'ombe alitangazwa mchezaji bora chipukuzi huku Method Mwanjale wa klabu ya Simba akitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Mapinduzi.

Post a Comment

0 Comments