Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA MARA: INASIKITISHA | VIJANA WAWILI WAJITOKEZA KUOA MAITI ILI KUONDOA MKOSI KATIKA FAMILIA.

Image may contain: 1 person, standing
Akitoa misa ya kumwombea binti aliye fariki dunia akiwa anajifungua katika hospitali ya kowak, PADRI Valens amekemea Tabia iliyo zoeleka katika makabila ya RORYA na mkoa wa Mara ya kudhani binti ambae hajaolewa kwamba ni mkosi anapo fariki .hali hiyo ilijitokeza alipo fariki binti ROSWITA MICHAEL KAMBONA wa kijiji cha majengo kata ya koryo wilayani rorya alipo fariki akijifungua. 
Image may contain: 1 person, standing and outdoor
vijana wawili kujitokeza wakitaka kila mmoja abebe msiba huo akazike na baadae kujakulipwa binti mwingine kwa maana ya kuondolea familia ile mkosi .jambo hill lilimlazimu
PADRI Valens kuamua kuingilia swala hili na kukemea na kuwataka wazazi wa marehemu kupuuza ndugu na jamaa ambao baada ya marehemu kufariki walianza mchakato wa kutafuta ni wapiti atazikwa binti Roswita ambae alifariki na kichanga chake akijifungua .
PADRI VALENS amewataka wana rorya hasa wajaluo kuachana na mila hizi ambazo zinalitia aibu Makanisa ,jamii na wanaharakati wanaojitahidi kuelimisha jamii kuachana na mila kandamizi zinazo kandamiza watoto wa kike ikiwemo na ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Image may contain: one or more people, people standing and indoor
Baba wa marehemu Michael Kambona na mama wa marehemu walikiri kupambana na wanandugu na ukoo kuhusu swala la wapi atazikwa binti yao Roswita .wao kwa pamoja walisema wakati wa kuendekeza mila na desturi ya kutokumthamini binti yao akiwa amefariki umepitwa na wakati .nakusema walijitokeza vijana wawili mmoja alitokea sehemu ya kamoti kata ya nyaburongo na mwingine alitokea kamageta tarafa ya girango wilayani rorya wote wakiwa tayari kila mmoja kutaka akamzike Binti yetu Roswita ambae ni marehemu na kichanga chake .tulikataa na kusema binti yetu atazikwa kanisani ,na alipotolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hosp ya tarime aliffikiswa nyumbani na baadae kupelekwa kanisani ambako Leo tumemzika kwa amani na hesima zote.
Image may contain: 2 people, people sitting, people standing and indoor
akitoa ushuhuda wake mama wa marehemu amewataka watu wote walio kuja kmsaidia kumsindikiza kipenzi chake mwanae marehemu Roswita kuondokana na milapotofu .akasema mtoto wako umemzaa ukamlea umekuwa ukimtuma, mkila pamoja,mkifurahi akiwa mzima, lakini anapofariki anakuwa ni mkosi unamtelekeza unamwogopa hata huwezi kuigusa hata maiti yake eti sasa amekuwa shetani .akawataka wabadilike mtoto wa kike nisawa na mtoto wa kiume wore wana haki sawa.tuwajali tuwapende na tuwape haki sawa wanapotangulia mbele ya haki kama sasa binti yangu Roswita alivyo tagulia na kichanga chake mbele ya haki amina alimaliza mama wa marehemu.
Image may contain: one or more people and people standing
Baada ya mazishi hayo PADRI aliwaambia waombolezaji kwamba amebeba lawama zote kama yupo wakulaumiwa alaumiwe yeye wasilaumiwe wazazi wa Roswita alaumiwe yeye na yuko tayari kufa kwa kutetea na kukomesha mila POTOFU ya kunyanyasa watoto wa kike na wanawake wilayani Rorya .
Image may contain: 1 person, standing, wedding, crowd and outdoor
Namwisho PADRI Valens amesema ataandika kitabu juu ya unyanyasaji wa mtoto wa kike na wanawake wilayani rorya.

Habari na kituo cha habari na mawasiliano Rorya

Post a Comment

0 Comments