Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 10 kwa wenyeviti wa mtaa mkoani kwake kuwataja watu wanaowahisi wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Wito huo pia ni kwa watu wote wanaohusika kwenye biashara hiyo haramu pamoja na wazazi kuwasalimisha watoto wao.
Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo Jumatatu hii katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam akiongea na waandishi wa habari.
“Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya. Natoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi naye, njoo utoe taarifa tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikuwa sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.”
Ameongeza, “Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekuwa ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa.”
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena