Header Ads Widget

Responsive Advertisement

HABARI PICHA | Mahafali ya Kidato cha Sita Girango High School yafana....

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye akitukunuku vyeti wanafunzi wa kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Girango iliyopo Wilani Rorya Mkoani Mara.

Wahitimu wakitumbuiza uwanjani


Mwalimu Mkuu shule ya Sekondari Girango iliyopo Wilayani Rorya  Mkoani Mara Mwl Joseph Nguru akitaja changamoto zinazokumba shule hiyo likiwemo suala la maji pamoja na miundombinu ya Barabara kwani mvua zikinyesha mto hujaa maji nakushindwa kupita.

Mgeni rasmi kushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye akiteta jambo na Katibu Tawala Wilaya ya Rorya Murumbe James Daudi katika Mahafali ya kidato cha Sita Girango High School


Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Sita Girango High school


Tunaondoka Sasa


          

Meneja wa shule Gerald Orembe akitoa Neno kwa Wanafunzi

                       

Katibu Tawala Wilayani Rorya Mkoani Mara Murumbe Daudi akitoa Neno katika Mahafali hayo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Rorya Simon Chacha amehaidi kufikisha changamoto ya Miundombinu ya Barabara katika Ngazi huska ili kutatua changamoto hiyo kwani miundombinu ya Barabra kuelekea shuleni hapo ni changamoto kubwa.

               

       

Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye akisisitiza jambo






Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye No3 amekemea matumizi ya Mitandao ya kijamii kwa wanafunzi katika shule za sekondari bali wajikite katika masomo ili kufaulu vyema
Hata hivyo mwenyekiti huyo amezidi kulaani Vikali matumizi ya Madawa ya kulevya kwa wanafunzi hivyo amewataka wanafunzi hao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya mashuleni ikiwemo Bangi pamoja na Viroba.

“Rais Wetu anapiga vita matumizi ya madawa ya kulevya hivyo tuungane kwa pamoja kwa lengo la kutokomeza suala hili mshike mwenyezi Mungu katika maisha yenu ili kufanikiwa” alisema Kiboye.

Hayo ameyabainisha hii leo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita Girango High school iliyopo Wilayani Rorya Mkoani Mara.


Mgeni Rasmi akikabidhi Vyeti.

Mmiliki wa shule hiyo

Ad

Picha ya pamoja


(c) Cleo24News

Post a Comment

0 Comments