Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA-MARA:: MKUU WA WILAYA YA RORYA SAIMON KIMORI CHACHA AHIMIZA KILIMO CHA MAZAO YA MUDA MFUPI.

Related image
Akihutubia Baraza la madiwani Rorya Mkuu wa wilaya Mhe. Kimori amewataka madiwani kuhakikisha wanawashauri wananchi kutumia mvua za masika zinazoendelea kunyesha kulima mazao ya muda mfupi. Amesisitizia madiwani kutokuonea aibu swala la kuhamasisha wananchi kulima mihogo,viazi na mtama kwani hali ya chakula siyo nzuri, Pia amesema tarafa ya girango inapata mvua za ukanda wa juu kidogo hali ya girango siyo kama tarafa za Suba, Luo imbo na Nyancha ambazo hali ya mvua siyo ya kuridhisha.
Akizungumzia hali ya mapato ya Halimashauri, mkuu wa wilaya amesema ofisi ya mkurugenzi ijipange vizuri kwa kushirikiana na wataalam wake kubuni njia mbadala ya ukusanyaji mapato.kwani kunavyanzo vya mapato lakini uaminifu kwa watendaji umekuwa mdogo.
Akizungumzia swala la mapato, Diwani wa Nyamagaro Mhe. Masana amesema anasikitishwa na taarifa zinazo tolewa na wataalamu kwani siyo sahihi, akatolea mfano wa mwalo wa nyang'ombe alisema taarifa inaonyesha ng'ombe wanao chinjwa ni 90 kwa mialo mitatu.wakati ng'ombe 3 zinachinjwa kila mwalo kwa siku kwa mwezi ni ng'ombe 270 kwa mialo yote mitatu 3.lakini taarifa inayo pelekwa ni ng'ombe 90 kwa mwezi na ng'ombe 180 taarifa zake kuishia mifukoni kwa wakusanya mapato.
Akijibu hoja mbali mbali za madiwani mkurugenzi wa halimashauri ya Rorya Ndugu Charles Chacha alisema kwa sasa halimashauri ina subiri kibali ili iweze kuajiri watendaji wa vijiji na kata kwani halimashauri ya Rorya inamapungufu makubwa ya watendaji wa vijiji na kata .
Mwenyekiti wa halimashauri Mh Albati Machiwa akimkaribisha mkuu wa wilaya kuhutubia baraza aliwataka watumishi walio hamishiwa rorya Injinia wa maji na mwanasheria kuisaidia rorya kupunguza kero zilizopo .akizungumzia mwana sheria mwenyekiti alimwambia asaidie halmashauri katika vyesi vinavyo funguliwa kwani kumekuwa na mazoea ya kila kesi inayo funguliwa halimashauri hushindwa hata kama ni kesi ya kushinda.
Pia mhandisi wa maji ametakiwa kusaidia kumaliza kero za miradi ya maji katika maeneo mbali mbali ya Rorya kama vile Shirati, Randa, Utegi, Nyamaguku na Kinesi. na maeneo yote yaliyo na miradi ya maji.
Picha na kituo cha habari na mawadiliano rorya.

Post a Comment

0 Comments