Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TOTTENHAM KUHAMIA WEMBLEY

Tottenham Hotspurs watacheza mechi za nyumbani kwenye uwanja wa Wembley na sio White Hart Lane kama ilivyozoeleka. Klabu hiyo ye Magharibi mwa London inapisha ujenzi wa uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 61,000.

Ujenzi huo utaanza msimu wa 2017/2018 huku mechi ya mwisho Tottenham kucheza kwenye uwanja wa White Hart Lane itakua Mei 14 watakapowakaribisha mashetani wekundi; Manchester United. Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema uwanja mpya wa timu yake utakua wa kisasa zaidi na utakuwa na sifa za kuchezewa michezo ya American Football.

Tottenham wataanza kuutumia uwanja wao mpya kwenye msimu wa 2018/2019.

Post a Comment

0 Comments