Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kamati Ya Olimpiki Tanzania Yatoa semina Ya Siku Tano Kwa Wadau Wa Michezo mkoani Manyara.

Na,Kennedy Lucas-Babati Manyara.

                                                          Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC imeanza leo kutoa semina ya siku tano kwa wadau wa soka mkoani Manyara kwa lengo la kujifunza jinsi gani wataweza kuiendesha soka katika mkoa huo ambao mara nyingi imeshuudiwa kuibuka kwa migogoro kwa viongozi wake wa chama cha michezo.
Akifungua semina hiyo mkuu wa Mkoa Manyara Joel Bendera amesema imefikia hatua ambayo viongozi wa michezo kutambua mipaka yao ya kazi na kufanya kazi kwa uhadilifu ili kuondoa dosari ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Mafunzo hayo yanatolewa na Henry B.Tandau ambae ni makamu mwenyekiti wa kamati ya olimpiki Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa mafunzo ya utawala wa michezo na uongozi,huku akisaidiwa na Mama Irine Mwasanya mkurugenzi wa mafunzo wa kamati ya Olimpiki Tanzania.
Mwandishi wa Rorya24 News Kennedy Lucas akifanya mahojiano na Afisa Utamaduni mkoa Wa Manyara Charles Maguzu kuhusiana na Mafunzo hayo.

Msemaji Wa Vilabu Wilaya ya Simanjiro Charles Mnayalu akisikiliza kwa umakimi Mafunzo hayo.

Mkurugenzi Wa Mafunzo wa Kamati Ya Olimpiki Tanzania. Mama Irine Mwasanya akiongea na Waahiriki wa Mafunzo hayo.

Mkuu wa Mkoa Manyara Dr.Joel Bendera akiongea na Wadau Wa Michezo Mkoani Manyara ambao wanachukua Mafunzo ya siku Tano.
Waandishi Wa Habari Wakifatilia Mafunzo hayo .
Mwandiahi wa Rorya24News akifanya mahojiano na moja kati Ya washiriki katika Mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti Kamati Ya Olimpiki Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi Wa Mafunzo Ya Utawala Wa Michezo Na Uongozi Henry B.Tandau akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Manyara Dr.Joel Bendera.



Post a Comment

0 Comments