Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Umiseta Yaanza Rorya

Na Jacob Adongo-Rorya.

         Mashindano Ya Shule Za sekondari nchini Maarufu kama Umiseta imeanza Wilayani Rorya Mkoani Mara ambapo shule mbali mbali Wilayani humo Zimeshiriki katika Mshindano hayo ambayo pia wataunda timu moja ya wilaya itakayo kwenda kuiwakilisha Wilaya hiyo katika Mashindano Ya Mkoa




Lengo kubwa likiwa  nikutafuta vipaji kupitia mashindano haya ambayo kila mwaka  huwa yanafanyika lakini ikumbukwe kuwa Mashindano Ya Umiseta  Mwaka Jana yaliweza kusitishwa kutokana na agizo La Rais  Magufuli ya kuitaka  wizara ya Elimu kuelekeza pesa ambazo zingetumika katika mashindano hayo kununuliwa Madawati kwani isingependeza kama Mashindano hayo yanafanyika wakati shuleni wanafunzi wanakaa chini kwenye vumbi

Lakini Licha  Ya Wilaya Ya Rorya kushiriki katika Mashindano hayo inakabiliwa na Cjangamoto nyingi Kweli na baadhi Ya Changamoto hizo  ni.

(1)Kutokuwa na muda wa maandalizi kwa washiriki ambayo usababisha kutokuwa na washiriki waliokamilika kimichezo
(2)Kutokuwa na mipango mizuri inayopelekea washiriki au vipaji usika kutopatikana.
(3)kutokuwa na kanuni zakuendesha mashindano usika na atakama ipo basi uwa aizingatiwi.
(4)ukanda wa juu yani tarafa ya girango kutokuwa na mipango mizuri ya kuwaunganisha washiriki nakupelekea kundi ilo kutofanya vizuri pamoja kwamba ndiyo wenyeji kiwilaya.aiwezekani kukutanisha shule tano kwa siku moja na ukachezesha mechi kwa washiriki mpaka upate timu.hii ali kila mwaka washiriki wamekuwa awapati muda wa kutosha kuonyesha uwezo uwanjani.mchezaji anacheza dk 40 tu kweli muda huo unatosha mchezaji kuonyesha uwezo wake uwanjani?.timu zinafika majira ya sanne  mpaka michezo ianze ni satano sita.Ali hii kwakweli inarudisha nyuma wilaya yetu.niwaombe waandaji waweze kujifunza toka wilaya zingine jinsi wanavyoshirikisha vijana wao nakupata washiriki na vipaji usika.timu ya mpira wa miguu yawasichana kwa miaka miwili ndiyo mabingwa wa mkoa wa mara.lla wao ndowamekuwa awapati kabisa nafasi kwenyeshule ikifika muda wa mashindano ndiyo wanaulizwa nani anaweza cheza.na wanacheza dk 20 tu.
    Wilaya Ya Rorya ni Miongoni Mwa Wilaya nchini ambazo ziko chini Kisoka hvyo Viongozi wa chama cha Soka Wilaya FARM watumie fursa hii kuhakikisha wanachambua wachezaji wazuri na kuwalea katika maadili ya kisoka hili waje kuiletea wilaya iyo  eshima

Post a Comment

0 Comments