Mkurugenzi wa Halimashauri ya wilaya ya Rorya Ndg Charles Chacha akifungua semina ya mafunzo haya kwa waratibu elimu wa kata na waganga wa vituo vya vya afya amewataka kupokea na kufahamu jinsi mfumo huu mpya wa uhasibu ambao kwa sasa utatumika katika kusimamia pesa ambazo kwa sasa zitapelekwa vituoni kwa ajili ya kusimamia na kutoa taarifa iliyo sahihi.
Nae mtaalam wa mambo ya uhasibu wa mikoa ya shinyanga na Mara ndugu Ng'wananyamate Mgengeji Langalanga amesema lengo kuu la mradi huu wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma (PS3)kupitia ufadhili wa shirika la maendeleo la kimataifa la marekani (USAID) ni kuimarisha utoaji wa huduma bora hasa kwa wananchiwalioko maeneo ya pembenzoni.
Akishukuru kwa mafunzo haya waliyo yapata, Mganga mfawidhi kituo cha afya Utegi Judith Manonga amesema kwa mafunzo haya ni mwendelezo mzuri wa sasa kuwawezesha kufanya shuguli katika vituo vyao vya kutolea huduma kuwa na ufanisi mzuri tofauti na siku za nyuma.
Semina hii imefanyika katika ukumbi wa Soa Hotel rorya
Picha na kituo cha habari na mawasilisno rorya.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena