Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | China inavyotumia Vuguvugu la Marekani na Korea Kaskazini Kulinda Maslahi Yake

Image result for North korea and america

Kwa muda mrefu sana suala la Korea Kaskazini kujaribu makombora yake ya masafa marefu na mafupi imekuwa ni stori inayouza sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari na na watu wengi  wamejaribu kulizungumzia kwa mitazamo tofauti  tofauti!
Image result for china and north korea
Mimi Leo nataka nijaribu kuangalaia namna China anavyoweza kuwa nyuma ya vurugu hizi za Korea Kaskazini akiitumia kama karata yake mhimu ya kuhakikisha analinda maslahi yake hasa katika eneo hilo la Mashariki ya mbali. Msingi wa wasiwasi wangu juu ya China unasababishwa na  ukimya wa taifa hilo juu ya vurugu hizi za Korea Kaskazini, kama Marekani anahofia Korea Kaskazini kumiliki Makombora hayo, inawezekana vipi China ambaye yupo karibu kabisa aonekane kutokushitushwa na kinachoendelea Korea Kaskazini.

Hili  ndilo linanifanya mimi nifikirie na kuziona vurugu za Korea Kaskazini kuwa ni sehemu ya mikakati ya China kufanikisha moja ya jambo kubwa katika harakati za kuhakikisha inaimarisha maslahi yake  hasa ya kiusalama na kiuchumi. Kuliona hili kwa undani wake nimelazimika kurudi nyuma hadi mwaka 1961 ambapo nakutana na tukio moja maarufu sana la The Bay of bigs  invasion

Image result for The Bay of Pigs Invasion
The Bay of Pigs Invasion

Mwaka 1959  yalitokea mapinduzi katika taifa la Cuba, mapinduzi yaliyomuingiza madarakani Fidel Castro. Catro alikuwa ni muumini wa ujamaa hivyo mara baada ya kushika hatamu akanuka kuifanya Cuba kuwa taifa la kijamaa ambapo alitaifikfisha makampuni na mashirika mbalimbali yakiyemo ya Kimarekani huku akijenga urafiki na muungano wa Usovieti. Suala hili halikuwafurahisha Wamarekani hata kidogo, kwao Castro alikuwa mfano mbaya sana kwa watoto wengine hasa eneo la America Kusini, hivyo ilikuwa lazima wamshughukikie ili kuhakikisha ubepari unadumu.

Ndipo walipoamua kuja na mkakati kabambe wa kumuondoa Castro. CIA walipewa jukumu la kutekeleza mkakati huo na raisi wa  wakati huo bwana Dwight D. Eisenhower akiidhinisha jumla ya USD million 13.1.CIA waliwapa mafunzo raia wa Cuba hasa wale waliokuwa wakipinga ujamaa lakini tunaweza kusema mkakati ukaingia dosari kwani raising Dwight wakati anaondoka ulikuwa haujakamilika hivo ikabidi asubiliwe rais mpya.

Baada ya uchaguzi  J.F.Kenendy akatangazwa raisi na kupewa mkakati kwa ajili ya kuuidhinisha, Kennedy aliidhinisha lakini alihakikisha ushiriki wa Marekani katika utekelezaji wa mkakati kwenye uwanja wa vita unakuwa mdogo, waandaji wa mkakati walimkubalia matakwa yake japo walijua hali hiyo ingewaletea ugumu ila wakajipa moyo wakiamini mambo yakiwa magumu wangemshawishi ili aidhinishe uhusika zaidi wa Marekani kwenye uwanja wa mapambano.

Kama walivyotarajia japo mwanzoni walionekana kufanikiwa lakini mambo yalibadilika ghafla hasa baada ya Fidel Castro mwenyewe kuamua kuchukua majukumu ya kuongoza mapambano na baada ya siku tatu tayari waasi walikuwa wameshindwa. Kibaya zaidi mateka walipohojiwa mubashara kwenye televisisheni walielezea kila kitu kuhusu walivofadhiliwa na CIA.

Kitendo cha kushindwa kwa mkakati huu kilionekana kuwa fedheha kubwa sana kwa taifa la Marekani na zaidi kwa CIA, hivyo wakaapa kuhakikisha wanamng'oa Castro kwa njia yoyote.

Castro na Jamhuri ya Usovieti walikuwa wameliona hilo
Image result for Fidel castro and soviet
Kutokana na kipigo alichokuwa amekitoa,  Fidel Castro aliamini hakuwa salama, alijua muda wowote Marekani wangerudi tena wakiwa wamejizatiti zaidi na alijua kabisa Marekani iliyojipanga vizuri asingeweza kusimama naye, hivyo alihitaji mkakati madhubuti unaoweza kumlinda dhidi ya Marekani!
wakati huo huo

Muungano wa Usovieti chini ya uongozi wa bwana Nikita Khrushchev walikuwa wanaungalia kwa ukaribu mno mtifuano huo kati ya Marekani na Cuba huku wakiiona fursa kubwa mno katika mgogoro huo katika kuhakikisha wanalinda maslahi yao kiuchumi, kisiasa na kiulinzi,l. Ni katika nukta hii walipokuja kumpa mkakati kabambe Castro tunaoweza kusema ndio uliomfanya Castro kufanikiwa kuishi maisha yake yote na taifa lake la kijamaa pembezoni mwa bwana mkubwa na msimamizi wa ubepari duniani wakati nchi zilizopo maelfu ya maili kutoka Washington zikiwa zimejisalimu amri, WALIMPA MAKOMBOLA YENYE UWEZO WA KUSHAMBULIA SEHEMU KUBWA YA MAREKANI.!!

Kwanini na ilikuwaje?

Tunaweza tukasema moja ya sababu ya wazi kabisa ya wasovieti kuamua kuingilia kati ni kwa kuwa wao ndio walikuwa baba wa ujamaa na Fidel Castro alikuwa moja ya mshirika mkubwa wa Usovieti na mfano kwa wengine wengi waliotamani kuishi katika mfumo huo, hivyo kuiruhusu Marekani kumuondoa Castro kungekuwa mfano usio mzuri kwa watoto wengine waliokuwa wameamua kufuata mfumo wa ujamaa. Lakini pia wasovieti walikuwa wameiona fursa nyingine, fursa ya kutengeneza mgogoro mkubwa kati ya Marekani na Cuba, mgogoro ambao ungemlazimisha Marekani kuja kwenye meza ya mazungumzo wakiwa na matakwa matatu:

1. Kuwalazimisha Marekani kuutangazia ulimwengu kuwa wamestisha na hawatakuja kujaribu tena kuivamia Cuba!

2.  Kuilazimisha Marekani kuyaondoa Makombora yake katika nchi za Uturuki na Italia yaliyokuwa na uwezo wa kushambulia hadi Moscow

3. kuilazimisha Marekani na washirika wake  Ufaransa, na Wingereza kuondoka eneo la Berlin Magharibi kwakuwa uwepo wao ulikuwa unatishia uhai wa Ujerumani Mashariki eneo ambalo Usovieti alikuwa akilitumia kama eneo lake mhimu kwa ajiri ya mapambano wakati wa vita baridi.

4. Raisi wa Urusi bwana Nikita Khrushchev alikuwa akiamini Raisi wa Marekani bwana John F. Kennedy alikuwa Raisi dhaifu hivyo ingekuwa raisi kupata kile walichokuwa wanakitafuta, kwa maneno yake alisema:"Keneddy ni kijana mwerevu, lakini ambaye ni mwoga wa kufanya maamuzi magumu hasa kwenye kipindi kigumu, mwerevu sana na dhaifu mno,  Keneddy would make fuss, make more fuss and then agree"


Hivyo basi baada ya kumpa mkakati huu kabambe na kufanyika mikutano kadhaa kati ya viongozi wa nchi hizi, mwanzoni mwa mwaka 1962 Cuba ilipokea ugeni wa wataalamu wa utengenezaji Makombora wakiwa kama sehemu ya maafisa wa kilimo kutoka Usovieti walioidhuru Cuba baadae wataalamu hao waliingia kazini Rasmi nchini Cuba kama wataalamu wa umwagiliaji, waendeshaji wa mitambo na wataalamu wa kilimo! Baada ya hapo Makombora yalianza kupelekwa kwa siri, hadi hapo bwana Nikita Khrushchev alikuwa ameamua kuivagaa Marekani with more than words.

Hapa chini ni rais Nikita Khrushchev na rais Fidel Castro na Makombola ya Marekani nchini Uturuki na Italia.

Moja kati ya maeneo ambayo Marekani walikuwa wameyawekea uangalizi wa hali juu basi ni Cuba, lakini cha kushangaza wasovieti walifanikiwa kuingiza makombora bila kugundulika. Haikuchukua muda Marekani wakapata taarifa za intelejensia ya kile kilichokua kinaendelea na haraka wakaanza kufanya uchunguzi na baadae mnamo 14 Octoba ndege ya uchunguzi aina ya U--2S ilifanakiwa kupiga picha zaidi ya 298 kutoka maeneo ya San Cristobal na Pinar del Rep province na baada ya kuchambuliwa wakajiridhisha Cuba ilikuwa na Makombora.

Haraka haraka rais Kennedy akajulishwa na kikaandaliwa kikao cha wakuu wa vyombo vya ulinzi wakiwa na mlolongo wa mapendekezo ya namna ya kupambana na hali iliyokuwa mbele yao, haya hapa ni baadhi ya mapendekezo hayo:

1. Tusifanye chochote kwani tishio la makombora ya Usovieti dhidi ya Marekani halikuwa jambo geni

2. Diplomasia; zitumike njia za kidiplomasia kuilazimisha Usovieti kuondoa makombora yake Cuba

3. Mikakati ya kisiri; zitumike njia za siri kuwasiliana na Fidel Castro na wampe machaguo mawili, achague kuachana na Usovieti au wamvamie kijeshi

4. Uvamizi wa kijeshi; wafanye full invasion na wamuondoe Castro madarakani

5. Mashambulizi ya anga; wafanye mashambulizi ya anga kwenye maeneo yalipokuwa makombola

6. Waweke vizuizi dhidi ya Usovieti  kuingiza tena makombora Cuba

Baada ya kikao wakuu wa vyombo vya ulinzi wakakubaliana kwa kauli moja kuwa full scale--attack and invasion ndo lilikuwa chaguo  mujarabu wakiamini Usovieti isingefanya chochote kama wataishambulia Cuba!

Lakini wakashangaa...

Walipopeleka pendekezo lao kwa rais John F. Kennedy lilikataliwa, na Kennedy alisema maneno machache tu:

Hawawezi baada ya maneno yote haya kuturuhusu kuharibu vijana wao bila kufanya lolote, kama hawatachukua hatua Cuba kwa uhakika watafanya hivyo Berlin.

Ksisitiza msimamo wake kwa kusema Marekani wangeonekana watu wa ajabu kama wangekubali kuipoteza Berlin na kuwakatisha tamaa washirika wao wa ulaya eti kwakuwa tu hawawezi kulimaliza tatizo la Cuba kwa mazungumzo, wanajeshi wakaamua kurudi kwenye meza na kwa shingo upande wakarudi na pendekezo la kuzuia Usovieti isiendelee kupeleka Makombola.


Marekani wanatekeleza agizo lakini moto unawaka

Baada ya kukubaliana hatimaye Marekani waliblock safari za vyombo vya maji vya Usovieti kwenda Cuba hata vile visivyokuwa vya Usovieti ili kupita vililazimika kukaguliwa, rais wa Usovieti bwana Nikita alilaani hatua hiyo nakuiita kuwa ni uchokozi wa wazi wazi amabao ulikuwa hauvumiliki hata kidogo!

Hali ikawa tete zaidi baada baada ya matukio yaliyofuata baada ya hatua hizo, kwa mfano  ripoti ya CIA kuonyesha Makombora yalikuwa operational, na baadae kupotea kwa helkopita mbili katika eneo la ghuba ya Mexico huku CIA wakidai zimeangushwa japo hadi Leo wapo wanaodai zikikuwa ni njama za CIA kujaribu kumlazimisha Kennedy kuruhusu uvamizi! Mtifuano haukuishia hapo ambapo ndege ya uchunguzi aina ya 2--US kwa bahati mbaya na bila kuruhusiwa ikakatiza kwenye anga la Usovieti eneo la Mashariki, Wasovieti wakajibu kwa kurusha ndege aina ya MiG Fighters kutoka visiwa vya wrangel, Marekani nao wakajibu kwa kurusha ndege vita aina ya F--102 ikiwa imebeba makombola ya kinyuklia na kuilekeza katika eneo la Usovieti!
Tifu hili lilifikia hatua ya juu sana mnamo Octoba 27 pale Meli vita ya Marekani ilipogundua uwepo wa nyambizi ya Usovieti na kusababisha kuletwa meli vita zingine na baadae kujaribu kuishambulia, hali hii alifanya nyambizi hiyo kukaa chini kwa muda mrefu kitu kilichosababisha hewa kuanza kupungua, na kuwacha maafisa wa kisovieti ndani ya nyambizi hiyo kubaki na chaguo moja, kujihami. Ambacho wamarekani hawakujua ni kuwa nyambizi hiyo ilikuwa na kombora la nyuklia aina ya Torpedo lenye kilo 15 na maafisa walikuwa na full authority ya kulitumia kombora hilo lakini kwa sharti kuwa lazima wote wakubaliane, hivyo baada ya kuzidiwa wasovieti wakataka kuliachia kombora hilo, bahati nzuri mmoja kati ya wale maafisa aliyeitwa  Vasili Arkhipov akagoma, kwa lugha nyingine akawa ameiokoa dunia kutoka kwenye janga la vita ya kinyuklia!

Ngoma ilizidi kuwa nzito marekani wakajiandaa kwa ajiri ya vita, huku washirika wake mhimu kama vile Canada, Ufaransa, Ujerumani magharibi na Wingereza wakatarifiwa kuwa wajiandae kwa ajiri ya hatua za kijeshi,

Jamii ya kimataifa nayo haikuwa nyuma wapo waliokuwa nyuma ya Usovieti mfano wachina wengine wakiwa upande wa Marekani mfano Wajerumani magharibi, wengine walibaki katikati na mmojawapo alikuwa Papa John XXlll ambaye alituma ujumbe kwa Usovieti na kuwaomba kutoziba masikio juu  kile alichokiita kilio cha ubinadamu na kuzitaka pande zote kufanya kila kinachowezekana!

Wanakuja mezani

Baada ya mtifuano wa hali wa juu kati ya mataifa mawili hatimaye wanaamua kukaa mezani, na baada ya mazungumzo marefu kati ya viongozi wa juu wa nchi hizo wakiwemo marais na hapa Usovieti ndipo wanapoitumia fursa hii kufanya kile walichokuwa wamekipanga.

Majadiliano yalikuwa makali mno huku rais F. Kennedy akipata upinzani mkubwa toka ndani, baadae wakikubaliana kwenye mambo kadha wa kadha na Kennedy alilihutubia taifa huku akiweka wazi kuwa marekani imestisha mipango yake yote ya kuivamia Cuba huku Usovieti wakikubali kuondoa makombora chini ya uangalizi wa Umoja wa mataifa! Lakini pia walifanya makubaliano ya siri ya Marekani kuondoka makombora yake katika maeneo ya Uturuki na Italia lakini katika hali ya kushangaza rais wa Usovieti akatoka na kuitangazia dunia kuwa kuondoa makombora yao Katika nchi hizo, Waturuki walipinga vikali swala hilo lakini haikusaidia kwani Marekani walilazimika kuyaondoa.

Mwisho wa picha wasovieti wakaua ndege wawili kwa jiwe moja, wakafanikiwa kumhakikishia usalama Castro na makombora yaliyokuwa yanawanyima usingizi yakaondolewa! Hawakufanikiwa kwenye dili la Berlin lakini walichokipata hakikuwa kidogo!!

Sasa basi.......

Kwanini nimeamua kurejea kumbu kumbu hii, ni kwa sababu naiona hali kama hii ndani ya kile kinachofanywa na Korea Kaskazini kikiwa katika picha ile ile na pengine ndio sababu kila Marekani anapojaribu kumtishia Korea Kaskazini ndivyo na yeye anavyozidi kupiga hatua zaidi za kuimarisha makombora yake.

Hiki ndicho kinachonifanya niamini kuwa China ndio aliye nyuma ya hili akitaka kutengeneza mgogoro mkubwa kati ya mataifa haya mawili na baadae hali itakapokuwa mbaya zaidi waje kwenye mazungumzo nukta ambayo ataitumia kucheza karata yake muhimu dhidi ya Marekani, ni karata dume hii.

Wote tunakubaliana kwamba kwa sasa China ni miongoni mwa mataifa makubwa zaidi matatu duniani na kama ilivo ada mataifa makubwa yote hupenda kuhakikisha maslahi yao yapo salama! Wote tunajua uwepo wa majeshi ya Marekani katika eneo la Rasi ya Korea, Japani na Ufilipino, bila kusahau kuonekana Mara kwa Mara kwa meli vita za Marekani zikiranda randa katika maeneo ya bahari ambayo China inaamini ni maeneo yake na siku za hivi karibuni kumekuwepo matukio ya meli vita za nchi hizi kukutana kwa uso katika bahari ya Pacific eneo la Mashariki ya mbali!

Hivyo basi China anajiona kama hayupo huru, hayupo salama na anaikosa hadhi ya kuwa baba katika eneo hilo, sasa anachokifanya ni kujaribu kuona namna ya kuuondoa ushawishi wa Marekani katika eneo hilo na yeye kujitwika majukumu ya kuratibu mienendo ya nchi za Asia, kiuchumi, kisiasa na kiulinzi!

Analifikiaje lengo hilo, ndio hapa sasa ninapoziona vurugu za Korea Kaskazini kama sehemu ya mkakati wa China kuyatimiza matamanio yake, anaweza asifanikiwe kuwafanya Marekani kuondoka kabisa katika eneo hilo lakini anaweza akafanikiwa kuwalazimisha kupunguza shughuli zao hasa za kijeshi amabazo ndio hasa zinatishia maslahi yake kufikia kiwango ambacho hakihatarishi maslahi yake hasa Yale ya kiusalama!

Haya ndio yamenifanya nifikiria na kuona kama hizi vurugu za Korea Kaskazini kama karata muhimu anayoicheza China dhidi ya Marekani huku nikiwa na kumbukumbu ya mchezo kama huo kuwahi kuchezwa miaka hiyo ya 1962.!



#TheBold_Write It

Post a Comment

0 Comments