Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Fahamu | Dar es Salaam ni jiji la watafutaji.

Image result for maisha ya dar

Kila mtu yuko bize kutafuta ngawira lakini gharama ya maisha huwa inakuwa kikwazo kwa wengi hasa wale ambao ni wabishi kujikana nafsi na kuwa flexible.

Kuna watu wanahamu ya kukimbia Jiji lakini inakuwa ngumu kwa sababu kuna fursa wanaziona na wanahisi zitatoa. Kuna wengine wengi wanasalimu amri na kurudi mikoani kama sio vijijjini.

Vijana Mabachelor na wale walio na familia lakini wanaishi maisha ya kawaida. Kuna wanaonunua tango 500TSH supermakert na wengine Matango manne Kwa hiyo hiyo 500Tsh jiji hilohilo. Mfano nenda sasa Buguruni sokoni Mia tano Unanunua Fungu la matango sio tango moja.

Dagaa safi kabisa ambao mwanza sokoni kisado ni 6000 hao hao kuna mahala DSM unakuta wanauzwa 6000 Utadhani huwa wanaletwa na Malori ya Makinikia.

Mchele upo 2000TSH kwa kilo lakini kuna wataalam wanaununua huohuo au wenye hadhi karibu na huo kwa TSH 1300 au 1400/1500 kwa kilo.Ukipita masoko ya michele ndio utaelewa vzr.

Wengine JioniJioni badala ya kujipikilisha ubwabwa au ugali, wanakula chapati safi kabisa mtaani panapoaminika na maarage anapata kitu kile kile ambacho angekipata akifakamia wali maharage ila hapo anakuwa anatumia gharama ya chini na kaokoa mapesa.

Asubuhiasubuhi wengine badala ya kununua mkate wa Buku+ ananunua mihogo ya kukaanga au kuchemsha hapo kwa mama nanii jirani hata miatano haiishi lkn anashiba anaweza asile hata mchana.

Kuna wataamu wa kucheza na misimu ya vyakula na matunda, Unakuta jamaa anaafya safi kabisa na menyu muda wote imekamilika lakni analipwa mshahara 300,000/= au 400,000/= huku anasomesha watoto. Wakati huohuo kuna jamaa analipwa 3,000,000+ lakini kakondeana analalamika maisha magumu asubuhi hadi usiku wa manane.

Kuna mwingine Amefungua Ujasiliamali analipia frame 100,000 au 200,000 lkn kwa siku anauza akikomaa sana 11,000. Hapo Luku hujatoa, EFD,TRA, Halmashauri,Gharama ya usafiri kurudi nyumbani,Pesa ya Usafi etc wakati huohuo unakutana na Mpiganaji kabana kwenye kona moja ya jiji na kagenge flani ka ovyoovyo halipi chochote akiongoka ni baiskeli hata daladala hapandi lakini anauza hadi laki 2 kwa siku.

Ukienda kwenye mavazi,Viatu na Urembo huko ndio kuna kila aina ya Michanganyika kulingana na maisha uliyochagua, Hata ukitaka suti Ipo ya hadi 2M+ pia unaweza Kununua Suruali nyeusi 4000, na koti zuri 10000, ukajichanganya kanisani au kwenye harusi na unakonekana kama BLACK AMERIKA amekuja Bongo kukagua Miradi yake kila mtu anataka awe karibu na wewe...


Kama HUJUI HESABU ZA ASILI (Sio za Shule) njoo ujionee hawa jamaa maisha yao.
Hawa jamaa hapa jijini Wanaakili nyingi sana na zinatofautiana kwa mbali sana.

Post a Comment

0 Comments