Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Kidon : Kikosi Kazi Maalum cha Mauaji ndani ya Mossad

Related image
Akiwa amesimama kwenye meza ya kantin huko Tel Aviv…. Mwalimu wa Ujasusi wa Israel alikuwa akiwatizama na kuwasoma wanawake na wanaume wanaopita mbele yake ambao ni watumishi wa shirika la kijasus la israel la Mossad.

Katika wiki chache baada ya kuichukua Mossad Meir Dagan alikuwa ameongoza mambo kadhaa ambayo wenzake hawakuwa wameweza kuyafanikisha.

Ni mara chache sana utamsikia akizungumza. Alikuwa mkimya na mwenye kuonekana anafikiria kila wakati.

nlipokuwa kwenye mapambano Lebanon nlishuhudia mmoja ya wanafamilia akiuawa. Kichwa chake kilifumuliwa na Ubongo kumwagika kwenye sakafu. Pembeni yake ilikuwa imelala maiti ya mke wake na baadhi ya watoto wake. Kabla sijaamua kufanya lolote mmoja ya wale wauaji alichota ubongo kwa kiganja chake ambacho kilijaa ule ubongo halafu akameza. Akasema hivi ndivyo ambavyo utafanya kazi ama sivyo siku moja kuna mtu atakuja kula ubongo wako”
Related image
Meir Dagan | Kiongozi wa zamani wa Mossad
Maneno yake yalikuwa makavu kabisa pasipo hisia yoyote ile ya huruma au kigugumizi kiasi kwamba kwa waliokuwa wakimsikiliza wangeweza kugangamaa kwa uthahibiti kabisa kama wamepigwa ganzi.hakuwa ni mtu wa mchezo.

Pale kwenye mgahawa walikuwepo ambao walikuwa wameshaua mara nyingi hapo kabla. Ilikuwa ni kawaida kuua maadui ambao haiwezekana kuwaleta mbele ya mahakama kuhukumiwa kwa kuwa pengine wamefichwa huko ndani ya nchi za kiarabu zenye uadui na Israel.kwa hiyo hao ilikuwa ni kuwafuata huko waliko na kumalizana nao kimya kimya.

Ni Mossad tu ambao walikuwa na Ujuzi na Uwezo wa kuwatafuta na kuwaua. Rafi Eitan Mkongwe aliyekuwa Mkuu wa Mikakati na Utekelezaji wa Mossad aliniambia tukiwa tumekaa pamoja sebuleni katika viunga vya Tel Aviv.

“ Mara zote Nilikuwa najaribu kuua waakati napoona macho ya huyo mtu yamekuwa meupe kutokana na kuakodoa ili niweze kuona Hofu yake. Niweze kunusa Pumzi yake. Wakati mwingine nlitumia mikono kuua. Kisu au Bunduki/bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Kutokana na unyama ambao walikuwa wanatufanyia nilijikuta nafurahia kuua na kamwe sikuwahi kujuta kutokana na mauaji nliyoyafanya”

Meir Amit. Alipokuwa Mkurugenzi wa Mossad aliwah kusisitiza baadaye “ Sisi ni kama tumethibitishwa kunyonga au madaktari wa vifo katika Gereza la wafungwa wanaopaswa kuuawa. Matendo yetu yamepewa ithibati na Serikali ya Israel. Mossad anapoua havunji sheria ila anakuwa ametimiza Hukumu iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Kipindi hicho”ilikuwa hamna kigugumizi linapokuja suala la kulinda raia wa Nchi yetu kwa gharama yoyote ile. Utaifa ulikuwa kwanza mengine baadaye." baada ya kuongea maneno haya alimeza mate kuonesha ameweka nukta au anafurahia Ujasiri wake.
Related image
Meir Amit akiwa na viongozi waandamizi wa Nchi ya Israel
Tulikuwa tunazungumza huku tunatembea eneo la kumbukumbu ya Mossad kwa waliofariki.Kulikuwa na umbo gumu kabisa ambalo limetengenezwa kama Ubongo na kila jina la marehemu lilikuwa limechongwa juu yake. Hii ilikuwa ni kumbukumbu kwa wana Mossad ambao walikufa wakiwa katika majukumu ya kuwaua maadui wa Israel. Hawa walikuwa ni mashujaa.

Baadhi ya hawa maajenti walikuwa na kitu kimoja kinachofanana Amit alikuwa amewatuma kwenda kuhudhuria vifo vyao wenyewe. kwa hiyo ilikuwa unakuwa umeamua kusaini hati ya kifo chako pia.

tulifanya kila tulichoweza kuwalinda. Tuliwafundisha vyema kuliko majasus wowote wale duniani lakini unapokuwa kwenye misheni lolote laweza kutokea na pia huko wapo wenye uwezo mzuri ambao wanaweza kucheza vyema karata zao"

Dagan , waliokuwa wakimsikiliza kwenye huo mgahawa walijua jina lake pia lilikuwa limewekwa katika kumbukumbu hiyo ya watu mashujaa. Huyu alikuwa anajulikana kwa kuweza kuwalinda kwa kila namna aliyoijua. Aliweza kuruhusu kutumia sumu ya kwenye nerve iwe kwa kibali au pasipo kibali. Angeweza kuwaruhusu kutumia dum dum bullets hizi zilikuwa ni risasi maalum ambazo zilikuwa ikipigwa ikaingia mwilini inapasuka na kule mbele inachanua. Hivyo inapotoka inachana sehemu kubwa ya mwili na kuacha shimo kubwa sana kuliko risasi za kawaida) hii njia hata Mafia, KGB na hata Chinahawakuwah kutumia. Ila hakusita kutumia risasi hizi ili kuhakikisha analinda usalama wa Israel kwa gharama yoyote.
dum 2.jpg dum dum 1.jpg 
Hizi ni Risasi za Dum Dum na namna zinavyoleta madhara mwilini. 


Haya ni mambo ambayo wote waliopo kwenye ule mgahawa walikuwa wameyakubali na walikuwa tayari nao kuyafanyia kazi.

Dagan, huyu alikuwa ni mtu pekee wa kumi kushikiria nafasi ya Uongoz Mossad na kuwa na kupewa cheo cha memune“yaani huyu alikuwa daraja la juu la kwanza katika waebrania” aliwakumbusha waliokuwa wanamsikiliza kukaa kwenye viti vya plastiki kitu ambacho alikuwa hapo kabla ameshakisema Meir Amit. Halaf Dagan akaongeza . "nipo hapa kuwaambia kuwa siku hizo zimerudi tena" 

Dagan akaruka kushuka kwenye meza na akaanza kutembea kutoka kwenye Mgahawa kukiwa kimya kabisa. Mara makofi yakalipuka na vigelegele vya kumshangilia. Huyu alikuwa Jasusi aliyekubuhu na mwenye akili zisizo za kawaida.ukimwona tu anavyotembea unagundua hakuwa mtu wa kawaida.

Ni muda mfupi baadaye tukaja kusikia mauaji yaliyotokea huko Mombasa Kenya. Siku kama kumi na moja zilizopita. Gari lililokuwa na bomu liliendeshwa mpaka maeneo ya mapokezi ya Hoteli iliyokuwa inamilikiwa na Muisrael ikifahamika kama Paradise Hotel.

Watu kumi na tano walifariki na wengine 80 walijeruhiwa. Na wakat huo huo makombola mawili kidogo yaiangushe ndege ya Abiria ya Israel iliyokuwa inawarudisha Watalii Tel Aviv kutoka Kenya. Watu 275 walikoswa koswa kukutwa na kifo kilichofanana na cha Lockerbie.

Meir Dagan haraka akahisi hiyo itakuwa ni kazi ya Osama Bin laden na kundi lake la al-quaeda na yale makombola yalikuwa yametoka katika jeshi la Iraq.

Huu ulikuwa wakati wa Meir dagan kurusha kete yake. Kila mtu aliyekuwa amethibitishwa kuwa ana uzoefu wa shughuli kama hizi alikuwa amepandishwa ndege kuelekea Kenya sehemu yalipotokea mauaji. Huko wangechunguza mabaki kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa walivyokuwa navyo. Walikuwa na ving’amuzi ambavyo vingeweza kugundua kitu chochote hata kwa udogo wa sindano kilichokuwa kwenye maiti ambacho kingeonesha huo mlipuko umetokea wapi. Yaani ulipotengenezwa. Na mengine kadhaa ya kiuchunguzi.

Hiyo timu ya majasusi walisafiri kila mtu kivyake kama ambavyo mara zote hufanya. Walikuwa na ndege tofaut na marubani wao peke yao walikuwa ni wanaume na wanawake wa KIDON… hawa ni wauaji Mahiri wa siri wa Mossad. Usiombe ukakutana na KIDON hawa huwa wanafurahia kuua na ni wakatili na wapo makini sana kwenye kuua na kutoacha alama ya kuwafanya wajulikane wao. Ndani yao walikuwepo wafagiaji.cleaners/sweepers hawa ni wataalam wa kuondoa ushahidi unaolekeza kwao na pengine kupandikiza mwingine.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kujipenyeza na Mombasa na kuwatafuta wauaji Husika na kuwafanya wawataje waliopanga hilo shambulio na mwishoni kuwaua wote popote watakapokuwa.ingeweza kuchukua siku,wiki,miezi hata miaka kama ilivyokuwa walipolipiza mauaji ya wanamichezo wa Israel huko Munich mwaka 1972.

Hawa walikuwa na ujuzi wa kutengeneza sumu ambayo ingekaa kwenye vijichupa vidogo mpaka wakati wa kuitumia. Walikuwa na visu virefu na vifupi. Walikuwa na nyaya za piano za kwa ajili ya kunyongea,mabomu yaliyokuwa na size ya kidonge kama vicks kingo ambayo yalikuwa na uwezo wa kupasua kichwa cha mtu vibaya vibaya. Walikuwa na bastola, na bunduk zinazotumika na snipers zenye uwezo wa kuua toka umbali mrefu.

Timu iliyokuwa imechaguliwa kwenda Mombasa ilikuwa na ujuzi mzuri wa kuzungumza lugha ya wenyeji ya Kiswahili na lugha nyingine za wenyeji. Bila kuwatilia shaka. Nao walijichanganya na wenyeji wakavaa kama wenyeji, wakashiriki kwenye shughuli zote kama kwenda klabu,kucheza ngoma za kienyeji na mambo menine ambayo wenyeji walikuwa wakiyafanya. Zaid zaid walikuwa na lugha yao tofauti ya kipekee ya kuwasiliana wao kwa wao.

Walikuwa wamejifunza namna gani ya kuweka kumbukumbu ya kila tendo linalofanyika na hata kuwatambua watu na kuwatolea maelezo. Walikuwa wanajua namna ya kuingia kwenye ofisi pasipo mwenye ofisi kujua ofisi yake kuna mtu aliingia kwa maana ya kuwa wakiingia watatafuta wanachotaka na kurudisha kila kitu kama mwanzo.iwe ni chumbani au sehemu yoyote ile wangeingia na kuweka vinasa sauti au mabomu. Masluh , huu ulikuwa utaalam wa kuwapoteza au kumpoteza mtu anayekufuatilia .

Wanawake walikuwa na utaalamu wakutumia jinsia na uzuri wao. Na walikuwa wapo tayari kulala na mtu yeyote ili waweze kupata habari muhimu. Uhusiano wa sex na kazi za kipelelezi hii ni mbinu ya zamani ambayo haikuwah kupitwa na wakati. Si unajua mwanaume mbele ya mwanamke? Wanasema mkate hata uwe mkubwa/mgumu vipi kiboko yake chai” Merit Amit aliwah kuzungumza kitu kama hicho akihusisha sex au wanawake na mambo ya kipelelezi .

Sex hii ni silaha kubwa ya wanawake. Pillow talk si tatizo kwa mwanamke. Ila jambo hili linahitaj aina flan ya ujasiri si kawaida kawaida tu. Na hapa suala si kulala au kufanya mapenzi tu na adui ila ni kupata taarifa na kuna namna ya kuzipata taarifa hizo. Hivyo walikuwepo watoto wakali sana waki Israel mitaa ya huko Mombasa wakizurura zurura na watu walipenda wapate nafasi ya kuwabambia. Ila hilo lilikuwa linawezekana kwa walengwa tu.

Team ya KIDON ilikuwa imepitia Mafunzo hatari ya Miaka miwili huko Henzelia karibu na Tel Aviv ya jinsi ya kuua kwa namna mbali mbali na walioaulu ndo walikuwa wanachaguliwa kuwa wana KIDON. Baadaye walipelekwa tena Jangwani kwenye kambi Maalum huko Negev walifundishwa zaidi namna Ya KUUA.

Jinsi ya kutumia ipasavyo silaha kwa mlengwa. Kukaba kwa kutumia kisu cha kukatia cheese ikiwa mhusika inapaswa auawe usiku. Matumizi ya bastola zenye kiwambo cha kuzuia Sauti. Matumiz ya sindano za sumu n,k alielezea Victor Ostrovsky aliyewah kuwa Mwanachama wa Kidon.

Victor Ostrovsky ambaye aliishi Huko Arizona kamwe hawezi taja ni akina nani aliwaua. Ila aliamua kuachana na Kidon anasema hakuweza kuvumilia mambo aliyokuwa akiyafanya. Chanzo changu cha taarifa cha mossad akanambiwa mambo yamebadilika kwa sasa hatutumii njia zile zile za miaka ile na kwa maana ya kwamba sasa ni Balaa zaidi. USIOMBE UKUTANE NA MWANA KIDON.

Mtu aliyefahamika kama injia wa mipango ile ( Mashambulizi ya Mombasa) alikuwa ni Mtu wa Hamas mtaalam wa kutengeneza mabomu ambaye aliishi ukanda wa Magharibi akilindwa na watu wenye Bunduki masaa 24x7x12.

Siku moja alipokea mgeni ambaye ni mpwa wake wa mbali kutoka Gaza . alikuwa kijana aliyekuwa akiongea kwa hisia na kuonesha mwenye mapenzi sana na Uislamu wenye Itikadi kali. Huyu tungeweza kusema alikuwa mnazi wa uislam wenye Imani Kali. Baadaye wakawa wakipata Chai ya mint. Hawa watu wawili walizungumza sana mpaka jioni. Mwishoni Yule Injia mtaalam wa Hamas wa kutengeza Mabomu akamwomba Yule bwana mdogo alale mpaka kesho yake wazungumze zaidi. Yule kijana akasita sita, Injia kasisitiza basi akakubali kwa shingo upande.

Baadaye akaomba kuwa basi apewe simu aweze kuwaambia ndugu zake kuwa hatorudi siku hiyo nyumbani. Alipokuwa akiongea akaonekana mawasiliano si mazuri sana akaomba kama inawezekana akaongee nje pengine network ipo vizuri. Yule Injia alimkubalia. Baada ya muda akarudi ndani na kumkabidhi simu yake. Wale jamaa wawili walinzi wakalala pembeni sakafuni punde simu ya Injia ikaita. Alipoiweka sikioni aanze kuongea Kichwa chake kililipuliwa na ukawa mwisho wake.

Yule kijana alikuwa mmoja ya wana Kidon kiengo cha MOSSAD ambaye aliweza kuweka Mlipuko wenye nguvu kwenye simu. Na detonation au kibanzio(signal) ya kilipuzi ilitoka umbali wa nusu Mile kutoka pale walipo. Hakuna aliyekuwa amemwona Yule kijana akiingia wala akitoka eneo.ikaishia hapo.
.............................................................................

Operations Zaendelea Sehem Mbalimbali Duniani.

Kwa miaka kadhaa iliyopita Mossad walitumia mbinu hii maeneo mbalimbali pia kuwaua maadui zao. “tunajaribu kutotumia njia moja katika kufanya mauaji yaliyokusudiwa hivyo mara nyingi huwa tunajaribu kuvumbua njia mbalimbali za kuwaua maadui zetu” alisema mmoja ya waliowah kuwa maofisa wa Mossad.

Kwenye list yao ya wanaopaswa kuuawa alikuwepo Fathi Shkaki aliyekuwa kiongozo wa Islamic Jihad na Gerald Bull huyu alikuwa mcanada ambaye ameasi na kuwa Mtaalam wa kutengeneza Silaha wa Saddam Hussein. Aliweza kutengeneza Bunduki kali kabisa kwa kuwa alikuwa amepata mafunzo mazuri sana huko kwao Canada.

Mara nyingi Timu ya kifo ilikuwa inaundwa na watu wanne. Mmoja huyu anamtafuta mlengwa alipo au jina lingine “Target Locator” huyu angemfatilia mlengwa popote alipo pasipo kumpoteza huku akiwasiliana na wenzie. Halafu kuna Msafirishaji au “The Transporter” huyu alikuwa na kazi ya kuwasafirisha wanatimu mpaka sehem salama kutoka sehemu ya tukio la mauaji. Alikuwa ni dereva mzuri sana ambaye pia ameshayajua vizuri maeneo yote kwa njia zote akifahamu wapi kuna foleni,wapi hapapitiki n.k

Wawili waliobakia hawa ndo walikuwa wauaji wenyewe sasa. Kwa upande wa mauaji ya Gerald Bull walienda kumgongea mlango wake wa mbele jioni moja. Wakati huo mtaalam wa Milipuko alikuwa ameshafika na kuwahakikishia kuwa kila kitu eneo lile kilikuwa salama baada ya kuwa pia wamewasiliana na mtu wao mmoja aliyekuwa mle mle Iraq. Hawa wasaidizi walikuwa wakifahamika kwa kiebrania kama Sayanim neno linalomaanisha wasaidizi. Duniani nzima wapo maelfu na maelfu wametawanywa. Kazi yao huwa ni kuwasaidia waisrael wenzao kunapokuwa na tatizo au nchi inapohitaj taarifa za kishushushu. Kila nchi duniani wapo kwa rangi mbalimbali. Hawa walichaguliwa kwa umakini sana na kupewa mafunzo maalum na walikuwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia Kidon wanapohitaj msaada wao. Na hapa walikuwa tayari kuwasaidia kidon kumuua Bull.

Jinsi ya Kumuua ilikuwa Rahisi sana. Wana Kidon hawa walivaa sare za FedEx. Mmoja akawa amebeba kamzigo au package na mwingine aligonga mlango. Bull alifungua mlango. Alipofungua tu akarushiwa kile kijimzigo akarudi nyuma kwa mshtuko akapigwa Risasi akaangukia sebulen kwake. Jamaa wa kidon wakaokota kile kijimzigo na kufunga mlango wakimwacha Bull ameshakufa. Wote wawili wakatembea kwa utulivu kabisa kuelekea alipokuwepo msafirishaji. Ndani ya masaa kadhaa walikuwa Tel Aviv wakigongeana glass za wine au maji kama kawaida.

Maandalizi na Mazoezi ya Kufanikisha tukio la Mauaji.

Mara nyingi maandalizi ya mauaji huchukua wiki kadhaa na wakati mwingine hata miezi. Timu ya mauaji inapochaguliwa inapelekwa kwenye moja ya nyumba za Mossad zilizoko Israel.

Ni nyumba ambazo huwezi kuzidhania jinsi zilivyo. Na ilikuwa ni katika nyumba kama hizo walipokuwa sasa wanajiandaa kupanga namna ya kumuua Saddam Hussein. Walikuwa wmaepanga kumuua Saddam alipokuwa akitembelea moja ya michepuko yake( mistresses ) Ajent Mmoja wa Mossad aligundua kuwa mmoja wa aliyekuwa mjane wa Mwanajeshi mmoja wa cheo cha juu wa Iraq ailikuwa apelekwe sehemu flan kwenda kukutana na Saddam Hussein kwenye moja ya Majumba yake ya kifahari huko Jangwan nje ya Jiji.

Mossad waliamini kuwa kulikuwa kuna nafasi wakati Saddam akishuka kwenye helkopta yake anapoelekea kwenye hilo jumba. Hilo jumba lilikuwa na ulinzi mkali sana. Mpango wa kumuua Saddam ulikuwepo kipindi Kirefu tu lakini mara nyingi waliahirisha kwa sababu Saddam alikuwa na tabia ya kubadilisha ratiba mwishoni kabisa mwa safari zake. Yaani kama ilikua aende Ubungo basi ataghairi na kwenda Temeke. Au atabadilisha ratiba n.k

Mossad waliamini kwa kipindi asingefanya hivyo sababu Saddam alikuwa anampenda sana yule mwanamke.

Yakaanza kufanyika mazoezi maeneo ambayo yalikuwa yanafanana katika Jangwa la Negev. Makomandoo wa Kiisrael wakaweka ulinzi mara mbili ya ule alio nao Saddam.Msafara wa Saddam wa Badnia ukawa unashuka mpaka karibu na hilo jengo ambalo lilijengwa kufanana na villa alilokuwa anaenda Saddam Wanakidon kadhaa walikuwa wamejiweka sehemu sahihi kwa ajili ya Kumshoot Saddam wa bandia. Lakini kushoot kwao kulikuwa tu ni kushoot kwa mazoezi na hakukuwa kumewekwa makombola halisi. Kwa bahati mbaya kabisa kumbe walikuwa wamesahau katika yale mazoezi kuna moja ya kombola halisi liliwekwa na hivyo likawa fired na kuua aliyekuwa Saddam wa bandia na walinzi wake. Mpango huu ukawa cancelled yaani uka hairishwa.

Lakini wiki iliyopita Meir Dagan alikuwa anafikiria kurudia tena zoezi hili kwa mara nyingine kwa ajili ya kumuua Saddam. Baada ya upelelezi wa siku kumi na moja Timu yake iliyokuwepo Mombasa ilimwambia kuwa waliohusika na tukio lile walikuwa ni Al-Qaida na si Saddam.

Akazidi kupewa taarifa kuwa kwa suala la Sadda ni muda tu ila kwa sasa wakimuua wanaweza sababisha vita. Akaambiwa watu wenyewe wa Iraq pia watafikia hatua watachoka naye hivyo ni suala la muda tu.

Dagan Mkuu wa Mossad usingeweza kuamini kuwa alizaliwa kwenye Train linalotoka Urusi kwenda Poland. Alikuwa na uwezo wa kuzungumza lugha kadhaa. Ni mtu wa vitendo akifanya kazi masaa 18 kwa siku. Maisha yake Binafsi ni rahisi sana hakuwa akipenda kuwa namna ya watu ambao wanaongoza MI6 au CIA. Mshahara wake ulikuwa ni sehemu tu ya wakuu wa hizo idara nyingine wakipata. Katika miezi mitatu tu aliyoanza kazi alikuwa akipendwa sana na watu wake.

Katika miaka iliyopita Mossad ilipitia changamoto nyingi sana ikiwepo kushindwa kuwa na jina zuri katik public na kupungua kwa mori na wananchi wenyewe pia walikuwa wakiikosoa sana. Ambacho Dagan alikuwa ameamua kukifanya ni kubadilisha hali hiyo kwa ujumla.

Hakuwa mpenzi wa kumsoma au kumwangalia James Bond mtu pekee Jasusi ambaye alipata kumsoma alikuwa na John Le Carre. Ila Dagan alikuwa akipenda sana kusoma historia ya intelejensia, na inasemekana alikuwa akifaham sana kuhusiana na CIA na MI6 kuliko hata wafanyakaz wa hayo mashirika ya Kijasusi. Siku zote alikuwa akiwasisitizia wafanyakazi wake kuwa ilikuwa haipaswi kuchelewa kufanya kitendo sahihi kwa wakati sahihi.

Tokea tukio la Mombasa litokee Dagan alikuwa mara nyingi akilala ofisini mwake ambapo dirisha la ofisi yake lilikuwa linatizama mashariki mwa Milima ya Yudea. Kipindi chote hicho Dagan alikuwa akiamini Osama amejificha Pakistan na kuwa kwenye lile Jangwa la Iraq siku moja Saddam anaweza kutaka kulitumia kukimbia kama vita vikimzidia. Hivyo akasema ataendelea kumsubiria tu.

Watu wa dagan walikuwa ni wastaarab na watulivu sana wanapokuwa na mashirika mengine ya Kijasusu kama CIA na MI6 pamoja na European Service. Wakiwa kazin Mossad hawakuwa na Urafiki na mtu. Ni mara chache sana kutaka kushirikiana na mashirika mengine. Utaratibu wao ulikuwa ni kufanya kazi peke yao. Wanaamini kuwa wao wanajua zaidi kuliko mashirika mengine linapokuja suala la Ugadi. Wamezungukwa na kuish na magaidi miaka yote. Na katika hili wanaweza kuwa sahihi.

Miaka 57 wakipigana huko Lebanon na maneno mbali mbali ya Mashariki ya Kati. Hili ni taifa ambalo limezungukwa na maadui wanaotaka kuliangamiza kabisa. Siku zote Israel wamekuwa wakihesabu Ushindi dhidi ya maadui wao. Dagan alikuwa mtu aliyenyooka hana kona kona anakwambia anachodhan anapenda kufuata kanuni na utaratibu alipigana vita vya kwanza vya Intifada Gaza mwaka 1971 na miaka miwili baadaye alipigana vita vya Yom Kippur . kwa yeye hili suala la Mombasa lilikuwa ni jaribio kwake na kwa Mossad pia. Na akataka kuonesha kuwa Mossad imerud jukwaani sasa kuwaonesha namna ya kulipiza. Nadhani wengi mmesoma makala ya Wrath of God pale Mossad walipoamua kuanzisha Operation ya Kulipiza vifo vya wana michezo wao waliouawa huko Munich Ujeruman.

Hakakuwa na Shirika lolote la Kijasusi lenye historia ya kufanya opareshen Afrika ya Kati. Katika miaka ya 1960 Mossadwaliwatimua majasusi wa Kichina. Na pia waliweza kumzuia Fidel Castrol kuleta mapinduz yake Afrika na kuwashinda KGB wa kuigeuza Congo kuwa sehemu yao ya kufanyia mapinduzi Afrika. Vilikuwa vita vikali na vya kutisha.

Kundi moja la Kigaidi liliwavamia Mossad huko Katsa Kongo na kumkamata mmoja kumrushia ndani ya mto aliwe na Mamba. Na wakawa wanachukua Video ya tukio hilo na baadaye wakatuma hiyo video kwa Mkuu wa Mossad wa eneo hilo. Alilipiza kwa kupandikiza Bomu lenye uzito wa Pound Mbili kwenye choo cha aliyekuwa Kiongoz wa Kundi hilo. Alipoenda kukaa kujisaidia lile Bomu lililipuka na Kulipua jumba zima na yeye kiongoz na wenzie 12 walifariki pale pale.

Mossad wamejenga taasis ya kufanya utafit huko Tel Aviv ambayo huwa inaandaa sumu kwa ajili ya shughuli za wana kidon. Wakat mashirika mengine kwa sasa hayaruhusu Maajent wao kuua. Kidon wao walikuwa hawazuiliw kuua ikiwa Waziri Mkuu ametoa agizo hilo kuwa mhusika anapaswa auawe kwa manufaa ya Ustawi wa Taifa la Israel. Ariel Sharon waziri Mkuu huyu alikuwa haruhusu kirahis kuua alikuwa mpaka apate ushahidi mkubwa kuwa Mhusika kweli ni tishio kubwa na anastahili kuuawa.

Mossad walikuwa pia wamepata mafunzo hata ya kuweza kuua na kufanya tukio lionekane kama ni ajali walikuwa na utaalam wa hali ya juu sana wa kuhakikisha kuwa kila kitu kinakaa vile ambavyo wao wanataka kionekani. Kuna sehemu walikuwa wanaua na kuacha hivyo hiyo iwe kama salamu kwa wengine kuwa wao ndo wamehusika. Na matukio mwengine ambayo hawatak kuhatarisha diplomasia na Mataifa husika huko walifanya matukio ambayo waliyafanya yaonekane kama ajali au wao wasihusishwe kabisa.

Hii ilikuwa Taarifa ambayo pia imebidi niifupishe kutokana na malalamiko ya wengi kuwa ni ndefu sana hivyo wanashindwa kusoma na wengine hata kuelewa. Haiwezi kuwa perfect kwa asilimia 100 lakini ni Elimu ambayo nimeamua kushirikiana nanyi hasa wapenzi wa habari za Kiintelejensia na Taasisi hizi za Kijasus za Kimataifa. Mwandishi hana uhusiano na ISRAEL lakini ni mtu anayetambua Mchango mkubwa wa Intelejensia katika Uchumi,Ustawi na Ulinzi wa Nchi. Hivyo kwa miaka mingi nimekuwa nikisoma habari za watu hawa KGB, MI6,CIA, MSS n.k kama kuna sehemu ya kuongezea usiste kuongezea. Mimi na wewe tutakaa uwezo wa Mossad lakini Majasusi wengine Duniani wanasema kwa Siri kuwa jamaa ni wazuri na kwa kuwa wao wanaishi maisha hayo kutokana na Mazingira yao. Hivyo Akili zao zinafanya kazi mara 10 zaidi ya Mataifa mengine. Hayo si maoni yangu.

Post a Comment

0 Comments