Kampuni ya Nissan imetengeneza kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu kiti ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.
Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.
Utafiti uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi..
Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari.
Teknolojia hii ni sehemu ya mpango ambao sio tu wa kufuatilia gari bali pia dereva anapokua anaendesha gari
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena