Mchai chai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake, lakini hapa nchini wengi huutambua mmea huu kama kiungo katika chai na husaidia kinywaji hicho kuwa na harufu nzuri.
Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Wengine huamini kuwa mchaichai huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Hizi ni baadhi ya faida za kunywa chai yenye mchai chai katika mwili wa binadamu.
1. Kuzuia kutapika
2. Kutuliza maumivu ya tumbo
3. Kupunguza makali ya homa.
4. Msaada kwa wenye tatizo la baridi yabisi,
4. Msaada kwa wenye tatizo la baridi yabisi,
5. Husaidia kusafisha figo
6. Huzuia tatizo la tumbo kuunguruma
7. Husaidia uyeyushaji wa chakula
8. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini.
9. Husaidia kupunguza maumivu kwa kinamama wakati wa hedhi
Chanzo: Mtandao
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena