CECAFA wameweka hadharani makundi mawili ya michuano hiyo, huku timu za Libya na Zimbabwe zikiwa timu waaliwa kwa mwaka huu.
Tmu ya taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) imepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya.
Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.
Kilimanjaro Stars itafungua dimba dhidi ya Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mpambano wa wenyeji Kenya dhidi ya Rwanda.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara kitarudi tena dimbani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9 na Rwanda kabla ya kumaliza na wenyeji, Kenya Desemba 11.
Michezo ya hatua ya makundi itachezwa hadi Desemba 12 na Nusu Fainali itaanza Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 utachezwa ,mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.
Uganda, The Cranes ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena