Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Wahuni Wa Ghana walivyoiliza Idara ya Ulinzi ya Marekani kwa zaidi ya miaka 10

Image result for internal security USA
Jumanne Nov 8 2016 dunia yote ikielekeza macho kufuatilia uchaguzi mkuu wa Marekani. kuna jambo kubwa sana lilitokea Accra ambalo lilikosa 'Air time' mubashara kutokana na media zote kuelekeza nguvu kwenye uchaguzi mkuu wa uraisi. Tukio hili la kustaajabisha, lililosukwa kwa akili kubwa sana na wahuni wa Ghana, na lilinipa sababu ya kuwaona Wamarekani ni 'watupu'.

Kwa zaidi ya muongo mmoja bendera ya marekani ilikuwa inapeperushwa nje ya jengo kuu-kuu la rangi ya pink katikati ya mji mkuu wa Ghana, Accra.

Mgeni yeyote aliyeingia ndani ya jengo hilo alikutana na picha kubwa ya Rais Barack Obama ikining'inia ukutani. Mapokezi-mezani kulikuwa na kitabu cha wageni chenye seal halali ya idara ya ulinzi ya Marekani. Kila mgeni alikabidhiwa coupon yenye maelekezo, na mwisho kulikuwa na maandishi "Welcome to the US embassy in Ghana".

Image result for Yaw Kwabedo
kijana machachari na mipango ya kibabe

Mwaka 2004 kijana wa umri wa miaka 23 aitwae Yaw Kwabedo anahitimu shahada ya sheria ya chuo kikuu cha Ghana - idara ya sheria. Alihitimu akiwa mmoja wa wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi darasani kwake. 

Kama ilivyo kwa vijana wengi wa Afrika Magharibi, Yaw alikua na ndoto na matamanio ya kwenda na kufanya kazi Marekani kama mshauri wa masuala ya kisheria katika makampuni makubwa.

Aliandaa makabrasha yake yote muhimu, kisha akaanza mchakato wa kupata visa ya Marekani. Aliomba visa mara 4 lakini alinyimwa, alipoteza kiasi kikubwa cha pesa lakini bado aliziishi ndoto zake. Ilimbidi auze baadhi ya mali za nyumbani kwao ikiwemo simu pamoja na runinga, kisha akaomba visa kwa mara ya 5. Lakini bado hakufikia vigezo, akanyimwa tena. Aliumia mno.

Kwabedo aliamini fika kuwa Ubalozi wa Marekani umemdharau na kumdhalilisha. Hivyo, 'piga - uwa - galagaza' atafanya kila awezalo kulipiza kisasi ambacho aliamini lazima angeidhalilisha marekani katika uso wa dunia. Aliapa gharama zake zote alizotumia kuomba visa na kunyimwa zingerudi, pamoja na fidia juu. Aliapa kuwawezesha waghana wote watimize ndoto zao za kuishi Marekani. 

Kisasi kinasukwa kwa ustadi wa hali ya juu sana

Feb 2005, Yaw akiwa anatimiza miaka 24 alimwita rafiki yake wa karibu ambaye alihitimu mafunzo ya uhandisi wa kompyuta, kisha akamshirikisha wazo lake ambalo lililenga kuidhalilisha Ubalozi wa Marekani, Idara ya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya kiintelijensia vya Marekani. Huyu rafiki alisita sana akihofia uwezo na nguvu waliyonayo Maafisa wa ulinzi wa Marekani. Lakini Yaw alifanikiwa kumshawishi, na wakaendelea na mipango.

Yaw alihitaji funding, hivyo aliwaingilia watu wenye uhasama na Marekani na kuwashirikisha mpango wake, aliwaendea Waturuki, akawafafanulia vizuri ramani nzima ya mpango aliousuka. Dili likakubali. Hawa Waturuki pia wakaleta jamaa zao Waholanzi wakaunganisha nguvu na resources. 

Yaw akaingia Ghana akakodi jengo kubwa lilolopo barabarani kabisa. Akajenga mlingoti kisha akaning'iniza bendera ya Marekani. Material aliyotumia inafikirisha sana - ukiwa mbali ni bendera ya Marekani iliyopungua namba ya nyota _ kati ya zile nyota 50, na kadri unavyozidi kuisogelea rangi inafifia hadi mwisho ukiifikia inakuwa bendera ya Ghana.
[​IMG]
Jengo lililopeperushwa bendera ya marekani kwa miaka 10.

Yaw akawaomba waturuki wale watafute 1st grade fingerprint scanner. Yule mhandisi akapewa jukumu ya kutambua software systems zinazotumiwa na Ubalozi wa Marekani. Kisha Wakazinunua kutoka kampuni kubwa ya Marekani ya mitandao. Hivyo waliweza kung'amua processes zote zinazotumiwa na wafanyakazi wa Ubalozini (consular).

Nje ya jengo lile Yaw akafunga satellite 2 za usalama, na pia nje kidogo ya lile jengo akafungua duka dogo la kuuza nguo na viatu.

Wakakodi apartment za hali ya juu na kununua magari kadhaa ya kusafirisha abiria.

vyombo vya ulinzi, usalama na uhamiaji vilivyodhalilishwa

Mwaka 2006 mpango mzima unaanza kutekelezwa rasmi. Yaw na team yake wakaanza kuingia mavyuoni, mitaani, vijiweni, vijijini, mjini pamoja na nje ya balozi halisi ya Marekani na kuzungumza na Waghana waliotoswa visa ya kuingia Marekani.[​IMG] 
Ubaalozi halisi ya Marekani nchini Ghana.

Wote waliokubali mpango wa kina Yaw wakawasafirishwa hadi Accra karibu na ofisi yao, wakawapa hifadhi katika apartment walizokodi pamoja na chakula. 

Kisha kila asubuhi walifatwa kutoka wanapoishi na kupelekwa ofisini, huko michakato ya kutengeneza visa bandia ilifanyika kwa ustadi wa juu sana.

Waliweza kufoji vyeti vyote kwa kiwango cha daraja la kwanza, kuanzia taarifa za kibenki, hati za umiliki wa mali, hati za kuzaliwa, vyeti vya daktari, barua za mialiko, barua feki za kupata kazi na admissions za chuo n.k.

Kwa umakini uliotukuka, visa ya kwanza ilitengenezwa, kisha mteja akalipiwa gharama zote za kuingia Marekani na team ya Yaw. Huyu alitolewa kama chambo kuthibitisha uhalisia wa visa hiyo. Baada ya masaa 26 ya safari, Yaw alikenua meno yote 32, pamoja na timu yake wakapiga mvinyo wa pamoja baada ya yule jamaa waliyemtoa chambo kupokelewa na

kukaribishwa Marekani kwa visa yao waliyoipika jikoni.[​IMG]Sampuli tu ya visa ya Marekani.

Lengo la muda mrefu la Yaw lilionekana kutimia. Mamia kwa maelfu ya Waghana wakawa wanachongewa visa za kuingia US. Huduma yao ikashamiri hadi nchi za jirani kama Cote d'Voire, Togo na Nigeria. Baada ya muda kidogo nchi za mbali kama Kenya, S.A, India, Palestine, Cameroon n.k. nazo zikaanza kupatiwa huduma. 

Wakaanza kujitangaza chinichini kupitia vipeperushi, billboards na magazeti ya udaku. Yaw na timu yake wakaanza kupiga pesa ndefu sana, wateja walimiminika si kawaida. Ilifika kipindi gharama zikapanda hadi kufikia $6000, watu bado walimwagika - walipiga pesa sana. Hakika idara ya Ulinzi (department of Defence) ilidhalilishwa kupita maelezo, tena na kijana wa kawaida kabisa, mbaya zaidi - hawakudhalilishwa kwa masaa kadhaa ama siku kadhaa, bali ndani ya miaka 10 na miezi kadhaa.

Marekani anaamka usingizini - Operation Spartan Vanguard.

Nov 15, 2015 idara ya uhamiaji inashtuka baada ya kugundua kua kuna idadi kubwa sana ya wananchi wa baadhi ya nchi wanapata vibali vya kuingia Marekani, ilhali nchi hizo awali hazikuwa na idadi kubwa ya wananchi wake wanaoingia Marekani.

Upelelezi unaanza... Idara ya ulinzi inatoa tamko la kusitisha kutoa visa kwa baadhi ya nchi kwa muda wa mwezi mmoja. Mshangao mkubwa unaibuka; balozi hazitoi visa, lakini kuna watu bado wanaingia Marekani kwa visa mpya kabisa zinazoonesha wamezitoa ubalozini.

Msako 'wa kufa mtu' unapigwa, wasafiri wote wenye visa mpya kutoka nchi ambazo Marekani ilisitisha kutoa visa zao wanaanza kupelelezwa (interrogated). Pole pole wakaanza kukusanya taarifa, hadi wakafika conclusion kuwa kuna wahuni Ghana ndio wamesababisha fedheha hiyo kwa nchi kubwa yenye ulinzi wa hali ya juu zaidi.

Uvamizi katika ubalozi bandia wa Marekani - Vyombo vya usalama vya Marekani vilitambua fika kua Yaw na timu yake hadi kuweza kufanikisha zoezi la kuidhalilisha Marekani, walijipanga sana. Hivyo, hata wao walibidi 'wajikoki' haswa wasijekudhalilika tena. Zoezi zima la uvamizi halikuwa la 'kispoti spoti'.

Uvamizi huo ulipewa jina la 'Operation Spartan Vanguard'. Kiufupi, operation 'spartans' zote huanzishwa na Marekani kwenye mashambulizi ambayo vikosi vya usalama vimeshindwa kabisa kupata taarifa za awali juu ya eneo wanalopanga kushambulia, hivyo wanajipanga vizuri sana na kwa tahadhari ya juu kwakuwa wameshindwa kumsoma vizuri adui yao. Mara nyingi operatins hizi hazinaga mwisho mzuri. Mfano ni :- Operation Spartan Shield, Operation Spartan Strike, Operation Spartan Fury, Operation Spartan Jordan n.k.[​IMG]Wanajeshi katika 1 ya operation spartan.

Kikosi cha maangamizi kilishiba haswa, hawakufahamu kuwa adui zao ni watu 'walaini'. Kikosi kiliundwa na askari wa Ubalozi wa Marekani, maafisa wa polisi wa Ghana wenye mafunzo ya kijeshi ya Marekani, Taasisi ya upelelezi ya Ghana (Ghana detective bureau), kikosi cha kimataifa maalumu kwa kupamba na uhalifu, askari wa Ubalozi wa Canada, Askari wa uhamiaji wa Marekani pamoja na INTERPOL.

Tena na tena kwa mara nyingine Marekani anadhalilishwa, dunia nzima inamkodolea macho. Kina Yaw wanaisambaratisha Marekani kiulaini kabisa.

Yaw pamoja na timu yake wakiwa ndani ya ofisi yao, tayari walielewa mchezo mzima uliokuwa unaendelea, hawakuwa na papara, hawakuhutaji kujaza risasi kwenye magazine zao. Waliweza kutazama movie nzima wakivamiwa 'mubashara' (live) kupitia satellite mbili walizotegesha nje ya jengo lao.

■ Satellite ya kwanza ilionesha eneo la kuingia ndani ya ofisi yao. Hivyo adui asingeweza kuwafikia bila wao kumshtukia.

■ Satellite ya pili ilionesha usalama la eneo lao la siri la maficho.

Walivyoona wanavamiwa walimuita mmoja wa kijana wa kazi kisha wakampa kichupa, na kumuagiza akifungue kisha akitupe kwenye 'dustbin' ambayo ilikua mlango wa kuingilia. Kichupa hiko kilikuwa ni 'lachrymation spray' - hii ni chemikali kali sana yenye kusababisha muwasho mkali mno sehemu za wazi za mwili (macho, masikio, pua, skin pores, na yale mashimo mengine ya ndani ya c.hupi).[​IMG]askari wa Spartan vanguard wakihenyeshwa.

Baada ya hapo Yaw na team yake wakatoroka kupitia 'built in tunnels' - mifereji ya ndani, ambayo ilipita chini kwa chini na kutokea kwenye lile duka la nguo na viatu nje ya ofisi yao. - Baada ya hapo lazima waingie bar kupongezana  .

Kikosi kazi kile cha Wamarekani kiliambulia muwasho 'wa upupu' na kuwakamata baadhi ya wafanyakazi ambao wala hawakuelewa shughuli haramu ziliyokuwa zikiendelea mule ndani.

Upelelezi bado unaendelea, hadi leo kiongozi mkuu wa shambulizi la Spartan vanguard hajaeleza kupatikana kwa wahalifu wakuu na dau nono tayari limetangazwa kwa atakayefanikiwa kukamatwa kina Yaw.

Katika uvamizi huo vitu kadhaa vilipatikana vikiwemo passport 190 (kutoka nchi 10 tofauti), printer 5 za kisasa, HD camera, mihuri bandia 75, laptop 8, smartphones pamoja na documents zinginge nyingi.[​IMG]baadhi ya vitu vilivyopakipatikana
[​IMG]

Kinachowaliza zaidi taasisi za usalama za Marekani

Wizara ya ulinzi, kitengo cha uhamiaji na maafisa wa usalama wa Marekani wameshindwa kabisa kung'amua mafumbo yafuatayo;-

○Wahuni wa Ghana wenye teknolojia ya kawaida kabisa wamewezaje kukamilisha zoezi 'sensitive' kama hilo kwa zaidi ya muongo mzima?!

○Wameshindwa kung'amua ni visa ya daraja gani ilikuwa inatengenezwa na wahuni hao?!

○Wameshindwa kabisa kung'amua utofauti kati ya visa halali na visa bandia.

○Wameshindwa kung'amua idadi kamili ya watu walipewa visa hizo, wangapi walirudi nchini kwao na wangapi bado wanaishi Marekani.

○Wameshindwa kung'amua jinsi gani wataweza kuwatambua na kuwakamata waliokabidhiwa visa bandia na kuingia Marekani.

○Watawezaje kumzuia Yaw na team yake kuendelea kuchapisha visa hizo bandia. Vipi kama wakiunganisha nguvu na maadui wao wakubwa?!

○Wameshindwa kabisa kupata 'identity' kamili ya Yaw na team yake. (Kwa kifupi jina la Yaw ni la kufikirika tu - uchunguzi unaendelea).

○Je ni kivipi wataweza kujisafisha na fedheha hiyo katika dunia paba ya kiintelijensia - watawezaje kuficha udhaifu wao??

Post a Comment

0 Comments