Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Breaking News | JPM awasilisha taarifa ya mali zake na akaunti ya Benki Sekretarieti ya Maadili



December 28, 2017 President Magufuli amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo  Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
JPM  ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe  December 31, 2017.
Namnukuu alichoagiza JPM, Jaji Nsekela ikifika  December 31, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” – President JPM
Baada ya maneno hayo ya JPM, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi,” –  Jaji Nsekela
Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza President Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.

Credits | MillardAyo.com

Post a Comment

0 Comments