Na:Kennedy Lucas-Manyara.
MKUU wa Wilaya Simanjiro iliyopo Mkoani Manyara Eng:Zephania Chaula anatarajiwa kufunga mashindano ya Maadili Cup Yaliyoaandaliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wilaya ya simanjiro desemba 10.
Mashindano hayo yaliyoanza desemba 7 kwa kushirikisha jumla ya timu 4 kutoka wilayani hapo yanatajia kufikia tamati desemba 10 katika uwanja wa Ccm Mirerani
Mkuu wa Takukuru wilaya ya Simanjiro Mashauri Elisante alisema mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani inayofanyika tarehe 10 desemba kila mwaka huku lengo lake likiwa ni Kuhamasisha na kushirikisha jamii kila mmoja kujitathmini amefanya nini na atafanya nini kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa huku kauli mbiu ikiwa ni "Wajibika Piga vita Rushwa ,Zingatia maadili haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati".
Timu zinazoshiriki katika mashindano hayo ni Naisinyai sports club,Mirerani Sports club,Tanzanite sports club na Veterans Mirerani.
Kwa upande wa zawadi alisema mshindi wa kwanza atapata seti moja ya jezi na Ngao,wa pili mipira miwili na timu zote shiriki pia zitapata mpira mmoja mmoja.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena