Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | MALAYSIA AIRLINES FLIGHT 370: USIRI & 'COVER UPS' (Utapeli, Conspiracy and Secret Societies)

Image result for Freescale Semiconductors. and flight 370
SEHEMU YA NNE


Katika sehemu hii ya nne ambayo natumai itakuwa sehemu ya mwisho ya mfululizo wa makala wa makala hii napenda tuangalie vitu vikubwa viwili muhimu; moja ni mahala gani hasa kwenge uwezekano mkubwa wa Malaysia Airlines 370 ilielekea na pili sababu ya kwa nini kisa hiki kilitokea kwa MH370 na si ndege nyingine.

Tuendelee…



FREESCALE SEMOCONDUCTORS INC.

Freescale Semiconductors ni moja ya kampuni za kwanza kabisa za utengenezaji 'semiconductors' duniani. Ilianza kama kitengo maalumi ndani ya kampuni ya Motorola nchini Marekani mwaka 1948.

Katika miaka ya 1960s serikali ya Marekani kupitia U.S Space Programme waliweka lengo la kupekea binadamu mwezini.
Kisha NASA wakaanzisha programu ya APOLLO ambayo iliajiri mamia ya wanasayansi nguli ili kuifanikisha. Freescale Semiconductors ndio ambao walipewa zabuni ya kuuzia NASA maelfu ya vifaa vya semiconductors kama vile Tracking Equipments za ardhini, Check uot equipments pamoja na 'on-board' Communications Units na Tracking Units.

Freescale Semiconductors pia ndio waliofanikisha kuunda mfumo wa "up-data link" kati ya command module ndani ya roketi ya Apollo na huku duniani.
Pia walifanikisha kuunda transponder ambayo ndiyo ilikuwa ikipokea na kutuma sauti na picha za video pamoja na 'data' kutoka juu mwezini kuja huku duniani.

Baada ya programu hii ya Apollo Freescale Semiconductors waliendelea kupewa mikataba mingi nyeti ya serikali. Na baadae wakafanywa rasmi kuwa 'Defense Contractor' wa Marekani. Defense Contractors kwa tafsiri rahisi ni yale makampuni ambayo yanapewa tenda ya kutekeleza jukumu fulani la masuala ya ulinzi kwa niaba ha serikali (mara nyingi kuunda mitambo, vifaa au mifumo).

Tuseme kwa mfano mwaka huu jeshi la Air Force wanataka kuongeza ndege aina ya F-35 labda tano.
Sasa serikali haina kiwanda cha kuunda ndege hizo japo wana wataalamu wa weledi wa juu wa kubuni mifumo ambayo wanataka iwemo kwenye ndege hizo. Kwa hiyo kinachofanyika serikali ya Marekani wanatoa tenda hii kwa Boeing na kuwapa specifications ni namna gani wanataka ndege hiyo iwe. Kwa hiyo Boeing ambayo ina kitengo maalumu ambacho kinahusika na kupokea tenda za kijeshi wanaunda ndege hizo za F-35 na kisha kuzikabidhi kwa Air Force. Ieleweke kwamba kwa miradi ambayo itahitaji usiri zaidi wa hali ya juu, 'top secret' serikali ya Marekani ina maeneo yake ya siri ya uundaji wa teknolojia hizo. Mfano mzuri ni "Area 51" kwenye jangwa la Nevada limekuwa likitumiwa na Air Force kwa ajili ya kufanya majaribio na kuunda teknolojia na mifumo ya siri ya jeshi.

Lakini nimetoa mfano huo hapo juu (Boeing na kuunda F-35) ili twende sawa na maana ya Defense Contractor. Haya makampuni nitayagusia sana katika makala yangu inayofuata ambayo nitaonyesha ni namna gani walishawishi Marekani kuingia kwenye Vita ya Iraq na ni namna gani walinufaika.

Tuendelee… kwa hiyo Freescale Semiconductors kwa miaka mingi sana tangu miaka hiyo ya 1960s imekuwa ni defense contractor wa Marekani, hasa hasa wakihusika kuunda mifumo kikompyuta inayotumiwa na jeshi.

Jana nilieleza hapa kwenye group kwamba kuna taarifa ambayo naifuatilia na imekuwa inanichelewesha kuandika sehemu hii ya mwisho ya makala. Nimeipekua internet up side down lakini nimeikosa. Nimeingia mpaka 'deep web' kwenye sites za whistleblowers lakini nako nimeambulia patupu. Taarifa nyingi zilizopo ni misleading. Lakini Mungu si Athumani hatimaye nifanikiwa kuipata japonkwa ugumu sana.

Nilikuwa natafuta taarifa za watu hawa wanne; Peidong Wang, Zhijun Chen, Zhihing Cheng na Li Ying.

[​IMG]
Picha Kuyoka US Patent Office inayoonyesha umiliki wa Patent #US 8671381 B1

[​IMG]
Namna ya umiliki wa Patent # US 8671381 B1 ulivyo chini ya Frewscale Semiconductors Inc


Majina haya maane yako kwenye 'manifest' ya abiria ambao walipotea na Flight 370.

Watu hawa pia siku kadhaa nyuma walikuwa wamekutana na maboss wa kampuni ya Freescale Semiconductors nchini Marekani. Nilichokuwa najaribu kuchimba ni kutafuta kama kuna taarifa zozote zinazoonyesha walikutana kwa lengo lipi japokuwa moja kwa moja inaonyesha kwamba kuna 'deal' kuhusu teknojia mpya ilikuwa inaongelewa kwenye kikao hicho. Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa hii inaonyesha dhahiri kwamba teknolojia hiyo lazima itakuwa ni 'top secret'.

Sasa kama siku zote… ili kujua ukweli wa jambo napendelea kuanza kulifukua kutoka kwenye mzizi. Lets see…

Katika tovuti ya Patent Office ya Marekani (hawa ndio wanaotoa hakimiliki ya gunduzi na bunifu mpya). Kuna patent ilitolewa siku nne hivi baada ya ndege ya Malaysia Airlines Flight 370 kupotea. Patent hiyo ina namba US 8671381 B1 na ilitolewa kwa watu watano… Peidong Wang, Zhijun Chen, Zhihing Cheng, Li Ying na kampuni ya Freescale Semiconductors.

Watu hawa walituma ombi la patent mwaka 2012 mwezi septemba tarehe 28 lakini Patent ilitolewa siku nne baada ya Flight 370 kupotea. Tazama picha niliyoweka kutoka Patent Office ya Marekani inaonyesha kwamba wachina hao ndio wagunduzi wa teknolojia hiyo lakini aliyepewa hakimiliki ni kampuni ya Freescale Semiconductors.

Hii maana yake nini… inaonekana dhahiri kwamba wachina hawa wanne baada ya kugundua teknolojia hiyo wakaamua waingie mikataba na makampuni na kuwapa vibali ya kuitumia kwa makubaliano maalumu ya malipo (licencing).
Pia inaonekana kwamba katika mkataba wao huo na kampuni ya Freescale kuna mwanya wa kisheria ambao unawapa Freescale Semiconductors hakimiliki yote ya teknolojia kama ikitokea kwamba wagunduzi hao hawako hai.

Sasa basi…

Katika ndege ile ile ya MH370 pia kulikuwa na wafanyakazi wa ngazi ya juu, 'Top level' staff wa kampuni ya Freescale Semiconductors wapatao ishirini. Hii sio 'rumor' tu bali pia hata Kampuni yenyewe ya Freescale Semiconductors wamethibitisha na kukubali kuwa kulikuwa na staff wao ishirini kwenye ndege.

Inaaminika kwamba watu hawa walikuwa ndio wasimamizi wakuu wa mkataba kati ya Kampuni yao ya Freescale Semiconductors na wale invetors. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuonyesha ni nini hasa walikuwa wanafanya nchini Malaysia lakini kuna dalili kwamba labda walikuwa wanajaribu kushawishi invetors hao wasifanye licencing ya teknolojia hiyo kwa nchi nyingine yeyote zaidi ya Marekani.

Kwa hiyo MH370 ilipopotea ndani yake ilipotea na top level staff 20 wa Freescale Semiconductors ambaye ni defense contractor wa Marekani ambaye anahusika kwenye miradi mingi nyeti ya siri lakini pia ndege hiyo ilikuwa na wagunduzi wanne wa teknolojia mpya na adhimu katika masuala ya ulinzi.

Sasa ishu sio ni nini wagunduzi hawa waligundua bali ni namna gani inaweza kutumika kuunda vitu vyenye uwezo gani kutokana na gunduzi yao hiyo.

Pia inatia mashaka makubwa kuona kwamba mkataba kati ya Freescale Semiconductors na wagunduzi hao ulikuwa na mwanya wa kuipa Freescale hakimiliki kwa asilimia mia moja kama ikitokea wagunduzi wote wakifariki. Inatia mashaka zaidi kuona kwamba wagunduzi hao wote "walifariki" kwa pamoja na siku nne tu baadae Patent ikatolewa kwa Freescale Semiconductors.

Invetors hawa waligundua nini? Au swali zuri zaidi walichogundua kilikuwa na uwezo wa kutumika kufanya nini? Swali hili mimi na wewe inawezekana kamwe tusijue jawabu lake… litabakia siku zote mioyoni mwa jeshi la Marekani lenyewe.

Licha ya kampuni hii ya Freescale Semiconductors kuwa ya Kimarekani lakini uendeshaji wake unafanyika Herzliya Pituah nchini Israel.

[​IMG]
Ofisi ya Freescale Semiconductors iliyopo Herzliya Pituah nchini Israel



Baadae kilifuata kitu cha ajabu sana…


Katika ukimwengu wa espionage, ujambazi, utakatishaji fedha, ufisadi na hata intelijensia… ukitaka kufuta na kuficha trail ya umiliki wa kampuni yako, pamoja na taarifa zake sahihi za kifedha mojawapo ya njia nzuri zaidi ni kutengeneza mlolongo wa shell/shelf companies. Yaani kampuni yako unaiweke kwenye umiliki wa mlolongo wa makampuni kwa kutumia mifumo complex. Yaani mfano Kampuni A inamilikiwa na kampuni B. Lakini asilimi mfano 80 za kampuni B zibamilikiwa na kampuni C. Alafu kampuni C inamerge na kampuni D ambazo zote zinamilikiwa na kampuni E. And on and on… mlolongo unaendelea hivyo hivyo kiasi kwamba mtu anashindwa kujua ni nani hasa mmiliki wa kampuni A.

Sasa basi, mwaka mmoja baada ya tukio hili kampuni ya Freescale Semiconductors ikauzwa kwa kampuni inaitwa NXP. Hii ni kampuni ya kidutch.
NPX kabla ya hapo ilikuwa ni sehemu ya kampuni ya Philips. Ndani yake (ndani ya NXP) ni makampuni mamwili yanayoitwa Signetics na VLSI Teknology. Baadae hii NXP ikauzwa kwa 80.1% kwa kampuni Kohlbervy Kravus Roberts ambaye waliingia ubia wa umiliki na Bain Capital, Silver Lake Patners, Apax Patners na AlpInvest Patners.

Mwaka jana NXP ikauzwa kwa kampuni inaitwa Qualcomm. Hii ni kampuni ya Kimarekani na pia ni defense contractor wa serikali ya Marekani.

Kwa hiyo kwa haraka haraka ni ngumu kusema moja kwa moja Freescale Semiconductors umiliki wake ukoje kwa sasa. Kampuni zinapouzwa na kumilikiwa kwenye mifumo complex kama hii… maana yake vitengo vya kiutendaji vinabadilishwa, vingine vinaunganishwa na vingine vinafutwa. Kwa hiyo ni ngumu kupata trail sahihi ya utendaji uliofanyika miaka michache iliyopita na kujua walio nyuma ya pazia.

Kitu cha msingi sana kikumbuka ni kwamba kampuni hizi zote ni Defense Contractors za serikali ya Marekani kwa hiyo wanajua siri nyingi na wana security clearance ya level ya juu kabisa. Kwa hiyo hauwezi kulala na kuamka asubuhi na kusema unauza kampuni. Ni lazima baraka zitoke kwa mabwana wakubwa na lazima masuala hayo yote yawe ya kimkakati. Kwa hiyo kuna sababu kwa nini Freescale Semiconductors iliuzwa mwaka 2015 mwaka mmoja baada ya MH370 kupotea na kuna sababu kwa nini iliuzwa kwa kampuni ya kidachi. Pia kuna sababu za kimkakati kwa nini mwaka jana kampuni ile ile ya kidachi iliyonunua Freescale Semiconductors ikauzwa kwa Qualcomm kampuni ya kimarekani ambayo ni defense contractor wa serikali ya Marekani.

Naamini mpaka hapa tutakuwa tumepata mwanga kidogo angalau kwamba kwa nini ni Malaysia Airlines Flight 370? Kwa nini tukio lile halikuikimba ndege nyingine bali ni Flight 370.

Swali lililobakia ni kwamba je ndege hii uwezekano unaonyesha iko wapi? Na ilifikaje huko? Na je kuna ushahidi wowote wa kuonyesha ipo huko?

Nitarudi...

Stay here.

Post a Comment

0 Comments