Kanuni ya kwanza ambayo binafsi naishi nayo na kuifuata ili kuweza kujihami na kuwa salama siku zote ni kwamba Kila kitu kiko tofauti na kinavyoonekana (nothing is as it seems).
Tunalala na kuamka. Tunakula na kunywa. Tunaoa na kuolewa. Tunajenga nyumba, tunapata watoto, tunakuwa watu wazima kisha maisha yanaisha. Tunazikwa. Haya ndio maisha ambayo wengi tunayajua na ndio picha ya ulimwengu tuliyonayo vichwani mwetu. Lakini hii haiakisi hata robo ya uhalisia wa ulimwengu 'halisi'. Uhalisia ambayo japo hatuujui lakini unagusa maisha yetu ya kila siku. Uhalisia ambao unaamua kesho ya ulimwengu iweje.
Katika mfululizo huu mpya wa makala, nitajitahidi kuchambua kadiri nitakavyoweza namna ambavyo vikundi vya watu wachache wanavyoamua kesho ya ulimwengu iweje. Namna ambavyo wanaendesha ulimwengu. Na namna ambavyo vitu wanavyofanya vinaathiri maamuzi ya mamilioni ya watu.
Watu hawa wachache sio viongozi wako wa kiserikali unawaona kwenye televisheni kila siku. Sio wafanya biashara maarufu ambao hawakauki kwenye vyombo vya habari. Tabia ya kwanza ya 'watu' hawa ni USIRI na kufanya mambo COVERTLY! Nyuma ya pazia na kuishi kama 'vivuli' lakini wanaathiri na kugusa maisha ya kila mmoja wetu.
Nitachambua masuala kadhaa yaliyoyokea nje ya nchi na ndani ya nchi. Mambo madogo mpaka makubwa. Kuanzia sakata kama EPA mpaka mdororo wa kiuchumi wa Dunia wa mwaka 2007-2009.
Mzee mmoja mwenye busara sana amewahi kuniambia kuwa kisanga cha Richmond ripoti iliyowekwa hadharani haiakisi hata nusu ya kisa chote kamili kilichotokea. Sasa je ikitokea kujua japo robo tatu au hata nusu tu ya kilichotokea. Ndani yake tutaona nini??
Vipi kuhusu mdororo wa kiuchumi wa mwaka 2008 na 2009? Je ni Lehman Brothers pekee wanapaswa kubebeshwa lawama au kuna "kivuli" nyuma ya pazia??
Na je vipi kuhusu visanga kama vya kupotea ndege ya Malaysia Airline Flight 370??? Kuna la zaidi nyuma ya pazia kuliko tuonavyo kwenye televisheni??
Au labda kuna kivuli gani nyuma ya skandali ya mpuliza kipenga kama Edward Snowden na Julian Assange? Kuna la zaidi nyuma ya pazia kuzidi yale tunayoyafahamu? Kuna kitu gani cha zaidi ambacho bado Snowden hajakisema au labda amekisema kwa watu wachache (pengine kwa Warusi) lakini hakijawekwa bayana kwa ulimwengu? Na dhamira iliyomsukuma kusaliti nchi yake, je ni mradi wa 'mass surveillace' wa NSA ambao ulimkera roho yake au labda kuna kitu kikubwa zaidi cha kuogofya ambacho alikiona?
Maswali ni pengi na pengine majawabu ni machache. Mfululizo wa makala hii utajikita kuchambua masuala haya kwa undani zaidi na walau kujipa mwanga japo hata kwa uchache kuhusu kile ambacho kinaendelea 'nyuma ya pazia' katika hii dunia yetu.
Ulimwengu wetu huu tunaoishi umejawa na siri. Siri kubwa zaidi. Siri ambazo nyingine ni labda ni vyema kutozifahamu kabisa.
Nitaanza makala hii "taratibu" ili kujenga momentum nzuri.
MALAYSIA AIRLINES FLIGHT 370: UTATA, USIRI & 'COVER UPS'
Mwaka jana 2016 nakumbuka ilikuwa mwezi June kulizagaa taarifa katika vyombo vyetu vya habari kwamba kumepatikana mabaki ya ndege kwenye pwani ya bahari ya Hindi uko kisiwani Pemba.
Mabaki haya yalikabidhiwa kwa serikali Australia ambayo kwa wakati ule ndio ambao walikuwa wameshikilia hatamu ya zoezi la utafutaji ndege ya Malaysia kwa ukanda huu wa bahari. Picha za kwanza rasmi za mabaki haya ambayo yaliokotwa kisiwani Pemba ziliachiwa na serikali ya Australia tarehe 20 July 2016. Baada ya uchunguzi wa pamoja wa wiki kadhaa, hatimaye tarehe 15 Septemba serikali ya Malaysia ilitoa tamko kwamba kuna "uwezekano mkubwa" kuwa mabaki hayo ni ya ndege ya Malaysia Airlines Flight 370 ambayo ilipotea katikati ya mwaka 2014.
Wiki kadhaa nyuma kuriripotiwa kuokotwa kwa kipande cha 'metal' kwenye pwani ya msumbiji ambacho kilikabidhiwa kwa serikali ya Australia pia. Baada ya uchunguzi wa siku kadhaa taarifa ilitolewa kwamba kuna "uwezekano mkubwa" kuwa kipande hicho cha metali kilikuwa ni sehemu ya "horizontal stabiliser" ya ndege ya Malaysia Airlines Flight 370.
Kuonekana kwa vipande hivi kwenye pwani hii ya Africa Mashariki kuliibua matarajio na matamanio ya kuweka uelekeo mpya wa utafutaji huu wa masali ya Malaysia Flight 370 upande wa magharibi mwa Bahari ya Hindi tofauti na awali ambapo mkazo mkubwa uliwekwa upande wa mashariki mwa bahari ya Hindi.
Baada ya taarifa hizi kuzagaa, moja ya watu ambao taarifa hizi ziliwapa hamasa ni mchunguzi wa kijitegemea Blaine Gibson ambaye ni mwanasheria kitaaluma kutoka Seattle nchini Marekani.
Gibson amewahi kuhusika katika kufanya uchunguzi wa mambo mengi yenye utata zaidi kwenye historia. Mfano miaka ya nyuma amewahi kufanya uchunguzi juu ya kisanga chenye utata cha "Tunguska Meteor" ambacho chanzo chake kilikuwa ni mlipuko mkubwa ambao ulitokea kwenye mto Tunguska huko nchini Siberia mwaka 1908.
Gibson pia amewahi kufanya uchunguzi juu ya namna gani 'Sanduku la Agano' la wana wa Israel lilifika na kupotea huko nchini Ethiopia.
Si hivyo tu, Blaine Gibson amewahi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupotea kwa utatanishi kwa jamii ya watu wa Maya. Jamii ya watu wa Maya ndio jamii ya kwanza kuvumbua na kutumia Kalenda yenye siku 365. Jamii hii katika kilele chake huko miaka ya kale ilikuwa na idadi ya watu mpaka kifikia milioni 13 lakini katika mazingira ya utatanishi mkubwa jamii hii ilifutika yote miaka ya 950 A.D.
Kwa hiyo katika ulimwengu wa visanga na skandali zenye utata, Blaine Gibson ni nguli anayejua anachokifanya.
Kama nilovyoeleza awali, baada ya vipande hivi vya metali kuanza kuokotwa kwenye pwani ya Afrika Mashariki zilivuta hamasa na kumtia mshawasha nguli Blaine Gibson naye kujitosa kutegua kitendawili hiko cha nini hasa kilitokea kwenye upoteaji wa Malaysia Airlines Flight 370.
Gibson kwanza kabisa alisafiri mpaka maeneo ya kusini mwa bahari ya Hindi, mahususi kabisa alikwenda Meldives kukutana na wanakijiji ambao wanadai kwamba waliona Flight 370 ikipita chini chini kabisa kwenye anga la kijiji chao. Kisha akaelekea visiwa vya Reunion kukutana na mtu ambaye anadaiwa kuokota 'Flaperon' inayosadikiwa kutoka kwenye Flight 370. (Nitaeleza kwa mapana kuhusu haya huko mbeleni) Baada ya hapa akaelekea nchini Australia hasa kwenye ukanda maalumu wa utatafutaji. Baadae akafanya kikao maalumu na Naibu Waziri Mkuu wa Ausrtalia Bw. Warren Truss ili kupewa taarifa za ndani kabisa kuhusu mahala ambako juhudi za utafutaji zimefikia.
Baada ya kukusanya taarifa za awali za kutosha kuhusu namna ambavyo ndege ilipotea na juhudi za utafutaji zilikofikia Gibson akaja barani Africa na kuweka makazi yake nchini Afika Kusini.
Mwanasheria na Mchunguzi wa Kujitegemea Blaine Gibson
Maafisa wa serikali ya Tanzania na Australia kwenye picha ya pamoja na mabaki ya ndege inayodhaniwa kuwa ni MH370
Uchunguzi na upekuzi wa Gibson ulianzia magharibi mwa bahari ya Hindi hasa pwani ya Afika Mashariki. Baada ya wiki kadhaa za kazi nzito ya uchunguzi, Gibson alifanikiwa kipata kipande kingine kimoja cha Metali kwenye pwani ya Msumbiji. Baadae uchunguzi wake baharini ukafika mpaka kwenye eneo la bahari la nchi ya Madagascar. Katika Pwani ya Madagascar alifanikiwa kupata vipande vingine vidogo vya metali ambavyo navyo vilionekana kuwa na uwezekano mkubwa kuwa vilitoka kwenye Flight 370.
Kutokana na mafanikio haya ya mfululizo ya Blaine Gibson serikali ya Australia pamoja na Malaysia wakaanza kumtazama kwa 'jicho la tatu' wakifuatilia hatua kwa hatua kuhusu anachokifanya.
Hatimaye katikati ya mwaka huu 2017 serikali ya Malaysia ikamteua moja ya wanadiplomasia wake muhimu zaidi, Bw. Zahid Raza kwenda nchini Madagascar kuangalia hatua za mafanikio ambazo Blaine Gibson alikuwa amefikia kwenye uchunguzi wake.
Zahid Raza aliwasili nchini Madagascar na kukutana na Blaine Gibson. Gibson alimpa muhtasari wa alikofikia kwenye uchunguzi wake, muhtasari ambao ulimshawishi Raza kweli kweli kiasi kwamba safari yake hii ambayo alitarajia iwe ya siku kadhaa tu ndani ya nchi ya Madagascar ikageuka kuwa safari ya wiki kadhaa. Mwanadiplomasia Raza alifurahishwa mno na uchunguzi wa Blaine Gibson.
Lakini Gibson akampa taarifa ya tofauti na kushangaza kidogo. Kwamba amekuwa akipokea jumbe za barua pepe za vitisho juu ya uhai wake kutoka kwa watu wasiojulikana wakitaka asitishe zoezi hilo la uchunguzi. Raza alimpa jibu jepesi tu ambalo wiki kadhaa baadae walikuja kujutia. Raza alimwambia Gibson kwamba apuuzie tu emails hizo kwani watakuwa ni wahuni tu fulani wanajaribu kucheza na akili yake lakini haiwezi kuwa kitu 'serious'.
Japokuwa Gibson bado alikuwa na wasiwasi bado lakini alijitahidi kupuuza barua pepe hizo za vitisho nankuendelea na uchunguzi baharini.
Mwanzoni mwa mwezi August mwaka huu 2017 Blaine Gibson pamoja na Mwanadiplomaisia Zahid Raza walifanikiwa kupata "ushahidi" mwanana zaidi kuhusu Malaysia Airlines Flight 370. Ushahidi unaosemekana kwamba uliwafanya hata wao wenyewe waanze kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao. Gibson alimshauri Raza kwamba wasiseme chochote kwa umma bali hicho walichokipata kiwasilishwe moja kwa moja kwenye serikali ya Malaysia.
Utaratibu ulikuwa kama ifuatavyo…
Kitu chochote kile ambacho Blaine Gibson angekipata kwenye uchunguzi wake anatakiwa kuwasilisha 'ushahidi' huo au kitu hicho kwa serikali ya Madagascar. Kisha serikali ya Madagascar watafanya nao uthibitisho wa awali kama kitu hicho au 'ushahidi' huo unahusiana na Flight 370 na wakiridhika kwamba kuna 'connection' basi watawasiliana na serikali ya Malaysia ambao kupitia muwakilishi wao nchini Madagascar Bw. Zahid Raza watawasafirisha 'ushahidi' au kitu hicho mpaka nchini Malaysia kwa uchunguzi zaidi na kutoa tamko rasmi kwa umma.
Haya ndiyo yalikuwa makubaliano ya ufanyaji kazi kati ya mchunguzi binafsi Blaine Gibson, serikali ya Madagascar na serikali ya Malaysia.
Nimeeleza hapo juu kwamba kuna "ushahidi" ambao Gibson na Raza waliupata. Ushahisi huu ulikuwa ni mabaki ya metali ambayo Gibson aliyapata kwenye maji karibu na pwani ya madagascar pamoja na "fact" fulani ambayo aliigundua. Vitu hivi viwili ndivyo ambavyo vilimpa wasiwasi kwamba haita kuwa busara kila mtu kujua nini walichonacho.
Lakini Zahid Raza alishikilia msimamo kwamba yeye kama mwanadiplomasia ambaye anawakilisha nchi yake hapo ugenini hawezi kwenda kinyume na maagizo ya Rais wake. Kama wakiificha serikali ya Madagascar kuhusu walichokipata kwenye uchunguzi wao inaweza kuleta mgogoro wa kimataifa.
Kwa hiyo ushahidi huu wa metali zilizopatikana ziliwasilishwa kwa serikali ya Madagascar tatehe 12 August mwaka huu 2017. Lakini kuna usiri mkubwa kama zile "fact" walizozigundua kama walizisema kwa serikali ya Madagascar (nitaeleza hii pia huko mbeleni).
Kwa hiyo serikali ya Madagascar walipokea metali hizo kutoka kwa Blaine Gibson siku hiyo ya tarehe 12 August na wakaanza uchunguzi wao wa awali.
Blaine Gibson (katikati) na Zahid Raza (Kulia)... kushoto ni afisa mwingine wa serikali ya Malayisia
Serikali ya Madagascar wakafanya uhakiki wao wa awali na kuthibitisha kuwa kuna uwezekano wa metali hizo kutoka kwenye Flight 370 na wakatoa taarifa hii kwa serikali ya Malaysia.
Serikalinl ya Malaysia ikateua mkandarasi ambaye atasafirisha "ushahidi" huo chini ya uangalizi wa mwanadiplomasia Zahid Raza.
Hatimaye siku ya siku ikawadia na siku hii ilikuwa ni tarehe 24 August mwaka huu 2017 ambapo mwanadiplomasia Zahid Raza alikuwa anatakiwa kufika wizara ya usafirishaji ya Madagascar (Malagasy Ministry of Transport) kwa ajili ya kutia sahihi nyaraka za kiserikali ili kusafirisha vitu vilivyopatikana kwenye uchunguzi wa Bw. Blaine Gibson, lakini kabla hajafika hapo wizarani… akiwa katikati ya mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, mchana wa jua kweupe kabisa… Mwanadiplomasia Zahid Raza alipigwa risasi na watu wasiojulikana na kupoteza maisha papo pao.
Waliyempiga risasi hawajulikani na hakuna yeyote ambaye amekamatwa kuhusiahwa na mauaji haya ya kinyama mchana kweupe.
Lakini nimeeleza kwamba Zahid Raza alikuwa anaelekea kusaini nyaraka za kiserikali kwenye Wizara ya Usafirishaji ya Madagascar ili mkandarasi wa Serikali ya Malaysia aweze kusafirisha "ushahidi" uliopatikana kwenye pwani ya Madagascar kuhusiana na kupotea kwa Malaysia Airlines Fligjt 370 mwaka 2014. Pamoja na hayo kuna ushahidi wa kutosha kwamba kuna "fact" ambayo Zahid Raza na Blaine Gibson waliivumbua na hii ndio iliyoponza uhai wake kukatishwa kinyama siku hii ya August 24.
Kabla sijaenda mbali zaidi, ili kuelewa hasa skandali na kisanga hiki cha aina yake tunapaswa kurudi nyuma kidogo kwenye mwaka ambao Fligjt 370 ilipotea.
MWAKA 2014
Kama ambavyo Tanzania tuna 'forum' kama vile Jamii Forums au Kenya walivyo na 'ushahidi.com' na kadhalika ndivyo China pia nao wana moja ya 'forum' maarufa zaidi inaitwa 'Tianya Club'.
Tianya Club inatoa huduma za BBS (bullutin board system), bloging, microbloging pamoja na 'kushea' picha kwa watumiaji wake.
Lakini pia Tianya Club inafahamika zaidi kwa kuwa chanzo cha kuibhka kwa mijadala mikali ambayo huwa inageuka kuwa miajadala ya kitaifa. Kama umewahi kufuatilia mijadala kama kisanga cha kulishwa sumu Zhu Ling, au kisanga cha "chinese slave scandal", au kisa cha Xiao Yueyue basi mijadala hii mikali ya kitaifa ilianzia huko Tianya Club.
Kwa nini naongelea mtandao huu..?
Tarehe 15 mwezi Desemba mwaka 2014 kuna mtumiaji wa mtandao huu wa Tianya Club ambaye jina lake la asili ya Mandarini linatafsiri ya "Landlord" kwa kiingereza (sio tafsiri sahihi sana kwa mujibu wa watu wanaongea Kimandarini lakini tutumie nina hilo hilo kuepuka kuandika silabi za kimandarini) alipost kitu cha kushitusha sana kwenye mtandao huo.
Aliweka "uzi" kwamba anawaasa Wachina wote wasipande ndege yeyote inayomilikiwa na Malaysia kwa mwezi wote wa Desemba kwa kuwa ana taarifa zenye uhakika kwamba kuna ndege ya Malaysia itadondoshwa mwezi huo. Mwanzoni watu walihisi ni utani tu na wakapuuzia. Lakini kesho yake, yaani tarehe 16 desemba, "landlord" alipost tena ujumbe huo huo kwa mara nyingine na siku ya tarehe 17 desemba kwa mara nyingine tena alirudia post hiyo kuwaasa Wachina wasipande ndege yeyote inayomilikiwa na Malaysia.
Siku kumi na moja baadae, yaani siku ya Tarehe 28 desemba 2014 ndege ya Indonesia AirAsia Flight 8501 (inamilikiwa na kampuni ya Malaysia) ikiwa safarini kutoka Surabaya, Indonesia kwenda Singapore ilipoteza mawasiliano na Air trafic Control na kudondoka kwenye bahari ya Java na kuua abiria wote waliomo kwenye ndege pamoja na marubani na wafanyakazi. Mabaki ya miili ya watu na ndege yalipatikana siku mbili baada ya utafutaji kuanza.
Malaysia Airlines Flight 370
Ndugu wa Abiria
Tukio hili liliwashitua mno watumiaji wa mtandao wa Tianya Club na hata watu kwenye jamii ya intelijensia. Huyu mtu anayejiita "landlord" amewezaje kujua uwezekano wa kutokea tukio kubwa kama hili hata kabla halijatokea.
Ndipo hapa ambapo vyombo vya intelijensia vikaanza kufuatilia post zote za "landlord" kwenye mtandao wa Tianya Club na hasa hasa post zake za siku zilizopita maana baada ya tukio hili tu "landlord" aliacha kupost kitu chochote kingine.
Katika kufuatilia post zake za siku za nyuma ndipo ambapo walikutana na kitu cha ajabu zaidi. Tarehe 4 July mwaka huo huo 2014 "landlord" aliandika "uzi" ambao aliwaasa wachina wasipande ndege za Malaysia kwa kipindi chote cha mwaka huo. Siku kumi na tatu baadae, ndege aina ya Malaysia Airlines Flight 17ikiwa safarini kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur ilidunguliwa nchini Ukraine na majeshi ya Urusi na kuua abiria wote 283 pamoja na marubani na wafanyakazi 15.
Kwa lugha nyingine "landlord" alijua juu ya mpango wa matukio yote haya mawili kabla hayajatokea. Kuna namna mbili tu ya kutafsiri hii, eidha "landlord" alikuwa ni mtu mwenye kujua sana kubahatisha au labda "landlord" alikuwa ni mtu wa jamii ya intelijensia ambaye alipata nyaraka/taarifa za siri sana kuhusu mpango fulani wa siri ambao ulikuwa unaendelea.
Katika post zake "landlord" alikuwa anaandika kwamba kulikuwa na mpango kabambe wa kiintelijensia unaosimamiwa na watu ambao aliwabatiza jina "black hand" au kwenye post nyingine aliwaita "despicable international bully". Japo alitoa tahadhali hii kuhusu "mpango kabambe wa kiintelijensia" lakini landlord hakutaka kuweka bayana ni akina nani anaowasema, mpango huo unalengo gani, au kwa nini ameamua kutoa tahadhali kwa umma (tabia dhahiri kabisa za mtu wa jamii ya intelijensia).
Suala hili mwanzoni liliripotiwa sana kwenye vyombo vya habari vya China na Malaysia lakini baadae lilikuja kuzikwa kiteknikaliti maridhawa na vyombo vya habari vya mataifa ya magharibi na inawezekana ndio sababu kwa nini hujawahi kusikia habari hii kuhusu "landlord" mpaka leo hii (mbeleni huko nitarudi tena kwenye hili).
Nilisema kwamba ili tupate uhondo zaidi wa kisa hiki ni vyema tukianzia mwanzo kabisa kwenye mizizi. Kabla hata ya ya Flight 8501 kupoteza mawasiliano na kudondoka bahari ya Java mwezi Desemba, kabla hata Flight 17 haijadunguliwa na warusi nchini Ukraine na kabla hata ya "landlord" kupost ujumbe wake wa kwanza wa tahadhali. Turudi nyuma kabisa kwenye mizizi. Nyuma kabisa kwenye siku ya safari ya Malaysia Airlines Flight 370 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing.
MIEZI MINNE ILIYOPITA - 8 MARCH 2014
Asubuhi tulivu kabisa yenye hali nzuri kabisa ya hewa na anga lisilo na mawingu. Ni siku nyingine ya kazi kama zilivyo siku zote katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur. Kila abiria alikuwa kwenye mstari wake wa foleni, wafanyakazi wa uwanja wa ndege wakiambaa huku na huko kutimiza majukumu yao na ndege nyingine tayari zikiruka kwenda zinakokwenda na nyingine zikisaranda na kukaa vyema kwenye maeneo husika kusubiri abiria wakwee na kupaa kwenda kwenye safari yao ya siku hiyo.
Moja ya ndege hizi ilikuwa ni ndege ya shirika la Malaysia Airlines ambayo ni Flight 370 yenye namba za usajili 9M-MRO ambayo ni toleo la Boeing 777-2H6ER. Kwa mara ya kwanza ndege iliruka siku ya tarehe 14 May 2002 (majaribio) baada ya kutoka kiwandani na baadae kuuzwa siku ya tarehe 31 May 2002 ikiwa mpya kabisa kwa shirika la ndege la Malaysia Airlines.
Ndege ilikuwa inatumia injini mbili za Rolls Royce Trent 892 na iliundwa kubeba abiria 282. Kabla ya siku ya leo ndege hii tayari ilikuwa imekusanya masaa 53,471.6 ya safari na kufanya jumla ya mizunguko 7,526 ya huduma na haikuwa kupata 'incident' yeyote.
Ukaguzi wa mwisho ndege hii ulifanyika wiki mbili kabla ya siku ya leo, yaani tarehe 23 February 2014 na ulikuwa ukaguzi wa daraja "A Check Maintainace" (Kuna B check, C check na D check).
Ndugu wa abiria wakiwa wameandamana kwenye ubalozi wa Malaysia nchini China kutokana na kuhisi kufichwa kwa taarifa muhimu kuhusu ajali ya MH 370
A chek ndio daraja la kwanza kabisa la ukaguzi ambalo linahusisha zaidi ya zaidi ya masaa 50 mpaka 70. Katika daraja hili ndege inakaguliwa kila ikifikisha masaa 400 mpaka 600 ya usafari au mizunguko 200 mpaka 300 ya safari (ndege ikiruka na kutua mahala kwingine ni mzunguko mmoja).
Pia siku moja kabla ndege hii ilikuwa imefanyiwa "replenishment" ya mfumo wa oksijeni na kila kitu kilikuwa sawa kabisa kwa asilimia mia.
Hatuwezi kuthubutu kusema asilimia mia lakini tunaweza kuthubutu kusema asilmia 99.9% ndege ilikuwa salama kabisa kusafiri hasa ukizingatia hali ya hewa nzuri ya siku hiyo. Kila kitu kilikuwa sawia kabisa namna ambavyo kilikuwa kinatakiwa kuwa.
Ndege ilikaa sawa mahala pake na jumla ya watu 239 wakakwea juu yake (abiria 227 na marubani na wahudumu 12). Watu hawa 239 kwenye ndege walikuwa wana uraia wa zaidi ya mataifa 14; Australua 6, Canada 2, China 153, France 4, India 5, Indonesia 7, Iran 2, Malaysia 50, Netherlands 1, New Zealand 2, Russia 1, Taiwan 1, Ukraine 2 na Marekani 3.
Rubani mkuu Kapteni Zaherie Ahmad Shah mwenye miaka 53 na msaidizi wake First Officer Fariq Abdul mwenye umri wa miaka 27 Hamid waliinua ndege kwenye runway kwenda angani mnano majira ya 11:06 MYT (Malaysia Standard Time) ikiwa inatakiwa kutua kwenye uwa ja wa ndege wa kimataifa wa Beijing nchini China.
Hakuna ambaye alikuwa anajua kuwa safari hii itakuja kugeuka kuwa utata mkubwa zaidi kuwahi kutokea kuhusiana na ndege kudondoka, utata utakaoumiza vichwa jamii ya intelijensia kimataifa kuliko skandali yoyote inayohusisha kudondoka kwa ndege.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena