Chama cha siasa cha Patriota kimesema si kweli kwamba mwanasoka Ronaldinho ‘Gaucho’ ndiye atakaye kiwakilisha katika nafasi ya ubunge.
Patriota kinaongozwa na mwanasiasa mwenye jina kubwa Brazili, Jair Bolsonaro, ambaye wengi wamempachika jina la ‘Trump wa Brazili’.
“Hakuna mazungumzo kati ya chama na Ronaldinho ili yeye awe mwakilishi wetu kwenye kinyang’aniro cha ubunge,” alisema Bolsonaro.
Awali, ziliibuliwa taarifa na mtandao wa O Globo’s zikidai kuwa Ronaldinho aliyewahi kuzichezea Barcelona na PSG, atagombea katika Jimbo la Minas Gerais.
Taarifa hiyo iliambatana na picha iliyomuonesha Ronaldinho mwenye umri wa miaka 37 akiwa na Bolsonaro.
“(Ronaldinho) si mwanachama wa chama chetu, lakini milango iko wazi na litakuwa jambo jema kuwa naye.”
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena