Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Olimpiki Maalumu Arusha yaahidi Kufanya Kweli michuano ya taifa

Image result for paralympic
Picha kwa hisani ya Mitandao

Na:Kennedy Lucas-Arusha.
Michuano ya taifa ya watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 6-11 kisiwani Zanzibar huku timu ya  Olimpiki Maaluum mkoa wa Arusha ikiahidi  kufanya vyema katika michezo hiyo.
Msafara wa watu 48, kati yao   wachezaji 35, waalimu Saba pamoja na viongozi sita ambao tayari wamendoka jijini Arusha tayari kabisa kwa michuano hiyo itakayohusisha michezo mbalimbali huku Arusha wakishiriki katika, Soka ,Riadha na Wavu .
 Katibu wa Olimpiki maaluum mkoa Arusha  (Special Olympics) Mwl Samwel Onesmo alisema wachezaji wako katika ari njema baada ya kuwa kambini kwa muda mrefu katika Chuo cha ualimu Patandi kilichopo Mkoani hapa.
" Michezo hiyo ni kwa wasichana na wavulana  itachezwa na wanafunzi au watu mwenye ulemavu wa akili ambapo ni katika Riadha kuanzia mita 50-5000,mpira wa miguu unashirikisha wachezaji watano kila upande pamoja na mpira wa wavu,"alisema.
Alisema kambi hiyo ya mkoa kutokana na changamoto kadhaa, ilishirikisha Wilaya nne ambazo ni Arusha DC,Arusha Mjini,Meru na Karatu kwa kuhusisha wanafunzi wa Shule za msingi pamoja na vituo vyenye watu mwenye ulemavu viliruhusiwa kushiriki.
"Tunashukuru wadau mbalimbali walijiyokeza kufanikiaka kambi na safari nzima ya timu hii na tunawaahisi Wakazi wote Mkoani hapa watarajie ushindi kulingana na maaandalizi mazuri yaliyofanyika,Aliongeza.
Naye Afisa Elimu mkoa Arusha,Mwalimu Gift Kyando aliwapongeza wote walishiriki katika zoezi la kufundisha timu hiyo ambayo umeenda kuwakilisha mkoa kitaifa kuwa ni jambo njema na kusema Serikali inatambua juhudi hizo licha ya kuwa bado haijafikia kiwango .
" Maandalizi ya michezo ya mwaka huu iwe ni maandalizi ya michezo inayofuata na tunwasihi wadau wengine wajitoe kwani hawa pia ni watoto kama wengine hivyo jukumu la kushirikiana ni la wote katika kuwapa nafasi watu mwenye ulemavu nao kushiriki michezo kikamilifu,"alisema.
Aliwasihi viongozi kuwa hao ni wanamichezo na wana kwenda katika mazingira mapya wazingatie malezi hao na waende kwa ajili  ya kushindana na si mambo mengine na katika michezo kuna kushinda kufungwa na kutoka suluhu.
Ofisa Michezo mkoa Arusha Mwanvita Okeng'o aliwashukuru wafadhili waliojitoa kufanikisha safari nzima ya vijana hao kwenda kushiriki kwani michezo ni ajira na watu wote ni sawa.
Mmoja wa wachezaji hao Fatma Khatib nayesoma shule ya msingi Kaloleni ambaye atakimbia Riadha mita 50 hadi 100 alisema mkoa wa Arusha watarajie ushindi na kurudi na medali za kutosha.

Post a Comment

0 Comments