Kocha wa timu ya taifa ya Algeria, Rabah Madjer ametangaza kikosi cha wachezaji 24 akiwamo kiungo wa Riyad Mahrez wa Leicester City tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania utakaochezwa Machi 22 kwenye Uwanja wa July5.
Mbali ya kuita nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya pia kocha huyo amewaita wachezaji 11 wanaocheza soka ndani kwa ajili ya michezo hiyo miwili kimataifa mbali ya Tanzania pia watacheza na Iran Machi 27.
Wachezaji ndani wengi wao itakuwa ni mara yao ya kwanza kuichezea timu hiyo ambao ni Mohamed Naamani (Belouizdad CR), Abdennour Belkheir (CS Constantine), Farid El-Mellali (Paradou AC), Salim Boukhanchouche (JS Kabylie), Mohamed Amine Abid (CS Constantine).
Kwa mujibu wa gazeti la lexpressiondz nchini Algeria, limedai kuwa Kocha huyo anataka wachezaji hao wa ndani waongeze ushindani kwa wanaotoka nje kwa lengo la kuwa na timu bora zaidi, imeelezwa.
Pia, kocha Madjer amewaita nyota wawili waliorejea hivi karibuni kutoka katika majeruhi Nabil Bentaleb (Schalke 04) na Saphir Taider (Montreal Impact), lakini atamkosa majeruhi Fawzi Ghoulam.
Kikosi cha Algeria kitaingia kambini Machi 19 katika National Technical Center of Sidi Moussa (Algiers). Mechi hizo mbili ni kwa ajili ya kujiandaa na kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2019 nchini Cameroon.
Kikosi:
Makipa: Faouzi Chaouchi (MC Alger), Abdelkadir Salhi (CR Belouizdad), Taoufik Moussaoui (AC Paradou)
Mabeki: Aïssa Mandi (Real Betis / ESP), Carl Medjani (Sivasspor / TUR), Ramy Bensebaïni (Rennes / FRA), Farouk Chafai (USM Alger), Mokhtar Benmoussa (USM Alger), Essaid Belkalem (JS Kabylie), Mohamed Naamani (CR Belouizdad)
Viungo: Yacine Brahimi (FC Porto / POR), Riyad Mahrez (Leicester City / ENG), Nabil Bentaleb (Schalke 04 / ALL), Ismael Bennacer (Empoli / ITA), Zinedine Ferhat (Le Havre / FRA), Sapphire Taider (Impact of Montreal / MLS), Abdennour Belkheir (CS Constantine), Salim Boukhanchouche (JS Kabylie).
Washambuliaji: Baghdad Bounedjah (Al-Sadd / QAT), Hilal Soudani (Dinamo Zagreb / ??CRO), Sofiane Hanni (Spartak Moscow / RUS), Mohamed Amine Abid (CS Constantine), Farid El-Mellali (Paradou AC), Islam Slimani ( Newcastle / ENG).
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena