Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika eneo la Jangwani jijini Dar es salaam, baada ya Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi hapa nchini, hali iliyofanya Mto Msimbazi kufurika maji na kupelekea sehemu ya eneo hilo katika barabara ya Morogoro kufungwa kwa muda. hali hiyo pia ilisababisha kituo cha mabasi yaeneondayo haraka (UDA RT) kufungwa na mabasi yote kusitisha safari zake za kuelekea maeneo ya katikati ya mji. Kwa mujimu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini, hali hii ya mvua inatazamiwa kuendelea hadi hapo Aprili 19, 2018, hivyo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhali ya mvua hiyo ambayo inaweza kuleta madhara.
Maji yakiwa yameenea kisa sehemu ya eneo la Jangwani.
Mmoja wa wakazi wa maeneo ya jirani na Jangwani akisaka chochote kwenye maji hayo, bila kujali usalama wake.
Nyumba zilizo kando ya eneo la Jangwani zikionekana kujaa maji.
Eneo la Jangwani linavyoonekana kutokea upande wa Mapipa, Magomeni.
Maji ni mengi sana.
Mdau akitafakari jambo katikati ya maji hayo.
Sehemu ya wakazi wa Maeneo ya Magoneni wakishuhudia Maji yalivyofurika katika eneo la Jangwani.
Wengine wakitafakari namna ya kwenda kwenye mishughuliko yao.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena