Header Ads Widget

Responsive Advertisement

News | Polisi Wamekamata Mbegu za Bangi Mkoani Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani, linamsaka dereva aliyefahamika kwa jina la Moshi Ramadhan Malinganya mkazi wa Kisarawe kwa tuhuma za kusafirisha bangi puli 193,katika gari alilokuwa akiliendesha . 

Pamoja na hilo ,kwenye buti ya gari hilo kumekutwa na ndoo ndogo mbili za lita kumi zenye bangi na kiroba kidogo chenye mbegu za bangi kilo mbili. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kisarawe, kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ambae anasubiri makabidhiano kuhamia Mwanza kikazi,alisema mtuhumiwa ametoroka baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka wakati akiwakimbia polisi. 

Alieleza , tukio hilo lilitokea agosti 21 majira ya usiku eneo la shule ya sekondari Minaki akiwa anaendesha gari namba T 801 AAF aina ya Toyota Mark II.
kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna akionesha namba za Gari kwa Wanahabari (hawapo pichani) 
.com/proxy/
“Tulipata taarifa toka kwa wasamaria wema juu ya gari hilo kusafirisha bangi kutoka kijiji cha Gwata kwenda Mombasa Jijini Dar es Salaam tuliweka mtego eneo la mnara wa TBC lakini tulipomsimamisha hakusimama”, alisema Shanna.Shanna alisema ,polisi walimkimbiza lakini walikuta gari hilo limepinduka huku dereva huyo akiwa amelitelekeza .” Vitu vingine vilivyokutwa katika gari hilo ni namba za magari mbili ikiwemo namba T 321 AJH na TZH 7255 jambo linaloashiria kuwa mtuhumiwa alikuwa akibadilisha namba hizo wakati wa matukio ya biashara haramu ya dawa za kulevya,”alisema Shanna.
.com/proxy/
Hata hivyo, alielezea wanamshikilia mmiliki wa gari hiyo (Majaliwa Salehe) kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusu gari lake kukutwa na madawa hayo.Kwa mujibu wa kamanda huyo ,wataiomba mahakama kutaifisha gari hilo kwa mujibu wa sheria ili kuwakomesha watu wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya

Post a Comment

0 Comments