Kuna uwezekano Linex Sunday Mjeda akawa ni msanii ambaye kwa
kile alichokisema akawa anawakilisha mawazo ya wasanii wengi, kutokana na hatua
kubwa anazoendelea kuzipiga msanii mwenzao Nasib Abdul aka Diamond.
Ukiachana na mengi ambayo tayari ameyafanya kama msanii na kama
Mtanzania anayepeperusha bendera ya nchi yake huko duniani, Platnumz amekuwa
chachu ya maendeleo kwa wasanii wenzake ambao kwa namna moja au nyingine
wanatamani kufikia mafanikio yake.
Linex ameguswa na hatua aliyofikia Platnumz ambaye bado yuko
Marekani alikoenda kuhudhuria tuzo za BET, na kuamua kueleza kile kilicho
moyoni. Amepost picha ya Platnumz akiwa na msanii wa Marekani Nelly, na
kuandika ujumbe huu.
“Kutoka moyoni this step ya uyu mwana ina ninyima usingizi but
haininyimi kwa ubaya inaninyima kwa uzuri na inanipa msukumo wa kupiga kazi na
kuamin Mungu aliweka kitu ndani yangu kwa maksud big S/o @diamondplatnumz
nachoamn mm ni umefungua njia za mziki wa tanzania#wemakwaubaya #Wethevoa.”
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena