Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MWANAMZIKI BINTI WA KISUKUMA JULIANA PATRICK KUTOKA MAGU MKOANI MWANZA AWATOA JASHO WAMAREKANI.


Hakika Kipaji hakichajui wala hakibagui, kokote kule chaweza kutua na kuucha Umma wa Watu wengi ukiwa na Maswali mengi ya kujiuliza pasi na kupata majibu.

Hii ni Habari njema kwa Watanzania hususani Wasukuma kutoka Isolo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza baada ya Mtoto wao, Binti yao, Mjukuu wao na hata mdogo wao Juliana Patrick
nyota yake ya Muziki kung'ara vyema na hatimae kuipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania katika Ardhi ya Marekani.

Akiwa na Umri wa Miaka 15 tu binti huyu amejinyakulia mafanikio katika tasnia ya Muziki baada ya kuachia kibao chake cha kwanza kinachokwenda kwa jina la "Dear Diary" kibao ambacho alikiachia Desemba 16 Mwaka jana na hadi kufikia mwisho mwa mwaka huo kibao hicho kilikuwa kimekimbiza mbaya na kushika nafasi ya Tatu katika mamia ya nyimbo huko nchini Marekani katika Mji wa Houston Texas.
Bonyeza hapa kuusikiliza wimbo wake >>>>>"Dear Diary"

Post a Comment

0 Comments