Waziri
wa Ujenzi Dr Joh Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema John
Mnyika,Mbunge wa Jimbo la Kawe -Chadema Halima Mdee,Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Meck Sadic Wakizindua ujenzi wa barabara wa barabara ya
External –Kilungule
Waziri wa Ujenzi Dr Joh Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema
John Mnyika,Mbunge wa Jimbo la Kawe -Chadema Halima Mdee,Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Meck Sadic Wakizindua ujenzi wa barabara ya Msewe-Baruti
Waziri wa Ujenzi Dr Joh Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema
John Mnyika,Mbunge wa Jimbo la Kawe -Chadema Halima Mdee,Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Meck Sadic Wakizindua ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangi Bovu
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, Waziri wa Ujenzi, Dkt John
Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee mara baada ya kuzindua
mitambo itakayofanya kazi katika ujenzi wa barabara ya Mbezi
mwisho-Goba-Tangi bovu
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, Waziri wa Ujenzi, Dkt John
Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Kawe, wakisalimiana na wananchi baada ya kuzindua
mitambo itakayofanya kazi katika ujenzi wa barabara
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Dkt. Pombe Magufuli
Muonekano wa sasa katika hatua za awali za ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangibovu eneo la Goba
---
Babaraba zilizowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ile ya
Kinyerezi-Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0,
Kigogo-Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6 na Kimara Baruti-Msewe
hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6
Barabara nyingine ni ile ya External-Kilungure hadi Kimara Korogwe
kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi Mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi
bovu kilometa 9.0
Waziri Magufuli alisema, barabara ya Wazo Hill-Goba yenye urefu wa
kilometa 20 ikikamilika kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za
Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa zikikabiliwa na msongamano kwa
muda mrefu.
Pia, barabara ya Kinyerezi-Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa
kilometa 14 itapunguza msongamano kwa kiasi kikubwa kwa kuwa itakuwa
inaunganisha barabara ya Morogoro na Nyerere.
Kwa umuhimu sana, Waziri Magufuli alisisitiza; "kumbukeni mkiiba vifaa
vya ujenzi hamuibi vifaa vya kampuni zinazojenga bali mnajiibia wenyewe
kwa sababu hizi ni fedha za kodi ya wananchi bali kwa kufanya kazi kwa
bidii na uadilifu kutawezesha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati
na ninyi (mafundi) kujihakikishia uhakika wa ajira"
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng.Patrick
Mfugale ameiomba serikali kuongeza bajeti ya barabara ili kuwezesha
miradi ya barabara kukamilika kwa wakati na kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa wakandarasi ili barabara zijengwe kwa kiwango
kilichokubalika katika mikataba.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena