Mrundi huyo, alijiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo lililofungwa Desemba 15, mwaka jana akitokea Simba baada ya mkataba wake wa miezi sita kusitishwa.
Safu ya ulinzi ya Simba inaundwa na mabeki wa kati Mganda, Juko Mrushid, Hassani Isihaka na mabeki wa pembeni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Hassani Kessy, Nassoro Said ‘Chollo’, Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’ na William Lucian ‘Gallas’.
Tambwe amesema kuwa Simba hawana beki wa kuizuia safu yao ya ushambuliaji.
“Nikwambie tu ukweli, kwa beki ile ya Simba ninayoijua mimi, kazi watakuwa nayo mara tutakapokutana nao kwa kuanzia huku kwenye Kombe la Mapinduzi na ligi kuu.
“Kwa sababu nikiiangalia ile safu ya ulinzi na hii safu yetu ya ushambuliaji inayochezwa na Sherman (Kpah), Msuva (Simon), Mrwanda (Danny) na mimi mwenyewe ni ngumu kushindwa kuwafunga Simba.
“Kiukweli kabisa sisi mbele tupo vizuri sana kuanzia namba sita kuja juu, hapa ninapokwambia wachezaji wote tuna hamu ya kukutana na hao Simba wakati wowote ule,”alisema Tambwe.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena