SIKU chache baada ya kuibuka utata mkubwa juu ya kichanga cha kike cha
mwimba Injili maarufu Bongo, Flora Mbasha huku mitandao ya kijamii
ikieleza kwamba baba wa mtoto huyo si aliyekuwa mume wa mwanamuziki
huyo, Emmanuel Mbasha ‘Ima’, familia ya mwanaume huyo inadaiwa kufanya
kikao kizito jijini Dar ili kupata ufumbuzi, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Mbasha, familia
hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita nyumbani kwa Ima, Tabata-Kimanga, Dar
ili kulizungumza suala hilo na kuona kama wanaweza kukubaliana kukilea
kichanga hicho endapo ni damu yao.
“Ndugu walitofautiana, kila mtu alikuwa na mtazamo wake hivyo wakaona
bora wakutane na kutafuta jibu la pamoja kama wanalea au hawalei,”
kilisema chanzo hicho.
KIKAO CHAVUNJIKA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kikao hicho hakikufikia
muafaka kutokana ndugu hao kutofautiana kimisimamo kwani kila mmoja
alitoa mawazo yake.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha ambaye sasa anatamba na Wimbo wa Haribu Mipango ya
Shetani ambao inadaiwa amekuwa akiutumia kama kijembe kwa Flora, alisema
aachwe kwanza kwani suala hilo linamuumiza kichwa na ni la kifamilia
zaidi.
“Naomba mniache kwanza, sipo vizuri kwa sasa,” alisema
CLIP YAONESHA MSIMAMO
Kwa mujibu wa ‘clip’ ya sauti yake (Mbasha) aliyoituma kwa Ijumaa
Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye ana mtoto mmoja tu, Elizabeth
Emanuel Mbasha ’Liz’ ambaye ana miaka kama kumi na moja.
Mbasha alisema hajui nini kinaendelea na kwamba ameambiwa habari za
Flora kujifungua mtoto wa kike lakini yeye haoni kama habari hizo
zinamhusu sana!
MSIKIE
“Mimi sijui niseme nini? Nimeambiwa kwamba Flora amejifungua. Kwa hiyo?
Mbona yeye Flora hajaniambia, si anajua taarifa hizo hazinihusu?
Amuogope Mungu, yeye angewaambia watu ukweli.”
Ijumaa Wikienda: “Kwa hiyo unataka kusema mtoto si wako?”
Mbasha: “Yeye anajua.”
NDUGU WA MBASHA
Ijumaa Wikienda lilizungumza na ndugu mmoja wa Mbasha (jina lipo) ambaye
alizungumzia sakata la shemejiye kujifungua mtoto akiwa mbali na
nyumbani:
“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mara baada ya ugomvi wao na kuondoka nyumbani miezi saba iliyopita,
Flora aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akikiri kuwa na
ujauzito na kusema: “Ndiyo nina mimba lakini siyo ya Gwajima.”
AZUNGUMZIA UNDUGU WAKE NA GWAJIMA
Hata hivyo, hivi karibuni, Flora alikazia tena maneno yake kwa kusema
kuwa Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ni anko
(mjomba) wake kwa hiyo watu wajaribu kuliangalia hilo, hawezi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mjomba‘ake.
KUHUSU MADAI KUWA MTOTO NI WA GWAJIMA
Mwanasheria: “Kwanza nataka kusema kwamba, chombo chochote cha habari
ambacho kiliandika habari ya kumchafua Flora tutakishitaki. Iwe ni
magazeti iwe ni mitandao ya kijamii. Wanaosema ni mtoto wa Gwajima ndiyo
wanaomchafua Flora kwa sababu si kweli.”
GPL
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena