Unapoingia katika penzi jipya, ni kipindi ambacho moyo wako unakuwa na furaha ya hali ya juu. Unaweza kuhisi unaibeba dunia nzima kwa raha ya penzi jipya, utajitahidi kumuonesha huyo uliyempata kila aina ya mahaba ilimradi aendelee kuwa na wewe na akupende zaidi.
Lakini kadiri unavyozidi kukaa na mwenzako na mnavyozidi kuzoeana, ndipo unapopata nafasi ya kuyajua maisha yake kwa undani.
Taratibu utaanza kufahamu yeye ni mtu wa aina gani, kabla yako alikuwa na nani (ex wake), anatokea kwenye familia ya namna gani au anaishi katika mazingira gani.
Hapo ndipo matatizo yanapoanzia. Yawezekana kuna mambo mengi alikuficha wakati mnakutana lakini sasa unaanza kuyabaini wewe mwenyewe. Hiki ni kipindi kigumu ambacho wengi hushindwa kukivuka na matokeo yake, kukaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa wiki kadhaa au miezi kadhaa ndiyo inaonekana fasheni.
Utafiti mwepesi unaonesha kuwa wanawake au wanaume wengi wanaingia kwenye uhusiano mpya baada ya ule wa awali kuvunjika au kulegalega. Ni wachache sana wanaoingia katika uhusiano ambao mwenzi wako hajawahi kuwa na mpenzi au amekaa kipindi kirefu bila kutoka na mtu yeyote.
Kwa mantiki hiyo, unapoingia katika penzi jipya, unatambua kwamba wewe siyo wa kwanza. Kuna wenzako walishatangulia kabla yako ambao mwenzi wako ndiye anayewajua kwa majina na sura.
Pia utafiti mwingine unaonesha kwamba hakuna jambo gumu kama kutengana katika uhusiano wa kimapenzi.
Pia utafiti mwingine unaonesha kwamba hakuna jambo gumu kama kutengana katika uhusiano wa kimapenzi.
Kwamba hata kama mwenzako ameshakwambia hakutaki, itakuchukua muda mrefu sana kuamini kwamba kweli anamaanisha kile alichokisema.
Katika kipindi cha mwishomwisho wakati uhusiano wa kimepenzi ukielekea mwisho, lazima yule anayeachwa atakuwa anaendelea kubembeleza apewe nafasi nyingine au asamehewe kama kuna jambo alikosea.
Kwa bahati mbaya, wengi wetu huwa hatujipi muda wa kutosha unapotoka kwenye penzi la awali kuingia kwenye penzi jipya. Matokeo yake, wengi wanajikuta wameanzisha uhusiano na mtu mwingine katika muda ambao mpenzi wa awali bado hajaliafiki suala la kutengana.
Bado anabembeleza na kuamini anaweza kupata nafasi nyingine ya kurekebisha pale alipokosea ili maisha ya kimapenzi yaendelee.
Kinachotokea sasa, unakuta umekaa na mpenzi wako mpya lakini bado yule wa zamani anakupigia simu au anakufuatilia mitaani akitaka kupata muda wa kuzungumza na wewe ili myamalize na kuendelea na uhusiano.
Ni hapo ndipo unapopata nafasi ya kujua kuwa kumbe mpenzi wako alikuwa anatoka na mtu mwingine na bado anampenda ndiyo maana anampigia simu ukiwa naye, anamfuata kila anakokwenda na wakati mwingine anakuja hata ukiwa na mpenzi wako mpya.
NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HALI HIYO?
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kufurahia kugundua mpenzi wake bado ana mawasiliano na mtu wake wa zamani. Ni katika kipindi hiki, wengine uzalendo unawashinda na kuamua kukubali kukaa pembeni kuepusha msongamano.
NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HALI HIYO?
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kufurahia kugundua mpenzi wake bado ana mawasiliano na mtu wake wa zamani. Ni katika kipindi hiki, wengine uzalendo unawashinda na kuamua kukubali kukaa pembeni kuepusha msongamano.
Hata hivyo, hutakiwi kuwa mwoga, kupandwa na jazba, kupigana, kutukanana au kuvunjiana heshima na x wa mpenzi wako.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena