Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | MALAYSIA AIRLINES FLIGHT 370: USIRI & 'COVER UPS' (Utapeli, Conspiracy and Secret Societies) FINAL

Image result for FLIGHT 370 cover ups
UTATA, USIRI & COVERUP: MALAYSIA FLIGHT 370



Kwa wale ambao hawakuwepo naomba nikimbushie kitu kimoja ambacho niliandika siku si nyingi zilizopita hapa hapa kwenye group.

Kwamba…

Kama ukisimama kwenye pwani ya Bagamoyo na kisha kusafiri baharini umbali wa maili elfu mbili kuelekea mashariki, utakutana na kijikisiwa kidogo sana chenye umbo ya kama mduara hivu kinaitwa Diego Garcia.
Kisiwa hiki kinamilikiwa na nchi ya Uingereza lakini kwenye miaka ya 1970 Uingereza ilihamisha wakazi wote wa kisiwa hiki na kuwapeleka Mauritius na Shelisheli ili kupisha ujenzi wa kituo cha kijeshi cha jeshi la Marekani kisiwani hapo, kituo ambacho kwa sasa kinajulikana kama Camp Thunder Cove ambacho kinahifadhi wanajeshi karibia 4000 na wakandarasi binafsi wa nchi ya Marekani wa masuala ya usalama.

Japokuwa Uingereza imekuwa ikikanusha vikali juu ya uwepo wa "black site" kwenye kisiwa hiki lakini upo ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba CIA wana black site katika kisiwa hiki.

Kwa mfano, ripoti ya Kamati ya seneti ya mambo ya Intelijensia mwaka 2014 japokuwa ilikuwa 'reducted' vitu vingi ili kulinda usiri wa shughuli za intelijensia lakini ilikiri CIA kuwa na "black site" katika bahari ya Hindi.
Si hivyo tu, Lawrence Wilkerson ambaye alikuwa ni katibu kiongozi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani kwenye utawala wa Bush awamu ya kwanza, Colin Powell… ameeleza kwamba baada ya tukio la 9/11 washukiwa wengi wa Ugaidi walikuwa wanashikiliwa kwenye jela ya CIA iliyoko bahari ya Hindi kabla ya kupelekwa mahala kwingine.

Sasa basi…

Kuna kila dalili kwamba ndege hii ilitua kwenye kisiwa hiki cha Diego Garcia.
Kuna sababu kuu tatu kwa nini kuna dalili hizi kwamba ndege hii ilitua Diego Garcia.

i) Ni uelekeo wa ndege mara ya mwisho kuonekana kwenye rada ya jeshi la Malaysia ambapo ilikata kona kuelekea magharibi na kisha kukunja kona nyingine kwenda kusini. Muelekeo huu ni wa eneo la bahari ya Hindi lenye visiwa vya Maldives na Diego Garcia.

ii) Wakazi wa Visiwa vya Maldives eneo la Kuda Huvadhoo wanasema kwa siku ya March 8, 2014 majira ya saa 06:15 ilipita ndege kubwa mno ikiruka usawa wa chini chini sana. Wanasema kuwa tukio hili lilikuwa la tofauti kwao kwani hawajawahi kuona ndege kubwa kiasi hicho kutokana na kuzoea 'jet' ndogo ndogo tu zinazotua kisiwani hapo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa dege kubwa kiasi hicho kupita kisiwani hapo tena chini chini sana kuashiria kwamba ilikuwa inataka kutua. Wakazi hawa wanadai kwamba ndege ilipita chini chini kiasi kwamba ukiangalia kwa makini ulikuwa unaweza mpaka kuona eneo la mlango ambao abiria utokea (japo ulikuwa umefungwa).

Wakazi hawa wa Maldives walipoambiwa waelezee muonekano wa ndege hiyo walisema kuwa ilikuwa nyeupe na mistari myekundu ubavuni (muonekano ule ule wa ndege ya Malaysia Airlines Flight 370).

Habari hii iliandikwa sana kwenye gazeti la kisiwa hicho linaloitwa Haveruu kwa mwezi mzima wa March.

Mohamed Zaheem ambaye ni Councilor wa eneo la Kuda Huvadhoo naye amethibitisha taarifa hii ya wananchi wake kwamba ni kweli ndege iliyoelezewa na wananchi wake ilipita juu ya anga la kisiwa chao na ilikuwa gumzo kutokana na ukubwa wake, kuruka chini chini na kelele ambazo ilikuwa inapiga.

iii) Data za staellite ambazo MH370 ilikuwa inafanya handshakes tukikokotoa tunapata coordinates ambazo zinaonyesha dhahiri kwamba muelekea wa ndege hii ulikuwa ni kwenda eneo hili la visiwa vya bahari ya Hindi.

[​IMG]
[​IMG]
[​IMG]
Mahala vilipo visiwa vya Diego Garcia na Maldives


Swali; hao ambao "waliiteka" ndege hii walifanikishaje tukio hili?

Ndege zote za Boeing toka mwaka 2012 zimewekewa mfumo maalumu wa Teknolojia unaoitwa "Uninterruptible Autopilot". Chini ya mfumo huu Boeing wenyewe kutoka ofisini kwao kupitia mifumo yao ya ulinzi ya kompyuta wanaweza kuiweka ndege chini ya 'uninterruptible Autopilot' na kuiendesha wao bila rubani kuwa na uwezo wa kufanya chochote kile. Walifikia uamuzi huu baada ya kuanza kutokea kwa matukio ya marubani kudondosha ndege makusudi wakitaka kujiua. Kwa hiyo ili kuokoa maisha ya abiria wengine Boeing walifunga mfumo huu ili wakiona kwamba ndege inaanza kwenda tofauti na vile inavyotakiwa basi wanaitoa kwenye udhibiti wa rubani na kuanza kuiendesha wao remotely.

Lakini pia CIA mwaka 2009 walizindua mfumo unaofanana na huu kwamba wanaweza kuitoa ndege kutoka kwenye udhibiti wa rubani na kuiendesha wao remotely ikitokea ndege hiyo wakiona inaendeshwa kwa mashaka ili kuepusha lisitokee tukio lingine la kufanana na lile la September 11.
Japokuwa mfumo huu walitangaza kwamba wanautumia kwa ndege zile ambazo zinakuwa kwenye anga la Marekani lakini kuna ushahidi kwamba CIA wana access na mifumo hii katika mashirika yote ya ndege ikiwemo Boeing. (Flight 370 ilikuwa mi Boeing 777).

Hii inaelezea kwa nini transponder ilizimika kwenye ndege na kupoteza mawasiliano na ACC zote, pia inaeleza kwa nini ELTs (Emergency Locator Transmitters) zote nne hazikufanya kazi kwa pamoja ni kwa sababu kuna watu ambao walikuwa wanaiendesha watakavyo ndege hii kutoka ardhini na marubani na wote waliomo kwenye ndege wasingeweza kufanya chochote kile.

Lakini pia hii inaeleza ni kwa nini ndege hii haikuonekana na rada zote kwenye nchi zilizopita, kwa rubani wa kawaida hana uwezo wa kuendesha ndege kukwepa rada. Lakini rubani mwenye weledi wa ndege za kivita ana uwezo wa kukwepa asionekane na Rada. Kikundi pekee cha watu wenye uwezo wa weledi huu ni CIA.

Lakini nisiandike sana mimi… nitoe ushahidi wangu wa mwisho kabisa kuhitimisha makala hii.

Wote tunamfahamu Dr. Mahathir Mohammed. Huyu ndiye "baba wa Taifa" la Malaysia. Ndiye mtu mwenye ushawishi zaidi nchini Malaysia. Ndiye aliyeijenga hii Malaysia ya sasa inayopigiwa mfano kila kona ya dunia. Huyu ni mtu ambaye ana ufahamu wa ndani kabisa kuhusu namna dunia inavyoendeshwa nyuma ya pazia.

Serikali ya Malaysia ilipotenga bajeti kwa ajili ya kuendesha zoezi la kuitafuta MH370 baharini alijitokeza na kupinga vikali akisema kuwa ni kupoteza fedha bure... alipoulizwa kwa nini alitoa maelezo yafuatayo.

Namnukuu;

"…lidege likubwa kama lile halipotei hivi hivi tu…kuna watu wanaficha taarifa fulani.! Kuna baadhi ya idara za serikali fulani duniani wana uwezo wa kuidhibiti ndege kutoka kwa rubani na kuiendesha 'remotely'. Si haki kwa nchi ya Malaysia na Shirika la ndege la Malaysia kuendelea kulaumiwa. Nakuhakikishia kuna taarifa ambazo Boeing na CIA wanazijua na hawawezi kuzisema. Ubaya ni kwamba hata tukitoa taarifa kuhusu CIA na Boeing kwa sababu fulani fulani vyombo vya habari havitaripoti au watapotosha……. Ndege ya Malaysia iko mahala fulani pengine imeshatolewa herufi MAS (Malaysia Airlines) na CIA wanajua ilipo."

Huu ndio msimamo wa moja wa viongizi mahiri zaidi kuwahi kutokea hapa duniani.
Dr. Mahathir Mohammed aliandika kabisa makala kuhusu uhusika wa CIA kwenye tukio hili la Flight 370 na unaweza kuisoma makala hii hata sasa kwenye tovuti yake.

Sitaki kukwambia yule mtafiti Blaine Gibson aliona nini kule Madagascar walichogundua baharini ambacho kilisababisha mwanadiplomasia wa Malaysia Bw. Zahid Raza kupigwa risasi mchana kweupe… lakini ninachojua ni kwamba iko siku CIA watajitokeza hadharani na kuomba radhi kama ambavyo wamekuwa wakiomba radhi kwa matukio yote waliyohusika na awali kukana uhusika wao.

Labda sio mwaka huu au mwakani au hata miaka mitano ijayo.. lakini iko siku kitendawili hiki kitapata jawabu lililo wazi kabisa na nina hakika kuna kikundi cha watu wataomba radhi jamii ya kimataifa.
Tusubiri.


[​IMG]
Dr. Mahathir Mohammed... Baba wa Taifa la Malaysia akihutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni

Post a Comment

0 Comments