Niliisha kwisha kuelezea katika makala zangu zilizo tangulia, ambazo zilichapishwa wenye gazeti la mtanzania kuwa kuna uwezekano mkubwa Bin Laden alishakufa tangu 2001, lakini maadui zetu hawatatangaza kifo chake mpaka watakapo maliza kazi na jina lake.
Nilisema hayo nikiambatanisha na ushahidi wa kutosha wa namna gani Osama anaweza kuwa ameshakufa kuliko kuwa hai, na nikaongezea kuwa maadui zetu watakapo maliza kazi na jina lake hawatosema wamemkamata bali wamemuua, tena kwa kikosi maalum.
KILIKUWA NI KIKOSI MAALUM
Na ndicho kilicho tokea. Inaonekana nilikuwa sahihi tangu mwanzo.
Sina haja ya kurudia tena hapa kuwa ni namna gani utawala wa Bush ukishirikiana na serikali vivuli za siri na asasi za siri walivyoweza kufanikisha 9/11 na kumrushia lawama zote Bin Laden. Lakini huenda baadaye nikarusha post zinazo muhusisha Bush moja kwa moja na 9/11, Ila nitakachozungumzia hapa kwa kina ni mustakabali wa ajenda nzima baada ya kifo cha bin Laden.
Kuna ushahidi wa kutosha kuwa bin Laden alishakufa tangu 2001.
Kwa kuanzia wakati Obama anatangaza kifo cha Osama Bin Laden kupitia kwenye luninga, kile ambacho watu wengi walikuwa hawakifahamu ni kuwa Obama alikuwa ni mtu wa tisa kwenye orodha ya viongozi wakubwa kiserikali kutangaza kifo hicho, yaani hiyo ilikuwa ni mara ya tisa kwa Osama kutangazwa kuwa amekufa.
Mr. OBAMA NA STAFF WAKE WAKIFUATILIA KWA MAKINI 'TUKIO'
Bin Laden alikuwa na tatizo la figo na alikuwa akihitaji mashine ya kusafishia damu , hili limeelezwa mara kadhaa na viongozi wa kiserikali wananchi mbalimbali, hivyo alishakufa muda mrefu hata kabla Obama hajakitangaza kifo hicho na yeye kuwa ni mtu wa tisa kufanya hivyo. Ni kama Osama amekufa mara tisa na kufufuka kila mara.
Wakati shambulizi la 9/11 likitokea, Osama alikuwa amelezwa kwenye hospitali ya kijeshi Pakistan akitibiwa tatizo lake hilo la figo. October 2001, Bin Laden alitokea kwenye video akiwa kavalia kijeshi na kajifunga kilemba, mwili umedhoofu na anaonekana kukonda.
BIN LADEN ALIVYOONEKANA MWAKA 2001, OKTOBA
Disemba 2001 akatokea kwenye video nyingine, akiwa kavalia kijeshi na kilemba, lakini hapa alionekana amechoka zaidi na afya yake imedhoofu maradufu kiasi kwamba hakuweza hata kunyanyua mkono wake wa kushoto.
BIN LADEN ALIVYOONEKANA MWAKA 2001, DISEMBA
Ilipofika Disemba 26, 2001, Fox News ilirusha habari iliyoichukua kutoka katika gazeti la Pakistan Observer ikisema kuwa viongozi wa Taliban walitangaza rasmi kifo cha Osama mapema mwezi Disemba 2001, na kwamba alizikwa ndani ya masaa 24 kama zilivyo taratibu za Kiislam.
TAARIFA YA TALIBAN JUU YA KIFO CHA OSAMA MWAKA 2001.
Januari 18, 2001, Rais wa Pakistan Pervez Musharraf alinukuliwa akisema kuwa, Osama Bin Laden alishakufa. Musharaf akaendelea kusema kuwa alifahamu Osama amechukua mashine mbili za kumuwezesha kuishi kama njia ya kusafishia damu yake kwa vile figo yake imekufa na mazingira ya kuhama hama anayoishi, pamoja na wataalam ambao wanahitajika kuziendesha mashine hizo, na umeme pia, ni vigumu kusema kuwa Osama yuko hai, na picha zake za hivi karibuni zinamuonesha amezidi kudhoofu.
Julai 17, 2001, kiongozi wa FBI kwenye kitengo cha kupambana na ugaidi, bwana Dale Watson alisema haya:
‘Mimi binafsi nafikiri Osama hayuko pamoja nasi tena’
October 2001, rais wa Afighanstan na kibaraka wa Illuminati, Hamid Karzai kupitia kwenye mahojiano na CNN alisema hivi,
‘ Naamini Bin Laden ameshakufa.’
Novemba 2001, Senator Harry Reid alisema kuwa ameambiwa kwamba Osama alikufa kwenye tetemeko la aridhi lilitokea Pakistan October, 2005.
September 2006, kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kilivujisha habari kuwa Osama bin Laden amefia Pakistan.
Novemba 2, 2007, aliyekuwa waziri mkuu wa PakistanBenazir Bhutto alisema kwenye mahusiano na kituo cha Al-Jazeera kuwa Osama bin Laden ameshauwawa na akamtaja muuaji wa Osama kuwa ni Omar Sheikh. Bhutto aliishi wiki moja tu baada ya mahojiano hayo, aliuwawa na mtu wa kujitoa muhanga.
Machi 2009, mtu aliyeshikilia wadhifa kwenye kitengo cha ulinzi cha Marekani na ambaye ni profesa katika chuo cha Buston bwana Angelo Codevilla alisema kuwa Elvis Presley anaweza kuwa hai lakini si Osama.
Mei 2009, kiongozi wa Pakistan, Asif Ali Zardari alisema kuwa, mashirika ya kijasusi ya Marekani hayajasikia chochote kutoka kwa Osama kwa miaka saba na sidhani kama bado yupo hai.
Leo hii Obama kaongezeka kwenye orodha ya watu hao mchanganyiko waliotangaza kifo cha Osama. Wengine wanaweza kusema taarifa za viongozi hao walio tangulia kabla ya Obama hazina ushahidi wa kutosha bali ni maneno matupu.
Lakini Pia taarifa ya Obama haina ushahidi wowote zaidi ya picha za mtu ambaye anaonekana nusu ni Osama, nusu mtu mwingine. Hata hivyo picha hizo tumeshazigundua kuwa ni za kughushi.
INGAWA BINA LADEN 2001 ALIKUWA MZEE SANA, LAKINI ALIPOKUFA MWAKA 2011 ALIONEKANA KARUDI KUWA KIJANA, KAMA ALIVYOKUWA AKIONEKANA KWENYE MIAKA YA 90, MAAJABU HAYA ...
Picha ya mtu asiyefahamika ambayo imeunganishwa na ile ya Osama ilikuwepo kwenye mitandao mikubwa kwa muda wa miaka miwili, kabla ya tarehe 1 Mei ambapo Obama alituambia kuwa picha hiyo ni ya Osama.
Picha hiyo ya mtu asiyefahamika ilikuwepo kwenye mtandao wa The Mail, Times, Telegraph, Sun na Mirror, hata hivyo mitandao hiyo iliiondoa picha hiyo kimyakimya baada ya kufahamika kuwa ni ya kughushi.
Picha ya Osama iliyounganishwa na picha ya mtu asiyefahamika ni ya mwaka 1998. Ndio maana kwenye picha hiyo anaonekana amekufa akiwa bado na afya, wakati video yake ya mwaka 2001 Disemba alikuwa amedhoofu kiasi hawezi hata kunyanyua mkono wake wa kushoto.
Hivyo kama unashaka na kifo cha Osama kwa vile walio tangulia kusema kabla ya Obama hawana ushahidi basi kuwa na shaka na taarifa ya Obama pia kwani ushahidi wake ni wakutengeneza.
Hakuna aliyeioyana maiti ya Osama, (hata samaki kwenye bahari ambayo mwili wa Osama umetupwa wanadai hawajauona mwili wake, ha hah ha hah ha …. Cheka kwa afya)
Obama na uongozi wake bado unajadili ikiwa kuna haja ya kuzitoa picha zingine ama la. Mazishi yake yamefanyika ndani ya masaa 12, baharini, ajabu wanasema hakuna nchi ambayo ingekubali kuupokea mwili huo. Sidhani kama wangwauliza Alshabab kama wanautaka ama la, nadhani alshabab wangefurahia kuwa na kaburi la Osama ndani ya Somalia ...
Ni vipi tukachukua maneno yao yasiyo na ushahidi watu ambao mpaka leo wanaendelea kutudanganya kuwa ni Osama ndiye aliyehusika na shambulizi la 9/11?
Osama ametangazwa amekufa nini kinafuata.
Kama nilivyo kwisha kusema kuwa kifo hicho kingetangazwa pale tu, Illuminati watakapo kuwa hawana haja na jina hilo kwenye ajenda yao.
PICHA ILIYO FANYIWA 'ADOBE' YA 'OSAMA' AKIWA AMEKUFA
Ndio kusema jina la Osama limeshamaliza kazi yake?
Ndiyo wameshamaliza kazi na jina la Osama na sasa watatumia mzimu wa Osama kuifikisha ajenda pale inapotakiwa.
Au kwa maneno mengine jina la Osama lilikuwa muhimu katika kufanikisha uvamizi wa Afighanstan na Iraq na kuzizorotesha baadhi ya nchi kiulinzi na kiusalama kama vile Pakistani, sasa tunakwenda kwenye hatua ya pili ya vita dhidi ya ugaidi, hatua ambayo haitakuwa na maana kuitangaza kama Osama atakuwa bado yupo hai, hivyo ‘Osama Must Go’ kama walivyokuwa wakisema Wakenya dhidi ya Moi ... huwezi kuanzisha vita vingine wakati vile vya awali kunayo kila dalili na ushahidi kwamba umeshindwa ... NA WAKATI WA KUINGIA HATUA YA PILI YA VITA DHIDI YA UGAIDI ULIKUWA UMEFIKA, HIVYO ‘GAIDI’ LAZIMA AONDOLEWE ILIKUTOA NAFASI YA ‘KUFUNGA VITABU’ VYETU HASA UKICHUKULIA KWAMBA HATUA YA PILI INGEKUWA NA MKANGANYIKO WA HABARI KAMA ‘GAIDI’ ANGEKUWA BADO YUPO HAI.
Kwa wale waliokuwa wanafuatilia taarifa za kifo cha Osama kupitia vyombo vya habari watakuwa waligundua kitu kimoja muhimu ambacho kinapaswa kufanywa na mzimu wa Osama Bin Laden. Taarifa za kifo cha Osama ziliambatana na hofu na vitisho kwa taifa la Marekani kuwa wafuasi wa Osama bin Laden watalipiza kisasi cha kiongozi wao.
Uwongo mtupu watalipiza vipi kifo cha Osama ambaye alishakufa karibu miaka 10 iliyopita? Haikuchukua muda wale wanaojiita ni viongozi wa Talibani wakaanza kutoa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa watalipiza kisasi cha kiongozi wao. Moja na moja ni mbili, wanaojiita Talibani, Al-Qaeda, Al-Shabab na wengine watakao kuja lao na Illuminati wote ni kitu moja, tumeshaona Osama alishakufa muda mrefu lakini kwa vile ajenda ilitaka kuendelea kulitumia jina lake hawakutangaza, na wala viongozi wa Al-Qaeda na Talibani hawakuwaambia walimwengu kuhusu hilo, taarifa za awali za kifo chake zilizo tokana na Talibani hazikutangazwa tena, wala wakati CIA na wenzake wakishirikiana kutengeneza video na audio za kughushi za Osama, Talibani wala Al-Qaeeda hawakuja kusema kuwa video na sauti hizo ni za kughushi, walinyamaza kimya, kwani ndivyo ajenda ilivyo taka, na wao na Illuminati ni pande mbili za shilingi, leo Illuminati wanatutangazia kifo cha Osama kwa mara ya tisa Talibani na Al-Qaeda wanajitokeza na kuthibitisha kifo, lakini hawaishii hapo na mrithi wa Osama wanamchagua.
MOJA YA VIDEO FAKE ZA OSAMA ZILIZO TOLEWA NA FBI, WALIKUWA NAZO NYINGI SANA KILA PALE ILIPOHITAJIKA MOJA, WALIZINDUA HASA KUPITIA ALJAZEERA, NA ZILIKUWA ZINAUZA KWELI, MPAKA AUDIO, BUSH NDIYO ALIFAIDIKA SANA MAUZO YAKE MPAKA AKACHAGULIWA MARA YA PILI KUWA RAIS WA MAREKANI, NAFIKIRI BUSH ATAMISI SANA BIN LADEN.
Waongo, wanafiki na wahaini wakubwa, wanaurubuni umma wa Kiislam kwa kujifanya wana uchungu na kifo hicho na kwamba wataendelea kuutetea Uislamu, lakini kumbe wanafanya kinyume chake kabisa, wao na Illuminati lao ni moja. Haijachukua muda vibaraka hao wa Illuminati walifanya shambulizi Pakistan na kuuwa watu wapatao 80 katika kile walichokiita kulipiza kisasi cha Osama, lakini tunajua hawalipizi kisasi bali wanaiandaa Pakistan na nchi zingine za Kiislam kushiriki kwenye WWIII. Na hii kwa taarifa yako ndiyo hatua ya pili ya vita dhidi ya Ugaidi.
Hivyo ndivyo mzimu wa Osama utakavyo endelea kutumika, wale wana jinadi kuwa ni Talibani na Al-Qaeda wataendelea kushambulia maeneo mbalimbali duniani kwa kisingizio cha kulipiza kisasi cha kiongozi wao. Wataachiwa wasambae kila kona ya dunia, leo kuna makelele mengi yanapazwa kuwa tayari wapo ndani ya Afrika Mashariki kupitia kwa ndugu zao wa Al-Shabab ambao nao walitangaza kujiunga na Al-Qaeedah kuwa kitu kimoja.
Tanzania na sisi hatupo salama kwenye, si kwamba hatupo salama kwa vile KUNAUGAIDI TANZANIA! HAPANA, HATUPO SALAMA KWA VILE TANZANI AHAKUNA UGAIDI, KAMA AMBAVYO DUNIANI HAKUNA UGAIDI LAKINI JUHUDI ZA MAKUSUDI ZIMEFANYA NA WANAO PIGANA ‘VITA DHIDI YA UGAIDI’ KUTENGENEZA JINAMIZI HILO DUNIANI, NA JUHUDI HIZO NAONA ZINAANZA KUSHIKA MIZIZI HAPA TANZANIA, NA TARATIBU WANAANZA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA UHASAMA BAINA YA WAISLAMU NA WAKRISTO ILI KUTOA MWANYA WA JINAMIZI HILO KUWEPO HAPA TANZANIA.
Picha kubwa inaonekana kuwa katika moja ya mashambulizi haya ya kulipiza kisasi, kuna kubwa ambalo litafanyika baina ya mwaka huu na mwaka unao kuja kiasi kwamba athari ya shambulizi hilo, litaweza kuipigisha ajenda hatua nyingine kubwa kama tukio la 9/11 lilivyo fanya.
Kipengele hicho hapo juu nilikiandika muda mrefu sana wakati bado naandika makala kwenye gazeti la Mtanzania, hivyo sikuwa nikifahamu ni tukio gani kubwa litakalo fuata katika kuwasogeza walimwengu uso kwa uso na WWIII .... Ila sasa nimefahamu.
Nadhani hatua hiyo kubwa itakuwa ni ya mwisho kuelekea kwenye WWIII au kuandaa mazingira ya mwisho ya vita hivyo vikubwa vinavyo subiriwa ili NWO isimame.
Endelea kufuatilia habari kwa makini na utaona mzimu huu wa Osama utakavyo tumika kufanikisha hilo. Kitu kingine cha kuangalia ni tarehe, utakumbuka ni September 1991 Bush baba aliitangaza ajenda hii rasmi ndani ya bunge la Marekani, Miaka 11 baadaye tukio kubwa na la muhimu la kufanikisha ajenda likatokea, nalo ni maarufu kama 9/11. Tukiwa tumebakiza miezi michache kabla ya miaka 11 kutumia baada ya 9/11 kifo cha Osama kinatangazwa, hii ni muhimu kwa sababu kwa kutumia kifo hicho tukio jingine kubwa la kuipigisha ajenda hatua linahitajika, tizama kalenda yako vizuri, baina ya mwaka huu na mwaka ujao utausikia mzimu wa Osama ukifanya kazi nyingine muhimu kwa ajili ya ajenda.
Tukio lenyewe ni kile kinacho endelea Mashariki ya Kati hivi sasa na kile kinachoendelea kwa baadhi ya nchi za Kiarabu zinazo patikana kwenye ukanda wa Afrika.
Waingereza kwa kutumia mamluki wao baada ya kuiangusha dola ya kiislamu kwenye WWII, Dola ya Ottoman, eneo la Mashariki ya kati ambalo mwanzo lilikuwa chini ya Dola hilo lilikuwa ni kubwa sana, hivyo kwa harakaharaka Freemason wa Magharibi hawakuweza kulihamishia eneo lote kwa familia zao za kishetani za Illuminanti, waliacha maeneo hayo kwa watu ambao walishirikiana nao kuiangusha Dola hiyo ya Kiislamu na lengo lao kubwa wakati huo ilikuwa ni mafuta na utaona baina ya hapo mafuta yote ya Mashariki ya Kati yalihamishiwa kwa wamiliki wa Ulaya.
Illuminanti wa Ulaya wakishirikiana na vibaraka wao wa Mashariki ya kati ambao wakijiita ni waislamu wakaanza kuvuna mafuta, lakini juu ya yote kwa kutumia mafuta hayo Illuminanti wakishirikiana na vibaraka wao wakazizamisha nzhi zinazo endelea katika mzigo mkubwa wa madeni na kuipatia Marekani U-Super Power baada ya kuamua kuwa mafuta yote yauzwe kwa sarafu ya Dola.
Sasa vibaraka wamelishwa na kunenepa mpaka wakasahau kuwa wao ni wanasesere mbele ya Illuminanti na wanamilikiwa na Illuminanti, katika hatua hii ni vigumu mno kumuambia kibaraka kuwa, mafuta peke yake siyo lengo la sisi kukuweka hapo, tunataka kuitawala dunia nzima ukiwemo wewe mwenyewe na wananchi wako.
Hivyo watu wengine walio andaliwa vyema na wenye maono mapana ya ajenda na mitazamo yake, wenye kufikiri kama ajenda inavyo taka, ndiyo wanao takiwa kuingia hapo kwenye hivyo viti, hivyo vibaraka wa zamani lazima waondoke kupisha vibaraka wapya watakao visogeza vita dhidi ya ugaidi kwenye mlango wa WWIII.
Hichi ndicho kinacho zikumba nchi za Kiarabu hivi sasa, yanayo itwa mapinduzi si chochote si lolote ni moja ya mipango kamambe, iliyo pangwa na kuratibiwa vyema katika kufanikisha zimwi la ugaidi kwenye hatua ya pili. Viongozi hawa wapya ndio watakao ulazimisha umma wa Kiislamu kuungana dhidi ya magharibi, na hiyo ndiyo kazi yao wanayo pewa. Hilo ndiyo lengo la vibaraka hao wapya, hawa ndiyo watakao washa cheche zitakazo lipua nyuklia ya kwanza kwenye uwanja wa WWIII.
Karata ya mwisho ya mchezo mzima ni kuwaingiza waumini wa Kiislam kwenye uwanja wa vita dhidi ya ulimwengu. Vita hivi ndivyo vitakuwa vita vikubwa kupiganwa kwenye uso wa dunia, tangu historia ya binaadam ilipo anza kuandikwa. Vita hivi ndivyo vitakuwa vita vikubwa kuliko vyote katika zama zetu, vita hivi vitaitwa WWIII, na baada ya hapo wanategemea kusimamisha NWO.
Hivyo Obama alikuwa radhi kumfufua Osama Bin Ladeni kwa mara ya tisa na kumuuwa tena kwa ajili ya kupisha njia mapinduzi mapya tunayo yaona hivi sasa
Source | SalimMsangiBlog.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena