Header Ads Widget

Responsive Advertisement

#KUNGUNI wageuka Dili Shirati

Lazaro Steven ambae ni Mtengenezaji na Mfanyabiashara wa dawa ya kuua wadudu wasio na Uti wa Mgongo kama vile Mende, Kunguni na Viroboto akiwa katika Soko la Obwele Shirati Wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
 Na: George Binagi-GB Pazzo
Biashara ya wadudu wasumbufu majumbani hususani kitandani aina ya Kunguni imevuta kasi na hivyo kushamiri sana katika Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, kutokana na wadudu hao kutumika kwa ajili ya majaribio ya dawa ya kuulia wadudu mbalimbali wakiwemo Mende, kunguni na Viroboto.

Hayo yalielezwa na Lazaro Steven ambae ni mkazi wa Mtaa wa Maswa Igoma Jijini Mwanza, wakati akizungumza na Binagi Media Group akiwa akiwa katika Soko la Obwele lililopo katika Mji wa Shirati Rorya Mkoani Mara kuhusiana na namna ambavyo Kunguni wamekuwa mhimu kwa ajili ya biashara yake.

Alisema kuwa alianza kutengeneza na kuuza dawa ya Kuua wadudu mbalimbali wasio na Uti wa Mgongo ambao ni pamoja na Mende, Kunguni na Viroboto, lakini akakumbana na changamoto ya wateja wake kutoamini kama dawa hiyo kama inaua wadudu kweli.

Kutokana na changamoto hiyo, aliamua kupita majumbani na kuomba watu walio na kunguni waweze kumpatia kwa ajili ya kuwatumia katika majaribio ya dawa anayoiuza ambayo inafahamika kwa jina la Fagilia ama Kausha ambayo hutengenezwa kwa miti shamba.

Steven alisema kuwa mtu akimpelekea Kunguni huweza kujipatia chupa moja ya dawa ya Kuua wadudu yenye thamani ya Shilingi 1,500 ambapo yeye huwatumia kunguni hao kwa ajili ya majaribio ya kuwaonyeshea wateja wake kama kweli dawa yake inaua wadudu.


Mbali na kubadilishana dawa kwa kunguni, pia mtu mwenye kunguni anaweza kujipatia kiasi cha fedha kuanzia shilingi 1,500 kutoka kwa bwana Lazaro Steven ikiwa hatokuwa tayari kuchukua dawa ya Kausha ama Fagilia kama inavyojulikana, huku akiongeza kuwa dawa hiyo amekuwa akiitengeneza kutokana na miti shamba na imeleta mafanikio makubwa katika kuua wadudu mbalimbali ukilinganisha na dawa alizoziita za Serikali akiwa na maana ya dawa za kisasa zinazouzwa madukani.

Lazaro Steven (Kulia) ambae ni Mtengenezaji na Mfanyabiashara wa dawa ya kuua wadudu wasio na Uti wa Mgongo kama vile Mende, Kunguni na Viroboto akihojiwa na George Binagi-GB Pazzo (Kushoto) katika Soko la Obwele Shirati Wilayani Rorya Mkoa wa Mara.

Post a Comment

0 Comments