Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Mwandishi wa Habari avamiwa na Vibaka

repotaMwandishi maarufu wa kituo cha Televisheni kutoka Afrika Kusini amevamiwa na vibaka hadharani wakati alipokuwa akijiandaa kurusha habari hewani akiwa mbele ya kamera yake.
Katika mkanda wa video umewaonyesha wanaume wawili wakimvamia Vuyo Mvoko, akiwa mbele ya kamera za Televisheni ya Taifa ya SABC ambapo alikuwa nje ya hospitali moja ya mjini Johannesburg akiripoti kuwasili kwa rais wa Zambia ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.


Hata hivyo mwandishi huyo alisema kuwa mmoja wa wezi hao alimtishia na bunduki alipokataa kumpa simu yake huku wakionekana kutojali kamera zilizokuwa mbele yao.
Baada ya mda mfupi bwana Mvoko ambaye ni mhariri wa kituo hicho cha habari alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa yuko salama salmin na kutuma kanda ya video hiyo mtandaoni.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wezi hao waliiba laptopu, na simu na kwamba maafisa walikuwa tayari wanachunguza kisa hicho

Post a Comment

0 Comments