Namshukuru Jalali kwa kuniwezesha kukutana tena na wewe msomaji wangu mpendwa wa safu hii nzuri ambapo tunajuzana, kushauriana na kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi .
Mada yetu ya leo, kama inavyojieleza kwenye kichwa cha habari , ni mambo unayopaswa kuyafanya unapogundua mpenzi wako amekusaliti wakati bado
unampenda na unahitaji kuendelea kuwa naye katika uhusiano wa kimapenzi .

Vitabu vya dini zote vinaeleza kuwa kosa pekee linaloweza kuivunja ndoa , hata ile
iliyofungwa kwa baraka za Mungu , iwe ni madhabahuni au msikitini , ni USALITI.

Yaani hata kama ulikuwa unampenda vipi, ikitokea amekusaliti na umegundua ukiwa
na ushahidi , una haki zote za msingi za kutoa/kudai talaka au kuachana kabisa (kama bado hamjaoana).

Hata hivyo, kuna mazingira ambayo yanaweza kukutokea , ukagundua mkeo,
mumeo, mchumba au mpenzi wako amekusaliti lakini kutoka ndani ya moyo wako , ukawa haupo tayari kuachana naye
kwa sabahu bado unampenda sana licha ya kwamba amekukosea .

Kutokana na maombi maalum ya wasomaji wangu kadhaa ambao wamekutana na hali
kama hiyo na hawajui cha kufanya, ndiyo maana leo nimeamua tuijadili mada hii na
wewe msomaji wangu .

Naamini mimi peke yangu sijui kila kitu wala ushauri wangu hauwezi kuwa wa
mwisho lakini nataka kukushirikisha wewe
msomaji wangu , hebu niambie utafanya nini unapotokewa na tukio kama hili ?

Unampenda kwa moyo wako wote ,umemfanyia mambo mengi lakini mwisho ukagundua kuwa amekusaliti, utafanya nini?
Mapenzi yamegeuka shubiri, usaliti na maumivu ya moyo yamegeuka na kuwa
sehemu ya kawaida katika uhusiano wa kimapenzi. Watu wengi wanalia kwa sababu
wanasalitiwa au waliwahi kusalitiwa na wenzi wao, si wanawake, si wanaume, si wanandoa, si wachumba wala wapenzi !

Zipo sababu nyingi zinazosababisha usaliti
lakini lengo langu leo siyo kuzungumzia hilo bali ni kujaribu kuiponya mioyo ya wote waliojeruhiwa na watu wanaowapenda sana kwa kuwasaliti .

Yawezekana ulitokea kumpenda sana mwenzi wako , ukaamini wewe ndiyo kila kitu kwake , ukamtimizia kila kilichokuwa
ndani ya uwezo wako lakini mwisho,ukaambulia maumivu baada ya kugundua
kuwa yupo mwingine anayekuibia mali zako.

Sitaki kupingana na maandiko ya vitabu vitakatifu au sheria ambazo zipo wazi kwamba malipo ya usaliti ni kuvunjika uhusiano lakini nataka tujadiliane, ni lazima kila unapogundua kuwa mwenzi wako amekusaliti dawa yake ni kupeana talaka au kuachana kwa ugomvi?
Mathalani umefunga ndoa na kuishi na mwenzi wako kwa kipindi kirefu mkipendana , kujaliana na kuoneshana kila
aina ya mahaba lakini akateleza na kukusaliti ilihali bado anakupenda na wewe unampenda, utakapoamua kuachana naye na kwenda kwa mwingine, ukigundua naye anakusaliti utafanya nini ?

Utaachana na wangapi? Siyo mara zote talaka au kuachana huwa suluhisho la usaliti ndani ya ndoa .Siwafundishi watu wasaliti ndoa zao au uhusiano wao kwa makusudi wakitegemea kusamehewa, hapana.
Nataka uelewe kwamba hata baada ya mwenzi wako kukusaliti, bado mna nafasi ya kuendelea na maisha yenu ikiwa wote wawili mtaamua kulishughulikia tatizo hilo kwa kina bila kujali watu wa nje wanasemaje.
Usikilize moyo wako , ni kweli amekusaliti ! Amekuumiza, unahisi dunia yote imekuelemea, unatamani kufa au kuua
,lakini je, moyo wako unakuambia nini?
,lakini je, moyo wako unakuambia nini?
JE,NINI CHA KUFANYA UNAPOSALITIWA ?
1. JIPE MUDA WA KUTAFAKARI
Sote tunakubaliana kwamba hakuna kipindi kigumu kwenye mapenzi kama unapogundua kuwa mwenzi wako
amekusaliti. Ni katika kipindi hiki mtu anaweza kujidhuru mwenyewe, kumdhuru
mwenzi wake au mwizi wake .

Hata hivyo, wataalamu wa mapenzi wanaeleza kwamba hatua ya kwanza na ya
haraka ambayo unatakiwa kuichukua baada ya kugundua kuwa mwenzi wako
amekusaliti, ni kujipa muda wa kutafakari kwa kina kuhusu kilichotokea .

Tafuta sehemu tulivu , kaa ukiwa peke yako na tafakari kwa kina juu ya kilichotokea .
Anza kwa kujichunguza mwenyewe kwani
yawezekana umesababisha mwenzi wako
akusaliti.
Anza kwa kujichunguza mwenyewe kwani
yawezekana umesababisha mwenzi wako
akusaliti.
Maamuzi ya busara hayafanywi ukiwa na hasira, ukijipa muda wa kutafakari utagundua kilichosababisha akusaliti .
2. USIKILIZE MOYO WAKO
Jiulize ndani ya moyo wako kwamba licha ya yote yaliyotokea , bado unamhitaji mwenzi wako na upo tayari kumsamehe ?

Uzuri wa mapenzi , moyo ndiyo
huzungumza ukweli , kama humhitaji tena, chukua uamuzi wa kuachana naye lakini
kama bado unampenda , mpe nafasi ya pili .
Epuka kuchukua uamuzi kwa hasira kwa sababu unaweza kuamua kumuacha wakati
moyo wako bado unamhitaji baadaye ukaja kujuta. Yafikirie mambo mazuri mliyowahi
kuyafanya pamoja kisha yapime.

3. ZUNGUMZA NAYE
Ukishakuwa umezifanyia kazi hatua hizo mbili za hapo juu , tafuta muda wa kuzungumza na mpenzi wako na muulize
kwa upole kwa nini amekusaliti.
Mpe muda wa kujieleza na msikilize kwa umakini.

Ikiwa anaonesha kujutia makosa
aliyoyafanya na akakuomba msamaha kutoka ndani ya moyo wake na kuahidi kutorudia tena, mpe nafasi ya pili .
Ukiamua kumsamehe , kweli umsamehe na
usibaki na kinyongo ndani ya moyo wako .

4. WASHIRIKISHE WATU UNAOWAAMINI
Yawezekana ukahisi umekosewa sana kuliko mtu mwingine yeyote lakini ukijaribu kuzungumza na watu unaowaamini ,
ushuhuda wao utakusaidia kuona kila kilichotokea kuwa ni cha kawaida .

Kama ndoa yenu ni changa, jaribu
kuzungumza na watu walioishi kwenye ndoa kwa muda mrefu na utashangaa kugundua kuwa wengi walishawahi kusalitiwa lakini wakawasamehe wenzi wao
na maisha yakaendelea .

Ni matumaini yangu kuwa mbinu hizo zitakusaidia kukabiliana na hali hiyo ngumu na utampenda tena pengine zaidi ya ulivyokuwa unampenda mwanzo .
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena