Ukiachilia mbali marais wengi wa Afrika kupenda kukaa kwa muda mrefu madarakani lakini kuna hili la kujilimbikizia mali, wengine huzipata kabla ya kuwa marais lakini wengi wao huzipata wakati wanashikilia madaraka kwa kipindi chote wanapotawala nchi husika.
Mohammed V1 Ni Mfalme wa Morocco ambaye amekaa madarakani kwa miaka 15 ,, ana utajiri wa dola bilioni 2.
Teodoro Obiang Nguema Mbasogo: Rais huyu wa Equatorial Guinea aliingia madarakani 1979, ana una utajiri wa dola milioni 600 licha ya wananchi wa nchi hiyo kuishi maisha ya kimaskini kutokana na uchumi wao kuwa chini
Uhuru Kenyatta ni Rais wa Kenya ambaye alichaguliwa mwaka 2011, ana utajiri wa dola milioni 500, mbali ya kuongoza nchi ana vyanzo mbalimbali vya utajiri ikiwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni mbalimbali,benki na mahoteli makubwa ya kifahari.
Paul Biya ni Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ana utajiri wa dola milioni 200, unaambiwa ndiye rais anayetumia kiasi kikubwa cha pesa katika ziara zake kuliko marais wote duniani na hutumia euro 30,000 kwa siku katika ziara zake
King Mswat iii Ni mfalwe wa Swazland akiwa na utajiri wa dola milioni 100, anashika nafasi ya 15 katika familia za kifalme tajiri duniani, Unaambiwa wake zake 13 hutumia zaidi ya dola milioni sita kufanya manunuzi yao pekee, pia Serikali yake hutenga bajeti ya dola milioni 61 kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena