Header Ads Widget

Responsive Advertisement

PICHA | FAHARI YETU. TAZAMA PICHA ZA WANAJESHI WETU KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO HAPO JANA.

Umewahi kuwaona Makomandoo wetu?? Kwa kweli najisikia mwenye amani sana na fahari kubwa pale ninapotazama kikosi hiki. Mwili hunisisimka ninapoona magwanda yao, hakika wanavutia na kupendeza!!! LONG LIVE TANZANIA!!!

jakaya 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMRjakaya3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. 
Picha na OMR

1 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr.Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na Wazee wetu Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, Dr. Jakaya kikwete ameongoza maelefu ya watanzania kwenye uwanja wa Taifa katika sherehe za kuadhimisha muungano huo sherehe zilizohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Vyama vya Siasa, viongozi wa dini na wananchi wageni waalikwa kwa ujumula2 
Rais Jakaya Kikwete akiendelea kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa.345 
#Vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikiwa vimejipanga katika gwaride hilo.6 
Rais Jakaya Kikwete akirejea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa.7 
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu kwa ajili ya kumpokea Rais Dr. Jakaya Kikwete.8 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania.9 
#Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Pandu Ameri Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mara baara ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania.10 
#Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh, Seif Sharif Hamad mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania, Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  Dr. Gaharib Bilal na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.11 
Rais Jakaya Kikwete akiakizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein huku Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiwaangalia kushoto ni Mke waRais Mama Salma Kikwete na kulia ni Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal.  wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania12 
Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka Vikosi vya ulinzi na usalana wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.13Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino Lyatonga Mrema akiwa ameungana na wageni wengine waalikwa katika maadhimisho ya sherehe hizo.14 
Kikosi Cha bendera kikitoa heshima zake Mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho hayo. 15 
Vikosi vya ulinzi na usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Mh Dr. Jakaya Kikwete.16 
Kikosi cha Mizinga kikipita na kutoa heshima zake17 
Kikosi cha wanamaji wanawake kikipita18 
Kikosi maalum cha walinzi wa viongozi kikipita na kutoa heshima.19 
Kikosi maalum cha mizinga ya kutungulia ndege kikitoa heshima zake20 
Kikosi maalum cha Makomandoo kikitoa heshima zake21 
Kikosi cha makomandoo wana maji kikipita na kutoa heshima.22 
Kikosi cha FFU kikipita 23 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.24 
Baadhi ya viongozi wakiwa katika sherehe hizo.25 
Wananchi mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo.

Baada ya Rais Kikwete kuingia alipokelewa na Mkuu ya Jeshi la Wananchi(JTWZ),Generali Davis Mwamunyange ambaye alimpeleka kukagua vikosi vya ulinzi na usalama.
 
Jeshi hilo limeonekana kufanya maboresho katika gwaride la mwaka huu ambapo waliandaa gadi 20 huku gadi 13 zikiwa nje ya uwanja na gadi 7 zikiwa ndani.
 
Gadi 13 zilizokuwa nje ya uwanja zilivalia mavazi ya mazoezi (Combat)huku wakiwa wamebeba vifaa vya kivita ambapo kati ya hizo,gadi 1 ilikuwa kikosi maalum cha makomandoo na gadi iliyobaki ilikuwa kikosi maalum cha wanamaji.
 
Gadi saba zilizobaki ndani kikiwamo na kikundi cha bendi walikuwa wamevaa mavazi rasmi ya gwaride.

Baada ya rais Kikwete kuingia ndani alipokelewa na Mkuu wa Majeshi(CDF), Davis Mwamunyange ambaye alimpeleka kukagua gadi saba zilizokuwa ndani huku mizinga 21 ikilia.
 
Baada ya kukagua, gadi hizo zilisogea mbele kwa hatua 15 kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa amiri jeshi mkuu na kuendelea kusimama ndani ya uwanja huku wakisubili gadi zilizokuwa nje ziweze kupita mbele ya amiri jeshi.
 
Gadi 11 zilipita kwa mwendo wa pole huku gadi mbili moja ikiwa kikosi cha makomandoo na wanamaji zilipita kwa mwendo wa kasi.
 
Viongozi Wanena:
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye maadhimisho hayo, baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wa serikali walisema kuwa muungano huo unapaswa kuigwa na mataifa mbalimbali.
 
Spika Mstaafu Pius Msekwa alisema vijana wana nafasi kubwa ya kuuenzi na kuendeleza muungano huo ili uweze kudumu miaka hamsini mingine.
 
“Sisi tumestaafu, tunawaachia vijana ili waweze kuendeleza, hivyo basi wanapaswa kuunga mkono na kuudumisha ili uweze kudumu miaka mia moja,”alisema Spika Mstaafu Pius Msekwa.
 
Alisema licha ya muungano huo kupitia kwenye mawimbi yaliyoibua kero za muungano, mpaka sasa wameweza kuyashughulikia na kubakisha mambo machache ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.
 
Akitolea mfano wa baadhi ya nchi ikiwamo Gambia na Senegal ambazo zilishindwa kudumisha muungano baada ya kujitokeza kwa migogoro ya hapa na pale.
 
Msekwa alisema kuwa ili kuonyesha kuwa muungano ni jambo la muhimu, ametunga kitabu maalum ambacho kimeelezea mambo mbalimbali yanayohusu muungano na misingi imara ya kuuenzi.
 
Naye Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema kuwa, muungano huo umeweza kuleta mafaniko makubwa katika Nyanja mbalimbali ikiwamo ya kiuchumi na kijamii.
 
Alisema hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuudumisha ili uweze kudumu miaka hamsini ijayo.
 
Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu, vijana wengi wanapaswa kujitokeza ili waweze kujiandikisha na kupiga kura.
 
“Ushiriki wa vijana kwenye kupiga kura kwa ajili ya katiba inayopendekezwa ni muhimu, kwa sababu inaweza kusaidia katika uchaguzi mkuu,”alisema Butiku.
 
Mtu  Mmoja  Akamatwa
Mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikamatwa na wanajeshi kwa kujifanya ni afisa wa usalama wa taifa.
 
Kijana huyo ambaye alionekana katika maeneo hayo akiwaongoza wananchi ili waweze kuingia ndani ya uwanja alikamatwa baada ya kubainika kuwa ni afisa feki wa usalama.
 
Baada ya kuhojiwa ilibainika kuwa aliwahi kuwa Askari wa Jeshi la Wananchi na kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu, jambo ambalo liliwafanya maofisa hao kumpeleka kituo cha Polisi Chang’ombe kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Post a Comment

0 Comments