Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | SASA OVENI ZATUMIA MKAA BADALA YA UMEME NA GESI

Wakati sayansi na teknolojia ikizidi kushika kasi duniani kote pamoja na mifumo ya kidijitali nayo ikipewa kipaumbele na mataifa mbalimbali ulimwenguni, hali hii imesababisha ongezeko kubwa la matumizi ya nishati ya umeme na gesi huku gharama za umeme zikipanda kutokana na kupanda na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la mafuta duniani. Je, watanzania na wanachi wa Afrika mashariki wanaweza kumudu gharama hizi za umeme? Na kama hawawezi ni nini msaada wao na kimbilio lao mbadala?


Kampuni ya Cookeswell Jikos iliyopo Nairobi nchini Kenya, ni mojawapo ya kampuni nchini Kenya ambayo ni mkombozi wa watanzania na wananchi wote wa Afrika mashariki pamoja ulimwengu kwa ujumla baada ya kubuni Oveni zinazotumia mkaa badala ya umeme katika kuoka mikate,biskuti n.k, kuchemsha maji, kupika mboga za majani na hata kuchoma nyama ili kuasaidia watu mbalimbali kama waokaji wa Mikate na wenye migahawa au maduka madogo ya kahawa kuepuka matumizi ya umeme katika mapishi na badala yake kutumia mkaa ambao kila mwanachi ana uwezo wa kumudu gharama zake na mkaa unaotumika si mwingi.

Akizungumza na Njia Mpya, mkurugenzi wa Cookeswell Jikos ndugu Teddy Kinanjui alisema Kampuni yao ina miaka mingi katika utaalamu wa utengenezaji wa majiko wakirithi kutoka kwa marehemu baba yao mzazi aliyekuwa mtaalamu wa utengenezaji majiko. “Kampuni ina miaka mingi na wataalamu waliobobea katika fani hii tuliamua kutengeneza hizi oveni zinazotumia mkaa ambazo unaweza ukafanya mambo mbalimbali kwa wakati mmoja tena kwa mkaa kidogo sana kama vile kuoka, kuchoma nyama au kuku, kurosti, kubanika na shughuli kadha wa kadha, majiko na oveni zetu zinamfaa kila mtu zipo za mtu mmoja ambaye hajaoa zinaitwa Bachelor Oven, kuna za familia zenye ngazi mbili kama vile safari oven na zote ni bei nafuu na uzuri wake unaweza kusafiri na jiko hizi mahali popote pale iwe porini au kwenye hifadhi kama wanavyofanya watalii na pia majiko na oveni hizi zinawafaa zaidi na waokaji ambao wana biashara zao na hata wauzaji wa kahawa na maduka madogomadogo ya kahawa kutokana na uimara na uwezo wa Majiko na Oveni zetu, gharama zetu ni kuanzia Ksh 35,00/= ” alisema.
Aidha alieleza gharama za majiko na oveni hizi kila mtu anazimudu kwani ni ndogo na zinapatikana kulingana na aina ya Oveni au jiko unalotaka. Pia alibainisha kuwa wateja wao wengi wanatoka nchi za Afrika mashariki, Afrika Kusini, marekani, Cambodia, Newsland, Uingereza, Congo DRC na nchi mbalimbali duniani na kubainisha kuwa kwa wale wanao hitaji majiko na oveni za jumla na rejareja vinapatikana na kuagiza ukiwa hata Tanzania unapata. “kwa watu wenye Mohoteli pia wasijali wanapata” Alimalizia.
Hivyo basi, kwa kulithamini hili kwa vitendo, Njia Mpya tumeagiza Safari Oveni moja itakuwa ofisini kwetu Kariakoo Dar es salaam Karibuni mjionee kwa macho na hata kununua na kukuagizia ukiwa Tanzania na ukaipata bila kwenda Kenya. Tanzania, wakati ni wetu tuokoe gharama kubwa na tutumie mkaa kiduchu kwaajili ya mapishi na kukuza biashara zetu kwa Oveni hizi na waokaji ni wakati wenu kwani Mkaa upo, Ardhi yetu ina rutuba nzuri na hali ya hewa safi.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na Ndg.Teddy +254700380009 au tembelea tovuti yetu www.njiampya.com , Simu 0712 202 133 Pia tembelea tovuti yao www.cookswell.co.ke au vidokezo(links) hiviwww.cookswell.co.ke/ovens

Post a Comment

0 Comments