Katika sehemu ya pili nilieleza namna ambavyo MH370 iliruka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur na mpaka kupotea kwake. Katika sehemu hii ya tatu nitaweka vielelezo vyenye kuonyesha utata wa mazingira ya ndege hii kupotea.
Tuendelee…
Wakati ambapo Waziri Mkuu wa Malaysia pamoja na shirika la ndege la Malaysia Airlines wakitoa taarifa kuwa wameipoteza ndege na wakiamini na kuaminisha ulimwengu kuwa ndege hii imedondoka baharini mahala kusiko julikana… lakini nyuma ya pazia kulikuwa na mambo ambayo yanaendelea.
Naomba ukumbuke kwamba taarifa hii ya "kudondoka" kwa MH370 ilitolewa na serikali ya Malaysia iliweka makisio ya muda wa kudondoka (kupotea) kuwa ni saa 01:21 MYT.
Pia tukumbuke kuwa katika sehemu ya pili nilieleza kwamba saa 01:19 sekunde ya 30 ndipo ambapo ilikuwa mara ya mwisho kwa ndege hii kuonekana kwenye rada ACC zote za Malaysia na nchi zote ambazo ilikuwa inatakiwa kupita kwenye anga lake. Hii ndio sababu ya kutolewa kwa taarifa kwamba ndege ilidondoka saa 01:21.
Ikapita siku ya kwanza huku msimamo ukibakia ule ule kuwa hawajui ndege ilikodondokea. Zikapita siku tatu, ikapita wiki ya kwanza na ikapita wiki ya pili na ya tatu huku msimmo ukibakia ule ule kwamba hawajui ndege ilikodondokea. Ndipo hapa haswa wajuzi wa mambo na jumuia ya intelijensia (ambao "hawakuusika") kukaanza kujengeka hisia kali kwamba kuna jambo ambalo lilikuwa linafichwa. Kuna masuala ambayo yalikuwa hayasemwi au wanaoyajua walikuwa wanahofu ya kusema.
Naomba usome kwa makini sana kipengele hiki kinachofuata.
Katika ndege kubwa ambazo zinafanya safari za kimataifa huwa na mfumo wa SATCOM (Satellite Communication). Ndege ikiwa angani mawasiliano yote yanafanyika kwa njia ya satellite hasa hasa ikiwa katika 'altitude' kubwa zaidi. Ili kuwezesha mfumo huu wa mawasilino kuna kifaa kinaitwa SDU (Satellite Data Unit). Huu ndio kama moyo wa mfumo wa SATCOM kwenye ndege. Kifaa hiki kinawasiliana na satellite kwa kutumia Radio Frequency (RF) na kisha satellite inawasiliana na kituo kilichopo ardhini (ground station).
Kama ambavyo nilieleza huko nyuma kwamba mawasiliano haya satellite yalikuwa yanafanyika kwa kutumia satellite ya kampuni ya Inmarsat (Satellite yao ya 'Inmarsat-3 series'). Lakini kampuni hii ya satellite huwa haina mkataba wa moja kwa moja na kampuni za ndege kutokana na shughuli zake za satellite kuwa na wigo mpana. Kwa hiyo wao wanaingia mikataba na makampuni makubwa na mawasiliano ya anga na kisha kampuni hizo ndizo zinaingia mikataba na mashirika ya ndege. Hivyo basi kampuni ya Malaysia Airlines katika masuala haya ya mawasiliano ya anga ina mkataba na kampuni inayoitwa SITA. Hawa ndio wanamkataba na Inmarsat na hivyo kiwezesha ndege za Malaysia Airlines kutumia Satellite za kampuni ya Inmarsat.
Kwa hiyo, ndege ikiwa inafanya mawasiliano na Satellite ambapo kama nilivyoeleza mawasilino hayo yanafanywa na kifaa cha SDU, kifaa hiki kwanza kabisa kitatuma ujumbe unaojulikana kama "log on request". Ujumbe huu unatumwa kwenye satellite na kisha satellite inatuma kwenye kituo cha ardhini. Ujumbe huu wa awali ni kama ndege "kujitambulisha" (lazima uwe na mkataba na SITA ambao wana mkataba na Inmarsat, kwa hiyo ujumbe huu wa "log on request" unatambulisha kwamba wewe ni 'active subscriber' wa huduma yao). Baada ya kituo cha ardhini kupokea ujumbe huu na kuaknowlemagde, baada ya hapo kila baada ya lisaa limoja unatumwa ujumbe mwingine kutoka kituo cha ardhini kwenda kwenye ndege kupitia Satellite, ujumbe huu unaitwa LOI (Log On Interrogation) au maarufu kama 'ping'. Katika nyanja ya mawasiliano ya anga, utaratibu huu unajulikana kwa jina maarufu la "handshake". Yaani ndege inafanya "handshake" kupitia satellite na ground stations kwenye nchi husika inapopita.
Sasa basi….
Wakati ambapo serikali ikitangaza kwamba ndege hii imedondoka muda wa saa 01:21 na hawajui imedondoka wapi, rekodi kutoka kwenye kituo cha ardhini cha Inmarsat kilichopo mjini Perth, Austaralia zinaonyesha kwamba saa 02:25 SDU kutoka kwenye ndege hii ilituma 'log on request'.
Baada ya kulog on kwenye mtandao wa satellite wa Inmarsat, SDU ya ndege hij iliendelea 'kurespond' kufanya 'handshakes' kila baada ya lisaa limoja na vituo vya ardhini vya Inmarsat.
Saa 02:39 ilipigwa simu ambayo iliita/ilifika kwenye cockpit ya marubani lakini haikujibiwa. Saa 7:13 ilipigwa simu nyingine ambayo nayo ilifika kwenye cockpit lakini nayo pia haikujibiwa.
SDU katika ndege hii ilirespond tena ilipotumiwa 'status request' kutoka kituo cha ardhini muda wa saa 08:10 (karibia lisaa limoja na dakika 40 mbele ya muda ambao ilikuwa inatakiwa kutua Beijing).
Saa 08:19 sekunde ya 29 SDU ilituma tena 'log on request'. Kituo cha ardhini kikatoa ruhusa. Na SDU kwenye ndege ikafanya aknowlegdement saa 08:19 sekunde ya 37.
Saa 09:15 (masaa mawili na dakika 45 mbele ya muda ilipotakiwa kutua Beijing) SDU kutoka kwenye ndege hii ilirespond kwa mara ya mwisho juu ya ombi la 'status request' kutoka kwenye kituo cha ardhini cha Inmarsat.
Naomba uone vitu viwili hapa muhimu sana,
Serikali ilitangaza kuwa ndege imedondoka saa 01:21 lakini SDU katika ndege hii iliendelea kufabya 'handshakes' na kituo cha ardhini cha Satellite ya Inmarsat masaa kadhaa mbele ya muda huo uliotangazwa kuwa imedondoka. Hata wakati ambapo watu wa serikali na shirika la Malaysia Airline wanaongea na vyombo vya habati mida ya 07:24 ndege ilikuwa bado hewani na ushahidi wa 'handshakes' ilizokuwa inafanya na ground stations unathibitisha hilo.
Lakini jambo la pili ambalo ni la kushangaza zaidi ni kitendo cha SDU kurespond kwa 'status request' muda wa saa 09:15 ambao ni zaidi ya masaa mawili na dakika 15 kutoka muda ambao ilikuwa inatakiwa kutua Beijing.
Kwenye sehemu iliyopita nilipoeleza kuhusu kiasi cha mafuta ambacho ndege ilijaza nilieleza kuwa ni muhimu kuikumbuka taarifa hii kwa sababu nitaiongelea tena huko mbeleni. Kama ulikuwa haujaikariri naomba nikukumbushe tena.
Nilisema kwamba, safari hii kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing ingetumia masaa 5 na dakika 34 ambayo ingekula mafuta ya kiasi 82,000 lb. Lakini ndege ilijazwa mafuta ya kiasi cha 108,200 lb na hivyo kuipa ndege 'endurance' ya masaa 7 na dakika 31 (saa 1 na dakika 57 ya ziada).
Lakini rekodi za satellite zinatuonyesha kwamba ndege hii bado ilikuwa hewani mpaka muda wa saa 09:15… yaani masaa mawili na dakika 45 ya ziada. Swali, MH370 ilipata wapi mafuta ya ziada kuweza kuwa hewani kwa extra time ya masaa mawili na dakika arobaini na tano??
Tukirudi tena nyuma inashangaza kuona difference kubwa hivi ya muda, kati ya muda ambao serikali ilitangaza kuwa ndege imedondoka (saa 01:21) na muda ambao SDU ya MH370 ilirespond kwa 'status request' ya mwisho (saa 09:15)… hii ni tofauti ya zaidi ya masaa 8. Inawezekana vipi serikali ikosee kiasi hiki? Na kama ndege iliendelea kuwa hewani kwa zaidi ya masaa manane kutoka muda uliokisiwa kudondoka, ilielekea wapi ndege hii… ilikuwa inaendeshwa kwenda wapi? Jeshi la Malaysia radar yao haifanyi kazi? Na kama inafanya kazi wanasemaje??
Naomba nigusie kidogo pia kuhusu vielelezo vilivyopo kutoka jeshi la Malaysia.
Tofauti na serikali ilivyotangaza kwamba ndege ilidondoka saa 01:21, rada ya jeshi la Malaysia iliiona ndege hii masaa kadhaa mbele ya muda huo.
Kwanza niseme kuwa Air Traffic Control wanatumua "Secondary Radar" (Secondary Surveillance Radar (SSR)) katika kujua ndege iliyoko angani na details zake. Secondary Radar yenyewe inafanya kazi kwa kuhisi 'signal' ambazo zinatolewa na transponder.
Kwa hiyo tunaposema kwamba ilipofika mida ya saa 01:19 Flight 370 ilikuwa haionekani kwenye rada za ACC maana yake ni kwamba transponder kwenye ndege ilikuwa imezimwa. Swali ni nani aliizima na kwanini aliizima??
Rada za jeshi mara nyingi zinakuwa na teknolojia ya SSR kama niliyoeleza hapo juu lakini pamoja na hiyo mara nyingi kunakuwa na nyongeza ya "Primary Radar" (Primary Surveillance Radar (PSR)). Teknolojia hii inafanya kazi kwa rada yenyewe kutupa mawimbi ya 'electromagnetic' angani na kisha mawimbi hayo yanakuwa reflected na kurejeshwa kwenye rada na hivyo kupata taarifa ya chombo hicho kilichopo angani.
Kwa hiyo baada ya Flight 370 kupotea kwenye rada za ACC ambazo zina teknolojia ya SSR pekee, rada za jeshi zenye SSR na PSR ziliendelea kuiona ndege hii katika vipindi kadhaa vya muda.
Muda ule ule ambao transponder katika flight 370 ilizimwa, rada ya jeshi iliona ndege hii ikigeuka na kupinda kulia. Kisha ikapinda tena kushoto kufuata uelekeo wa Kusini-magharibi.
Saa 01:30 sekunde ya 35 mpaka saa 01:35 rada ya jeshi la Malaysia ilioona ndege hii ikiruka katika altitude 35,000 ft kwenye magnetic heading 231°. Flight 370 iliendelea muelekeo wa Malay Peninsula ikibadili badili altitude kutoka 31,000 ft mpaka 33,000 ft. Baadae ikapotea kutoka kwenye rada ya jeshi la Malaysia.
Kwa "bahati mbaya" kuna rada ya kirai katika uwanja wa ndege wa Sultan Ismail Petra iliiona flight 370 mida ya saa 01:30 sekunde ya 37 na saa 01:52 sekunde ya 35. Iliiona flight 370 ikipita kusini mwa kisiwa cha Penang. Baada ya hapo ikapita eneo la bahari la Malacca.
Kwa hiyo taarifa zote hizi kutoka kwenye rada za jeshi la Malaysia zinatueleza kwamba sio sahihi kama ambavyo serikali inasema kwamba ndege ilidondoka saa 01:21. Ndege iliendelea kuwa hewani kwa zaidi ya masaa manane kutoka muda huo ambao serikali inasema kwamba ilidondoka.
Kwa hiyo hoja yangu ya kwanza nataka tuone kwamba ndege hii haikudondoka na nitaweka vidhibiti vingine hapo mbele kidogo lakini kwa sasa nataka tuangalia kwa ufupi sana hiki kitendawili cha pili cha kwamba "haijulikani ilipo".
Kwanza kabisa inashangaza kuona kwamba hakukuwa na "distress signal" yoyote iliyotumwa kutola kwenye flight 370 kama kweli ilikuwa inadondoka. Kama ndege ilipata hitilafu au labda kuna jambo lilitokea na kufanya labda ndege ianze kudondoka chini marubani walikuwa wanaweza kutuma distress signal katika frequecy ya kimataifa ya 121.5 MHz. Lakini labda tuseme kwamba hawakupata muda wa kutuma distress signal, lakini ndege hii MH370 ni aina ya Boeing 777 ambazo zimeundwa na mfumo maalumu wa kutuma distress signal automatically kama ikitokea imepata hitilafu na inakaribia kupata ajali. Ajabu ni kwamba yote haya hayakutokea.
Kama hiyo haitoshi…
Ndege zote za Boeing 777 zimefungwa vifaa maalumu vya ELTs (Emergency Locator Transmitters). Hivi ni vifaa ambavyo vinasaidia kujua ndege ilipo ikitokea imedondoka au imepoteza mawasiliano au transponder kuzimwa kama ambavyo ilitokea hapa kwenye flight 370. Ikitokea ndege imedondoka basi ELT inatuma signal kwenda kwenye satellite na kuonyesha mahali ndege ilipo. Mfano ndege hii ya Flight 370 ilikuwa na ELTs nne.
Ya kwanza iko kwenye cabin ambayo inatakiwa kuwashwa kwa mkono.
Mchoro kutoka kwenye Satellite ya jeshi la Malaysia ambao unaonyesha muelekeo wa Flight 370 baada ya transponder kuzimwa. (Rangi ya kijani ndio ndege yenyewe). Tazama hilo duara la bluu ambapo ndege ilipotea kwa muda kwenye satellite ya jeshi na baadae kurudi tena kabla ya kupinda kulia na baadae kushoto kwenye kusini magharibi
Mfano wa Antenna inayotumiwa na 'Secondary Radar'
(Video inagoma kupanda) Mfano wa 'Primary Radar' na namna inavyofanya kazi kwa kutupa mawimbi ya Electromagnetic angani
Mfano wa Transponder kwenye ndege
Ya pili iko kwenye fuselage ambayo yenyewe inakuwa activated automatically ikotokea ndege ikiwa inashuka chini kwa kasi isiyo ya kawaida (ikiwa inadondoka).
Ya tatu na ya nne ziko kwenye 'kwapa za mabawa' ya ndege ambazo zenyewe zinakuwa activated automatically ikitokea ndege imegusa maji au inakaribia kugusa maji (ikikaribia au kudondoka kabisa baharini). Ikitokea hitilafu na ndege kuanza kudondoka, vifaa hivi vinatoa signal na kupokelewa na satellite zizilizo kwenye mradi wa "International Cospas Sarsat Programme" na kisha 'location' ya ndege ilipo au ilipodondokea inakokotolewa kutokana na signal hizi. Ajabu ni kwamba mpaka leo hii bado hazijaonekana signal zozote kutoka kwenye ELTs za ndege hii. Kitu ambacho ni 'almost immposible'.
Nadhani unaanza kupata picha juu ya ukakasi unaolizunguka suala hili. Kuna kila dalili kwamba kuna mtu au kikundi cha watu kwa kutumia akili na weledi wa hali ya juu walipanga mpango maridhawa na kutekeleza tukio la kuipoteza ndege hii.
Nikurudishe nyuma kidogo… japokuwa imefanyika juhudi kubwa na 'watu wasiojulikana' kuhakikisha ndege hii kamwe haijulikani ilitua au kudondoka wapi… lakini kuna dirisha… dirisha la fursa ya kujua 'location' ya hii ndege ambako ilielekea. Na fursa hii tunaipata kwa kutumia data za satelite ambazo Flight 370 ilipokuwa inafanya 'handshake' kama ambavyo nilieleza.
Iko hivi… nilieleza kuhusu kifaa cha SDU kwenye ndege namna ambavyo kinafanya kazi ya kuwasiliana na satellite pamoja na ground stations. Sasa kifaa hiki cha SDU kwenye ndege kinafanya kazi sanjari na mfumo wa kifaa kingine kinaitwa ADIRU (Air Data Inertial Reference Unit). Kifaa hiki ndicho ambacho kinatoa postion ya ground station kwa ndege na pia kinatoa orintation ya ndege kwa ground station. Na ADIRU inakokotoa 'error rate signal' kutoka kwenye vituo hivyo ardhini. Kwa hiyo kinasaidia SDU kujua itumie satellite gani kufanya mawssiliano na ardhini itumie ground station ipi na pia kujua position yake ilipo kutoka ardhini (iko mahala gani).
Data hizi zote kwenye ndege zinahifadhiwa na kifaa kingine kinaitwa MDDU (Multi-purpose disk-drive Unit) na huku ardhini zinahifadhiwa kwenye ground station (kwa ndege hii ya flight 370 ilikuwa inatumia ground station ya Inmarsat iliyoko Perth, Australia).
Taarifa hizi za SDU na MDDU tunaweza kuzitumia kabisa kujua muelekeo wa ndege ya MH370 baada ya kupotea kutoka kwenye rada na ilielekea na ilitua mahala gani.
Swali, je tunaweza kupata taarifa hizi za SDU, MDDU kutoka kwenye satellite au ground station ya Pert, Australia hata kaama ni kwa kuzidukua?? Yes we can… Tukizipata tunaweza kufumbua kitendawili hiki?? Absolutely.!!
Kwa kutumia taarifa hizo, taratibu na kwa umakini tutachambua na kufahamu ndege hii ilielekea wapi na kutua. Na tukifahamu mahala ambako ilielekea inatupa mwanya wa kujua ni nani au akina nani ambao wako nyuma ya tukio hili. Na tukijua ni nani yuko nyuma ya tukio hili ndipo tutafahamu kwa nini ni Malaysia Airlines Flight 370?? Kwa nini sio ndege nyingine iliyokumbwa na dhahama hii…!!
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena