Waziri wa nishati Mh Medadi Kalemani amefanya ziara wilayani Rorya kwa kutembelea vijiji ambavyo viliachwa na mradi wa REA awamu ya pili na sasa REA awamu ya tatu kuvipatia umeme. Akiongea na wananchi wa kata ya Bukwe, Waziri Kalemani aliwahakikishia kwamba vijiji ambavyo vilirukwa na REA sasa vitapata umeme na vitongoji vyote. Amesema hakuna kuruka kitongoji hata kimoja katika kijiji ambacho kiko kwenye mradi wa REA amesema kila mwananchi anatakiwa kulipia garama za kuingiziwa umeme ambazo ni tsh 27000/= tu unafungiwa umeme . Akawahakikishia wananchi wa Kijiji cha Lolwe kwamba vitongoji vyote vitapata umeme.bila kujali kwamba viko umbali gani kwani lengo ni kila mwana nchi kupata umeme.amesema mkandarasi mwenye asili ya kihindi hatatoka nchini bila kukamilisha mradi huu kwani wamelipwa pesa na serikali miezi 5 iliyo pita na hawana sababu ya kuchelewesha mradi.
Waziri Kalemani akiongea na wananchi wa Bubombi na KIrongwe katika kata ya Bukura amewahakikishia kwamba lazima watapata umeme vijiji vyote na vitongoji vyote mpaka boda ya kirongwe ameagiza umeme ufike kwa ajili ya usalama wa nchi. Waziri alisema fursa zipo na kwamba ni vijiji vya mpakani ambavyo vinahitaji uwekezaji mkubwa kwa Sera ya sasa ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda ambavyo wananchi watakiwa kuanzisha viwanda vya kuchakata mahindi na kuuza sembe nchi jirani na kujipatia kipato. Mh waziri amempongeza Mh mbunge wa Rorya Lameck Airo kwa kuwabana Mawaziri kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ya Rorya, amesema kazi ya mbunge sio kupiga kelele bungeni ndo atapata Maendeleo kwenye jimbo lake Bali ni kumwomba waziri na kumweleza mahitaji ya jimbo lake kama anavyo fanya Mh Lameck Airo.
''Kwa sababu ya Mh Lameck kufuatilia kila wakati ndio maana mawaziri wanakuja kwa ajili ya kuwaleteeni Maendeleo'' Kuhusu kero ya maji katika wilaya ya Rorya waziri Kalalemani amesema serikali ya CCM ni moja atafikisha kilio hicho kwa waziri husika na ufumbuzi wake utapatikana. Akiwa ameambatana na Mh mbunge wa Rorya Mh Lameck Airo alipo ulizwa kuhusu shule ya Bukura ambavyo madarasa hayajakamilika mbunge Airo alitoa sementi 300 na mabati 100 kutoka katika mfuko wa jimbo ilikuonda shida ya upungufu wa madarasa katika shule hiyo.pia kuhusu bwawa ambalo aliahidi kuwachimbia wananchi wa Bukura mh mbunge Airo alimhakikishi diwani wa bukura Meshaki Mamba kwamba mwezi wa pili 2018 ataleta caterpillar kwa siku 7 ili lambo hilo likamilike na kuondoa kero hiyo ya maji. Mkuu wa wilaya ya Rorya Saimon Kemori Chacha alizungumzia zoezi la uandikishaji vitambulisho vya uraia NIDA katika ziara hiyo ya waziri katika kata ya Bukura alisema zoezi litakapo anza wanao ruhusiwa kuandikishwa ni RAIA wa Tanzania tu. akasema anajua kuna mwingiliano wa mpakani kwa RAIA wa nchi jirani litakuwa kosa kumwandikisha MTU asie RAIA wa Tanzania.kwahiyo watendaji na wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanaoandikishwa ni raia wa Tanzania tu sio vinginevyo. Kuhusu suala LA wavuvi wa Tanzania kuvamiwa na kunyang'anywa nyavu na watu wanaosadikika kuwa ni wa nchi jirani ya Uganda mkuu wa Mkoa wa Mara Adamu Kigoma Malina alisema yeye ndie mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa Mkoa suala hill litaisha kwani kwa sasa wanafanya taratibu za kufanya Doria ziwani na kupambana na maharamia hao na kwamba mpaka sasa vyombo vya usalama viko kazini.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena