Yawezekana umewahi kujiuliza sana, ni nani hasa aliyetoa wazo la hili jina tamu la nchi yetu. leo nimepitia sehemu mbalimbali kwenye mitandao na kufanikiwa kumpata mtunzi wa jina hili adimu.
Mohammed Iqbal mtunzi wa jina "TANZANIA" katika shindano la kutafuta jina la nchi baada ya Muungano mwaka 1964. Alikuwa mwanafunzi katika shule ya Aga Khan mkoani Morogoro, alisoma tangazo la shindano kupitia Daily News (zamani Tanganyika Standard)
Historia inasema walikuwepo washindi wengine (15) ambao nao walipata jina "TANZANIA" lakini 14 hawakuwepo siku ya kupewa zawadi.Mmoja aliyekuwepo hakuwa na barua rasmi ya ushindi toka serikalini (alisema barua ameipoteza), hivyo zawadi yote akapewa Mohammed Iqbal.
Jumla ya zawadi katika shindano ilikuwa Tshs. 200/=, kama wote 16 wangejitokeza kila mmoja angepewa gawio la Tshs. 12.50. Kutokana na kutojitokeza au kutokidhi vigezo kwa washindi wengine 15 Mohammed Iqbal alikabidhiwa zawadi yote ya Tshs. 200/= na ngao.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena