Kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwa siku ya tatu leo imeendelea kusababisha uharibifu wa miundombinu mingi ya jiji la Dar es Salaam kuharibika vibaya huku mingine ikifungwa kwa kushindwa kutumika hasa kwa magari yaingiayo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Modewji blog imeshuhudia maeneo kadhaa katikati ya jiji na maeneo mengineo ya nje ya jiji yakiwa katika ubovu mkubwa hata magari kupita kwa taabu na mengine kuzama katika madimbwi.
Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Magomeni, Jangwani, Mchikichini, Sinza, Tandale, Mwananyamala, Bamaga, Kigogo Tabata na maeneo mengine mbalimbali ya jiji huku yakijaa maji hasa mitaa na madimbwi yaliyo kwenye barabara hizo.
Hata hivyo, tayari Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, limetoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara kutoka maofisini mapema kufuatia baadhi ya barabara kujaa maji.
Kwa hali hiyo kumeongeza msururu mkubwa kwenye maeneo mengi ya jiji hasa yanayoingia na kutoka.
Kwa nyakati za asubuhi, barabara ya Bagamoyo hasa ile iliyokuwa ikielekea katikati ya jiji la Dar es Salaam, ilikuwa na foleni kubwa iliyoanzia Makongo hadi njia panda ya Mbuyuni na Salasala.
Taarifa ya Kivuko cha Mv Kigamboni kugoma:!
Awali Modewji ilipata taarifa za kivuko cha Mv Kigamboni kugoma kufanya kazi hali iliyosababisha umati mkubwa wa wananchi wa pande zote mbili wa Feri Ilala na wale wa Kigamboni Temeke kujazana kwenye eneo la kusubiria kivuko hicho wakiwa wasijue watavuka saa ngapi.
Hata hivyo, baadae taarifa zilieleza kuwa, Kivuko hicho kiliendelea na kazi zake pasipokueleweka tatizo hasa la awali lilikuwa ni nini?.
Gari likiwa limezama kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar na kupelekea watu kutoona vizuri mwanzo wa madaraja na mwisho wake.
Eneo la Magomeni mapipa baada ya barabara kufungwa.
Wananchi wakishangaa nyumba zilizofunikwa na maji maeneo ya Kigogo.
Barabara zikiwa zimefurika maji ya mvua na mitaro ya maji machafu.
Foleni ambayo haisogei.
Eneo la Jangwani likiwa limefurika na kupelekea kufungwa.
Jangwani.
Eneo la Mikocheni karibu na kwa Mwalimu Nyerere.
Barabara ya Mikocheni.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena