Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NEWS | MELI YA TANZANIA YAKAMATWA NA TANI TATU ZA DAWA ZA KULEVYA

Newspaper

Kwa mara nyingine, Jina la nchi limeendelea kuchafuka baada ya Meli ya MV Hamal iliyosajiliwa Tanzania kukamatwa Ulaya ikiwa imebeba shehena ya dawa za kulevya aina ya cocaine yenye uzito wa tani tatu, kama dawa hizo zingeuzwa mitaani nchini Uingereza zingekuwa na thamani ya Sh1.5 trilioni, kiasi ambacho nchi wafadhili zinatarajiwa kuichangia Tanzania kwenye bajeti ya mwaka 2015/16.
Mwaka 2013 meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa Tanzania ambayo ilikamatwa Septemba 2013 katika bahari ya Mediterranian, Italia wakati ikielekea Uturuki ikiwa na tani 30 za bangi zenye thamani ya Pauni 50 milioni za Uingereza (sawa na Sh125 bilioni).

Kiwango hicho cha dawa zilizokamatwa kimeweka rekodi ya ukubwa wa mzigo wa dawa hizo haramu zilizowahi kukamatwa Uingereza..
Upekuzi wa meli ulikuwa mrefu na unaosababisha maumivu, na uliofanywa na watu wenye utalaamu mkubwa wa kufanya kazi kwenye mazingira magumu”—alisema John McGowan, afisa mwandamizi wa Uchunguzi wa NCA.
Rekodi za mtandao wa shughuli za baharini unaonyesha kuwa katikati ya Februari, meli hiyo ilikuwa Uturuki na wiki mbili zilizopita ilianza safari kutoka visiwa vya Tenerife, Hispania.. ilipokamatwa ilikuwa inaelekea Hamburg, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ujerumani ambako ingefika jana usiku.
Meli hiyo imekutwa na watu tisa wenye umri kati ya miaka 26 na 63 wote raia wa Uturuki na wameshitakiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya

Post a Comment

0 Comments