Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akikata utepe kufungua maonyesho ya uwekezaji katika majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015. Makampuni na mabenki mbalimb ali yanashiriki kwenye maonyesho hayo.
Mkuu wa mkoa akisaini kitabu cha wageni cha Mfuko wa Pensheni wa PPF, kushoto ni afisa wa Mfuko huo anayeshughulikia masuala ya uwekezaji katika majengo, Godbless Robian.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akipatiwa maelezo na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, anayeshughulikia uwekezaji katika majengo, Augustine K Paul, wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea banda la Mfuko huo mara baada ya kufungua maonyesho ya siku nne ya uwekezaji katika majengo (DAR property Expo), kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015.
Mkuu wa mkoa akiangalia baadhi ya michoro ya majengo ambayo PPF tayari imewekeza kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akisikiliza kwa makini juu ya uwekezaji wa PPF katika majengo.
Theresia Woiso, (kushoto), akimpatia maelezo mwanzanchi huyo aliyetembelea banda la PPF.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwapatia maelezo wananchi kuhusu namna wanavyoweza kupata nyumba na jinsi walivyowekeza kwenye majengo waliotembelea banda la Mfuko huo.
Maafisa wa PPF, wakiwapatia maelezo ya kina wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo.
Wakazi wa Dar es Salaam, wakitembelea banda la PPF.
Mkuu wa Mkoa akitembelea banda la Nevada Properties, kampuni inayojihusisha na ujenzi wa majengo.
Mkuu wa mkoa akitembelea banda la benki ya Kenya Copmmercial Bank, (KCB), huku maafisa wa benki hiyo, EloiA. Msella, (kushoto), na mwenzake wakiwa tayari kumpatia maelezo
Mkuu wa mkoa akipatiwa maelezo na Mkuu wa masoko wa kampuni ya AVIC International Real Estate (T), Ltd, Linda Zhang, wakati alipotembelea banda hilo.
Mkuu wa mkoa akimsikilizaAfisa biashara mwandamizi wa kampuni nya Kilimani Industrial Automation Ltd, (KIAL), Shaban Issa, kuhusu mashine ya kumnyanyua fundi ujenzi kwenda juu wakati wa ujenzi wa majengo marefu ijulikanayo kama Aerial Work Platform (AWP-Machine), wakati alipotembelea banda hilo.
Meneja mikopo ya nyumba wa benki ya Stanbic, Bernartd Mfugale, (wapili kushoto), akimpatia maelezo ya namna ya kupata mkopo huo, Mkuu wa Mkoa Said Mdecky Sadick, alipotembelea banda hilo. Kulia ni Mercy Mosha, ambaye ni afisa wa benki hiyo.
Mkuu wa mkoa akipatiwa maelezo na Asha Shahabu, ambaye ni afisa mahusiano na wateja, wa kampuni ya Kopa Nyumba, wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena