Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TECHNOLOGY |Marekani Watengeneza Risasi Yenye Uwezo wa Kukata Kona na Kumfuata Mpigwaji!

Je unakumbuka kuona sinema ambazo watu wanakwepa risasi? Kama vile katika muvi ya The Matrix?

Katika maisha ya kawaida uwezo huo utaondoka hivi karibuni,  kitengo cha DARPA (Defence Advanced Research Projects Agency) kinachohusika na tafiti za kiteknolojia za kiulinzi/kijeshi kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza risasi ambazo zitaweza kufuta mtu aliyerengwa ata kama atakuwa kwenye mwendo kasi au kukimbia upande mwingine.

Risasi hizo zinaweza kufanya mabadiliko 30 ndani ya sekunde 1 ilikujihakikishia inafanikiwa kumfikia mlengwa. Na haya yote ni ikiwa kwenye kasi ya zaidi ya km 100  kwa saa.
risasi-teknolojia
“0.50 Caliber – ukubwa wa risasi inayofanyiwa majaribio”
Wanasema kwa sasa risasi hizo zitaweza pia kupunguza uwezo wa kukosa pale ambapo risasi imepigwa katika eneo la upepo mkali. Risasi hizo zitaweza kutoathirika na athari za kusogozwa au kusumbuliwa na upepo, bado zitaweza kupiga pale ziliporengeshwa.
Risasi
Risasi hizo zinaweza kufanya mabadiliko 30 ndani ya sekunde 1 ilikujihakikishia inafanikiwa kumfikia mlengwa. Na haya yote ni ikiwa kwenye kasi ya zaidi ya km 100  kwa saa.
Kwa sasa bado teknokojia hii inazidi kufanyiwa uchunguzi na maboresho zaidi na inasemekana kwa sasa tayari jeshi la Marekani limefuruhishwa sana na mafanikio yaliyofikika hadi sasa. Na inategemewa muda si mrefu risasi hizi zitaanza kutumika na jeshi la nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments